Ndugu Watanzania,
Kwa heshima na taadhima, ninawaandikia barua hii nikiwa mwenye uchungu wa kweli juu ya hatima ya nchi yetu. Sauti yangu ni sauti ya mamilioni ya Watanzania waliokata tamaa. Ni kilio cha taifa lililonyimwa haki, likakandamizwa kisiasa, na sasa likielea bila dira.Leo tunashuhudia kilele cha udanganyifu wa kitaifa unaoitwa uchaguzi. Kinachoendelea mbele ya macho yetu si uchaguzi, bali ni maonyesho ya kisiasa yaliyotengenezwa na CCM kwa ajili ya kudumisha utawala wake wa mabavu. Mfumo wetu wa uchaguzi umepoteza uhalali. Tume ya uchaguzi haijitegemei. Sheria zimejaa upendeleo. Na uhuru wa wapinzani unadhibitiwa kwa vitisho, vifungo, na masharti ya hovyo.
Katika hali hii ya giza, chama kikuu cha upinzani CHADEMA tumechukua msimamo wa kishujaa na wa kizalendo: “No Reforms, No Elections.”
Hakuna mageuzi, hakuna uchaguzi.
Hakuna tume huru, hakuna ushiriki.
Hakuna sheria ya haki, hakuna maana ya kura.Msimamo huu wa CHADEMA si wa ukaidi. Ni msimamo wa kulinda heshima ya wananchi, wa kupigania demokrasia ya kweli, na wa kusema ukweli kwa ujasiri wakati ambapo wengine wanaogopa.
Lakini kinachouma zaidi ni hiki: wakati CHADEMA wanasimama imara kwa ajili ya taifa, wimbi kubwa la watu — hasa vijana — linakimbilia kuchukua fomu za kugombea. Wengi wao hawana sera, hawana maadili, wala hawana dira ya taifa. Wanaona kutokuwepo kwa CHADEMA kama fursa ya kupenya bila ushindani. Wanadhani kuwa uchaguzi bila chama kikuu cha upinzani ni “mteremko wa kisiasa.” Hawajui kwamba wanashiriki katika kufunika kaburi la demokrasia. Na kilicho cha aibu zaidi ni kuwepo kwa baadhi ya vyama vinavyojiita vya upinzani vinavyoshiriki uchaguzi huu huku wakijua fika kuwa hakuna usawa, hakuna haki, na hakuna matumaini. Hawa si wapinzani — ni wasindikizaji wa watawala. Wamesahau wajibu wao wa kupigania haki ya wananchi. Wameamua kuuza heshima ya siasa kwa tiketi ya kugombea.
Sisi ndio tulipaswa kuwa mstari wa mbele kulinda msingi wa “No Reforms, No Elections.” Sisi ndio tungepaswa kulia na kudai tume huru. Tungepaswa kuandika, kuandamana, kuhamasisha na kushinikiza mageuzi ya kweli ya kisiasa. Lakini badala yake, tumekuwa mashabiki wa mfumo huu wa hovyo. Tumeingia kwenye siasa bila kusoma historia ya taifa letu. Tumejitosa kwenye uchaguzi wa aibu tukidhani kuwa siasa ni jukwaa la sifa na Fedha badala ya uwanja wa majukumu.
Nawauliza leo:
Je, ni ujasiri au ni ujinga kugombea uchaguzi ambao tayari umepangwa?
Ni uadilifu au ni tamaa kugombea pasipo haki wala sheria ya haki?
Na ni uzalendo au ni usaliti kushiriki uchaguzi ambao unawadhulumu mamilioni ya Watanzania kwa kimya?
Wito wa “No Reforms, No Elections” si wimbo wa CHADEMA peke yake. Ni wito wa kila Mtanzania anayejua tofauti kati ya haki na hila, kati ya uongozi na ulaji, kati ya siasa safi na siasa ya hovyo.
Watanzania wenzangu, huu si wakati wa vigeugeu. Si wakati wa kusubiri kufaidika kwenye mfumo uliopinda. Ni wakati wa kusema ukweli, hata kama ni kwa uchache.
Wito wangu, tuunge mkono kauli ya “No Reforms, No Elections” kwa vitendo, si maneno.
Tuwakemee vijana wanaogeuza siasa kuwa jukwaa la kutafuta umaarufu badala ya majukumu
Tuwalaani wapinzani bandia wanaosaidia CCM kudumisha mfumo huu wa mabavu.
Pasipo mageuzi, uchaguzi ni mzaha.
Pasipo uchaguzi huru, hatuna uhuru.
Pasipo ujasiri wa vijana, hatuna kesho.
Basi utasikia Jambo linaibuka Kuhamisha watu kwenye Kilichotokea Leo Kuhusiana na Kesi ya MH. LISSU, Kama Sio Wasanii basi Timu za Mipira hasa Simba na Yanga kama Kawaida yao.
Tumewashtukia Siku hizi sio WAPUMBAVU tena.
#FreeLissu#LissuSioMhaini#NoReformsNoElection
Waporaji wa HAKI za Wananchi wanajificha kwenye Kivuli cha AMANI, kwamba watu wakidai Haki wanataka kuharibu Amani.
Amani bila Haki ni Useless
Haki ndio huleta Amani, Usipotenda Haki unahatarisha Amani.
#NoReformsNoElection
@OlotuGasper@HecheJohn Mboga Mboga uwezo wenu wa Kufikiri ni mdogo sana, Kwani mikutano ni Lazima iwe ya Kampeni!? Mikutano ni haki ya Kikatibu muda wowote unafanya sio kipindi cha Uchaguzi tu. Pia Hebu jua Kuandika Vizuri ndio ulete shobo kwenye Post za Watu.