Tangu mlipoanza kuua na kupoteza watu kwa lengo la kuwanyamazisha mpaka leo watu hawajanyamaza.
Infact upinzani dhidi yenu unazidi kuwa mkali mpaka raia watakapowaondoa.
Mlimteka, Mdude, Kipanya, Soka, Polepole,Ben Saanane na wengi kwa maelfu. Je mmefanikiwa kupendwa au kutia watu hofu?
Wenye akili wangeacha mbinu hii kwasababu imefail, kwasababu hamtumii akili mnazidi kuendeleza ujinga huu na kwa kweli hamtafanikiwa.
Mwisho wa ubaya huu itakua aibu na majuto makubwa kwenu na familia zenu.
Acheni ujinga wa kuteka na kuua watu.
POLE KWA WATANGANYIKA KWA KUADHIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUTOKUWA HURU.
Ameandika @Mwabuk2Boniface , Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS).
Tulipata Uhuru wa kutokuwa Huru.WATANGANYIKA kwa Mara ya kwanza tunaadhimisha Uhuru wa kutokuwa huru kwa kuwekwa kifungo cha hiyari cha kuto toka nje.
Tumefika hapa kwa viongozi kutowajibika na kuamini kwamba
1.Wao wanamiliki Ukweli
2.Wananchi wanawajibika kwa watawala.
3.kugeuza Cheo kama Mali ya Familia na siyo dhamana kama tulivyodanganywa kabla ya kusanuliwa na Gen Z ( Mbwa wa Waziri anakuwa Waziri wa Mbwa wote automatically ...Mtoto wa mtawala anakuwa mtawala wa watoto wote.
4.Wameshindwa kujibu hoja za GEN Z sasa wanazipiga rungu.
5.Kumbe wapigania Uhuru walipigania Uhuru wa kunyang'anya Uhuru wa Wenzao .
6.GEN Z wametuonesha kwamba nyumba haina nyufa tu bali ni kama Bonde la ufa.
7.Hivi ile Tume iliyopewa uhuru wa kuwa huru eti kutafuta chanzo cha uvunjifu wa Amani badala ya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu imeweka ratiba yake hadharanI kabla ya kuanza kazi? Imeitisha ushahidi na namba inavyoweza kufikiwa na wenye ushahidi?
8.HAKI,UKWELI NA UWAJIBIKAJI ndiyo suluhu ya haki ya kulitoa Taifa hapa tulipo.Tujue nini kilifanyika kabla wakati na baada ya uchaguzi.Ndugu zetu waliotekwa na watekaji wanarudishwa lini? Hatutakubali mambo ya funika kombe mwanaharamu apite.Kila jiwe lifunuliwe na ukweli udhihiri ili uwajibikaji ufanyike na Mengine ya fuate.
9.Maoni yangu TANGANYIKA ilifungishwa ndoa ya Utotoni na Zanzibar.Hivyo kwa sasa ilikuimarisha ndoa hii Tanganyika anahitaji kuulizwa ridhaa yake kesha kuwa mtu mzima sasa na kila akiuliza kuhusu uhalali wa mpango huu wa ndoa toka 1992 anapigwa chenga.Ridhaa yake ni Serikali 3 .Ya JMT,Serikali ya Tanfanyika na Serikali ya Zanzibar.
10.Tuache siasa za kizamani.Dunia imebadilika sana yale mapropaganda yetu ya alfu lela ulela hayafanyi kazi tena.Mtu ni Utu na kiongozi mwenye Utu hauwi watu...hupenda watu.Hulia nao wakati wa kulia na hucheka nao wakati wa furaha. Kiongozi anayependa watu huelewa shida yao na kuzingatia mahitaji yao na siyo Familia yake tuu.
TUJISAHIHISHE
Dear Nyerere, the Tanganyika you cherished is now a scary place for the sons and daughters of this land. They have even baptised it with a different name. But today as sons and daughters of the land we want back our land. May you continue to rest in peace while watching us.
Nani aliwahi kuwaza derby ya @SimbaSCTanzania na Azam kukosa mashabiki?
Siasa za kipuuzi, siaaa za mauaji, siasa za kishamba, siasa za chuki zinazotokana na uroho wa madaraka na ujinga wa watawala zinaharibu kila angle ya uchumi. Maeneo mengi uchumi unadorora.
Yo bro, niki meet friend jana kwa utani tu, ananipiga story hii , Lema, zamani, kama wife au girlfriend akikutafuta na akakukosa kwa muda, akija kukutana na wewe utasikia hii line , Endelea na uhuni wako tu, mimi sitazivumilia.’ Bro, hiyo ilikuwa old school vibe.
Lakini sasa? Ukikosekana hata masaa 3, hawa wanapiga polisi, wengine mochwari wanaku-track, na mwisho akamalizia, Mangi… this is f***ing life. Seriously bro, lazima tu push hii kitu ifike mwisho. Haiwezekani tena kuishi hivi.”
Kuna kitu hakipo sawa. Jana P.M. alitupa salamu za Pres. Jana ikazuka rumors anaumwa, jana hiyo hiyo viroboto wake wakapost picha yupo na Balozi wa U.S. Imekuja kugundulika ile picha ni ya 8th Oktoba!
“Yo 😤✨ stop all that shady energy vs me & Heche 🚫💀
Mbona mimi niko peaceful, nataka mema tu kwa country 🇹🇿❤️
God got me 💯🙏 japo najua sometimes namkosea kiboya 😅, lakini love yake iko strong sana kwangu 💖
Drop those fake stori’s & relax 🥴🍻 Wale jamaa wenu wakilevi na drama watawapoteza na kuwavuta mshiko kifara na hizo ripoti zao za kuandika wakiwa club na bottles za kuharibu brain na yada yada na english za Ki NGO🔥
Mkiendelea na uduansi, leo usiku nitamwambia My Dad Almighty God achomoke na mmoja wenu kabla ya vibes ya 2026 ⚡🙏 maana mmezidi evil plan juu yetu !!
Peace & good vibes only 🌟🫶”
Aliyetunga methali ya "sikio la kifo halisikii dawa" bila shaka alikuwa ameona jinsi mtu au watu wanavyoshauriwa kwa hekima na busara, lakini wakakataa kusikia kabisa kwa kuwa tayari wamefikia hatua ya mwisho ya uharibifu na kuwa tayari kuangamia bila kubadilika. Hata hivyo, bado hatujachelewa! Tuzibue masikio, tujisafishe mioyo na fikra, tusije tukafikiwa na maangamizi kwa kukaidi ushauri unaoleta haki na kuokoa nchi yetu.
Marekani imeanzisha Ushirikiano na Kenya katika masuala ya Afya, ambapo Marekani itaipa Kenya Tsh Trilioni 4 kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Afya. Marekani imesema inashirikiana na Kenya Sababu Kenya wana taasisi na mifumo Imara ya Kiserikali. Makubaliano yamefanyikia huko USA.