@EsirEid Umenena vyema!
Ukombozi wa nchi unahitaji mikakati zaidi ya hisia, lakini watu wengi wanaendeshwa zaidi na hisia kuliko uhalisia. Na hili hupelekea wao kuwaamini zaidi wale wanaoamsha hisia zao bila kujali kama mipango yao inatekelezeka.
Utashambuliwa sana juu ya andiko hili!
#TajiriLaKihaya
Watu wananiuliza,
“Tajiri, huu utofauti na wanaharakati uchwara umetokea wapi? Mbona mlikiwa marafiki tu?”
Ni kweli, binafsi nilikuwa nawakubali sana wanaharakati. Niliamini katika nguvu ya pressure ya wananchi, uwajibikaji wa viongozi na matumizi ya mitandao kuibua mambo ambayo wengi wanaogopa kuyasema.
Lakini nilipoanza kuona baadhi yao wakisema kwamba THE ONLY WAY ya kumuondoa CCM madarakani ni Marekani kuingilia Tanzania, mpaka wengine kumuomba Trump aje afanye Tanzania kama anavyofanya Iran au Cuba 😅😂, hapo ndipo nilipoanza kujiuliza, Hawa kweli wanaipenda Tanzania au wana agenda nyingine?
Mimi naamini mabadiliko ya Tanzania lazima yajengwe na Watanzania.
Mababu zetu walipigana kuondoa ukoloni. Leo tunataka kuwarudisha wakoloni kupitia mlango wa nyuma kwa kuomba mataifa ya nje yaje kutukomboa ? Hiyo kwangu ni contradiction kubwa sana.
Kama Marekani au Trump wangekuwa na nia njema kwa Afrika kuliko maslahi yao wenyewe, basi tungekuwa na mazingira tofauti katika nchi kama Uganda, Rwanda, Cameroon na nyingine ambazo zimekuwa na viongozi wale wale kwa muda mrefu.
Nchi kubwa hazina marafiki wa kudumu; zina maslahi ya kudumu.
Na historia imetufundisha kwamba nchi yenye nguvu ikija Afrika, mara nyingi inaangalia kwanza maslahi yake ya kiuchumi, kisiasa na kimkakati. Usipokuwa makini, unaweza kuondoa tatizo moja na kuingiza tatizo kubwa zaidi.
Na mimi siamini kwamba solution ya Tanzania ni kuomba foreign power itupangie mustakabali wetu.
Toka uchafuzi huu uishe, tumekuwa tukiona matamko mengi kutoka nje. Lakini swali langu ni rahisi,
WHAT NEXT?
mwaka Sasa unakata,ni nini hasa tumefanya sisi wenyewe kujenga nguvu ya kisiasa na kiraia ndani ya nchi?
Kama wanaharakati wanataka mabadiliko ya kweli, waambie Watanzania,
Tunatoka hapa kwenda wapi?
Tunafanyaje?
Tunawashawishije wale ambao hawakubalian nasi?
Na tunalindaje demokrasia bila kuigeuza nchi kuwa uwanja wa vita?
Ukijibu kila swali kwa tutapambana, na matusi kibao,hiyo si strategy.Hio ni hasira.
Na kinachonishangaza zaidi ni kuona baadhi ya watu wanaotumia lugha kali zaidi ya mapambano wakiwa nje ya nchi, huku watu waliopo Tanzania ndio watakaobeba consequences za kila hatua itakayochukuliwa.
Ni rahisi sana kusema tufanye hivi ukiwa mbali na uwanja.
Lakini mwananchi wa Tanzania akienda kazini kesho, watoto wake wanaenda shule, biashara yake inaendelea, kodi inalipwa,anataka kujua,
WHAT NEXT?
Tutaishia kulalamika mitandaoni mpaka lini?
Na tuseme ukweli mwingine ambao wengi hawataki kuusema,
Ikiwa kesho Lissu atafungwa, wananchi watafanya nini?
Ikiwa watu kama Polepole, Soka, Ally, Mdude na wengine wanakutana na mazingira magumu ya kisiasa, sisi tumefanya nini zaidi ya tweets, spaces, hashtags na matamko?
Kama hata mambo makubwa yakitokea,makamu wa rais, wiki Sasa hajaongea na hatujamuona,na taifa linabaki kimya, basi lazima tukubali kwamba tatizo letu si ukosefu wa tweets,tatizo ni ukosefu wa strategy ya kisiasa na nguvu ya taasisi.
Serikali inaendelea na kazi zake. Inajenga, inajipanga, inaimarisha mifumo yake.
Wakati huo huo sisi tunazidi kugawanyika, kutukanana na kutafutana wasaliti.
Hapo ndipo mimi ninaposema,
Sitaki activism inayotengeneza hasira na chuki bila strategy. Sitaki activism inayotegemea nchi za nje kutuletea uhuru. Sitaki activism inayowatukana Watanzania badala ya kuwashawishi.
Nataka activism inayojenga wananchi.
Nataka siasa inayojenga taasisi.
Nataka upinzani unaoweza kutoa alternative ya kuongoza nchi.
Na zaidi ya yote, nataka mabadiliko yatakayokuwa yamejengwa na Watanzania, kwa maslahi ya Tanzania.
Kama tunataka kubadilisha nchi yetu, tusisubiri Trump, Marekani, Ulaya au mtu mwingine aje kutufanyia kazi.
Tanzania ni yetu.
Mustakabali wake ni wetu.
Na jukumu la kuijenga ni letu.
“Should you find yourself in a chronically leaking boat, energy devoted to changing vessels is likely to be more productive than energy devoted to patching leaks.”
-Warren Buffett
@EduTalkTz Nadhani kama taifa hatujajua malengo yetu ni nini.
Ni kama tunataka kushindana kwenye soko la dunia na wakati huohuo tunataka kulinda utaifa wetu.
Matokeo yake tunatengeneza nguvukazi ambayo haiwezi kufanya vyote.
@hunchosmile@Nasibu_255@rayasel94 Mwanzoni mwa miaka ya 1800, watu weusi walikua ni sehemu kubwa ya POPULATION ya Argentina.
Maeneo kama CORDOBA, karibia nusu ya POPULATION ilikua ni watu weusi.
BUENOS AIRES watu weusi walikua ni takribani 30% ya POPULATION. Leo hawafiki hata 2%.
Unadhani wamepotelea wapi!