@EsirEid Leo Watanzania wote tutakuwa busy kujadili kuahirishwa kwa Match ya Yanga na Simba, vizuri Taifa hili halina mambo Mengine ya kujadili!!!!!!!! 🙌🙌
#TajiriLaKihaya
MWISHO MWEMA KATIKA UISLAMU…
Hakika bin Aadam hajui wapi atafariki wala hajui lini atafariki kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
[Luqmaan: 34]
“Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.”
Ikiwa hatujui tutakachokichuma kesho, jambo ambalo ni katika matendo yetu, basi hakika hatujui pia lini tutakufa kwani hilo ni katika matendo ya Allaah ('Azza wa Jalla).
Na ikiwa hatujui nchi (au mahali) gani tutakufa juu ya kwamba mtu anakwenda nchi (au mahali) anayoichagua mwenyewe, basi hakika yeye hajui lini atakufa.
Kwa hivyo basi, mahali pa kufariki na wakati wa kufariki haujulikani!
Tunamuomba Allaah Aturuzuku
husnul-khaatimah (mwisho mwema)
Na si muhimu mtu kufariki lini wala kufariki wapi.
Si muhimu ikiwa atafariki Makkah au Madiynah au atafariki nchi nyinginezo za Allaah na si muhimu akifariki siku ya Ijumaa au Jumatatu, au siku nyinginezo za wiki.
Hakika hakuna la muhimu isipokuwa jambo la muhimu ni katika hali gani mtu atafariki?
Hili ndilo la muhimu; atafariki katika hali gani? Je, utafariki ukiwa katika iymaan na ikhlaasw na tawhiyd?
Tunamuomba Allaah Atujaalie hayo yote (kufariki katika hali hizo za iymaan, ikhlaasw na tawhiyd).
Au je utafariki katika shaka na shirki na kufuru na ukanushaji?
Hili ndilo muhimu, hili ndio muhimu enyi Waislamu!
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mjue Allaah katika (hali ya raha) Atakujua ukiwa katika shida (au dhiki).”
Jambo kuu na la muhimu ni kujua mtu atafariki akiwa katika hali gani!
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamrisha kuwa tunapomaliza tashahhud zetu za mwisho katika Swalaah tuseme:
[Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) - Al-Bukhaariy (2/102), Muslim (1/412)]
“Allaahumma inniy a’uwdhu Bika min ‘adhaabil qabri, wa min ‘adhaabi jahannam, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil-Masiyhid-dajjaal “
Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako na adhabu za kaburi, na adhabu ya (Moto wa) jahannam, na fitnah ya uhai, na (fitnah) ya kifo, na shari ya fitnah ya Masiyhi-Dajjaal
Enyi Waislamu! Alimjia Malakul-mawt (Malaika anayefisha) kwa Nabiy Musaa ('Alayhis-Salaam) ili kumtoa roho yake. Malaika akarudi kwa Allaah kumwambia:
“Umenituma kwa mtu asiyetaka kufa bado.”
Allaah Akasema:
“Je anataka kuishi bado?”. Akajibu: “Ndio”.
Akasema (rudi umwambie) aweke mkono wake katika ngozi ya ng’ombe basi kwa kila unywele utakaokuwa mkononi mwake ndio itakuwa ziada ya umri wake”.
Malaika akamwendea Musaa ('Alayhis-Salaam) akamwambia hivyo. Musaa ('Alayhis-Salaam) akasema: “Kisha baada ya hapo?” Malaika akajibu: “Kisha mauti” Akauliza: “Kisha baada ya hapo?” Malaika akajibu: “Kisha mauti.
Kila nafsi itaonja mauti!
Musaa ('Alayhis-Salaam) akasema: “Basi bora nifishe sasa.”
Hivyo ni kwa sababu, vyovyote bin Aadam utakavyorefuka uhai wake (duniani), lakini pale inapomfikia mauti, ni kama kwamba hakuishi (duniani) isipokuwa saa moja ya mchana. Bali hakika Siku ya Qiyaamah itakapofika, itakuwa kama kwamba hawakuishi isipokuwa saa moja katika mchana (wa siku moja) kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
[Al-Ahqaaf 46: 35]
“Siku watakayoyaona yale waliyoahidiwa itakuwa kama kwamba hawakukaa (duniani) isipokuwa saa moja (tu) ya mchana.”
@Neto_Tanzania Haya Majitu yako vipi, watu tumepiga Interview zaidi ya 40 na zote hola tuko tunapambana na Maisha Mengine, yenyewe yanawaza tu Kupewa Ajira Shida walimu mlizoea Ajira za bure
Asanteni hatimaye nimefikisha 300K. Hizi ni jitihada za rafiki zangu ambao hu Retweet post zanugu. Leo nita follow kila atakaye Retweet post hii. Niinue na wengine.
@EsirEid Mimi naona hizi Simba na Yanga ni team Ambazo zipo kwa ajili ya kutudumaza Akili Watanzania, wiki nzima tunajadili hizo team, hivyo hatuwezi kuwa na Muda wa kutumia Muda huu kufikiri namna ya kujikomboa na Janga la Umasikini