Vijana Kupata magonjwa ya zinaa na mimba za umri mdogo hutokana na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi na jinsia. Hii hupelekea kuyumba kwa mustakabali wa maisha ya vijana wengi. #MichongoEndelevu#O3plus
Je, wajua watu 85 kati ya 100 wanapata mimba ndani ya mwaka wakishiriki ngono isiyo salama.?
Kwanini upate mimba usiyoitarajia kwa kushiriki ngono isiyo salama...
#MichongoEndelevu
Vijana walio na mahusiano ya kingono na wenzi wengi huwa wana uwezekano mdogo wa kutumia kondomu,lakini pia wako katika hatari zaidi ya maambukizi mapaya ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa.
#MichongoEndelevu || #O3Plus
"Kati ya umri wa miaka 10 na 14 wasichana na wavulana wengi huanza kuona mabadiliko kwenye miili yao. Mabadiliko haya ya Kimwili na kihisia huchukua miaka kadhaa, hivyo ni kipindi sahihi chakuzungumza nao athari watakazokutana nazo kama watashiriki ngono."
#MichongoEndelevu
Ukosefu wa taarifa sahihi kuhusiana na afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kumechangia kwa kiasi kikubwa kwa vijana wengi kujihusisha na tabia hatarishi ikiwemo kujihusisha na mahusiano ya kingono katika umri mdogo. Tuwape vijana elimu ya afya ya uzazi.
#MichongoEndelevu