Kuanzia 20-23 Machi, 2025 Naivasha mbio kali za WRC Safari Rally! Pia Kenya ina vivutio vingi miji yakihistoria, tamaduni adhimu na fukwe nzuri. Waone @magicalkenya kupitia link: https://t.co/of6CnLDO7Z kwa taarifa zaidi
#WRC#MagicalKenya#TwendeKwaJirani#SafariRallyKenya2025
Anne Makinda kuna mda alikuwa anamruhusu Lissu tu kwenye agenda za kisheria...wabunge wengine wote walikuwa wanaambiwq watulie...tena anamuomba ushauri kabisa
Hivi tunatengeneza Utajiri au TUNAILISHA TU ALGORITHM?
Bongo kulikuwa na shida ya ajira kwa vijana.
Shwaaa boda boda zikamwaga vijana wanapiga kazi.
Hapa na pale Taxi gharama sijui kikaenda kikarudi. Bajaji zikajazwa.
Bado haikutosha. Kijana una IST au VITZ yako umetoka job saa kumi ile unaingia mzigoni.
Unawasha data kuna app fulani zinaitwa UBER au BOLT unafungua unaendela na kazi.
Wazungu wanasema hii ni “Tech Empowerment”.
Hizi App mbili zimewawezesha watu wa bodaboda, bajaji na gari ndogo kuzitumia kwa ajili ya biashara ya usafirishaji.
Ni mwaka 2026 sasa kuna swali niliwahi kuuliza na nauliza tena.
Je hizi apps kwa watumiaji (wamiliki wa vyombo vya usafiri) ni kweli zina faida ya kubadili maisha hata ukiwa na fleet of vehicles au ni digital feudalism ?
Ukiingia kwenye majiji Dar Es Salaam au Dodoma unakuta mida ya saa nne au tano usiku kijana jicho nyanya yupo kutafuta pesa.
Zaidi ya saa 15 kila siku mtu yuko mzigoni kutafuta ugali. Hakuna uhakika wakazi wala bima za afya.
Hizi apps kesho ikitokea zimezimwa nao ndo basi tena.
Kwa kila trip kupitia hizi app wanakatwa commission ya 25%. Unatoa gari/boda/bajaji unagharamia mafuta, service, na hatari yote barabarani kwenye barabara zetu hizi.
Ila bado kuna 25% moja kwa moja inaenda kwenye server fulani huko San Fransisco.
Boss wa huu mfumo ni algorithm fulani ambayo server ipo USA huko. Wakiamua kupunguza bei ya trip kwa kila kilomita wanapunguza tu.
Hapa mtu unabaki huna cha kufanya ni kufanya tu kazi masaa mengi zaidi.
Kwanini kusiwe na platform ambayo ni local hapa hapa Tanzania? Ambayo commission ni 5% mpaka 10% ili huyu mmiliki/dereva abaki walau na 90% ya jasho la kazi yake.
Wakati tukiendelea kusubiri taarifa ya Tume ya Uchunguzi wa machafuko ya 29 Oktoba na yatokanayo tukitumaini itazaa matunda bora na mapendekezo yake yatawezesha muafaka na maridhiano kuliponya taifa, ninashauri tubadilishane mawazo kwa kurejea Mapendekezo ya Tume ya Katiba ya Jaji Warioba. Jambo muhimu la kwanza ni kuamua MUUNDO WA SERIKALI ikiwezekana swala hili lipigiwe kura ya maoni ya wazi na isiyochakachuliwa na yeyote. Je ziwe serikali ngapi? 1 iliyopendekezwa na Watanganyika asilimia 13%?. Au 2 zilizopendekezwa na Wazanzibari 34% na Watanganyika 24%?
Au serikali 3 zilizopendekezwa na Watanganyika 61% na taasisi zote.? Au 4 serikali ya Mkataba (kati ya nchi 2 huru) zinazoshirikiana kiuchumi na kijamii yaani kijumuiya iliyopendekezwa na Wazanzibari asilimia 60%. Kwa kuwa mchakato wa kutengeneza katiba mpya Inshallah Rais kasema utakuja tujitayarishe kwa kujielimisha kwa hoja na mantiki. Tupeane mawazo na hoja za kuchagua ama serikali 1 au 2 au 3 au 4 hapa katika comments. ELIMU NDIYO ITATUKWAMUA
Tangu Hii nchi ipate Uhuru Hakuna Kipindi Ajira za Afya na Sector zingine zimetoka kwa Kasi Kama Kipindi hichi.
Nadhani Kila mtanzania anatakiwa kuwa proud na Uongozi wetu.
Tuwape sifa zao Kwa Namna wanapambana kuwatoa Vijana mtaani na Kwenye Ujobless..!!🙏👏👏👏
“Najifunza kila kitu ninachohitaji YouTube. Sihitaji elimu.”
Wametumia miaka mingi kusoma, wakaelewa, wakajua namna ya kurahishisha wanachojua, halafu wakakuwekea ‘clip’ YouTube ili uje ututambie elimu haina maana.
@EduTalkTz@MabalaMakengeza@depedrodeniss@EnoldKassedy Una maana gani unaposema nectaism. I thought shida kubwa ni mindset zetu kuhusu nini hasa maana ya elimu—na ndio maana nafikiri tatizo ni kubwa zaidi kwa Chuo Kikuu kuliko hata sekondari.
Leo Mwl. Christopher Mwakasege kasema kitu kikubwa sana "Nguvu kubwa inawekezwa kwenye kuwafundisha watu kuishinda dhambi na sio kuwapa watu maarifa juu ya pesa" This man of GOD🥹🙌🏾💒
Hujambo? Mnapungikiwa nini na mwenye dhamana na sekta niko hapa? Na mawasiliano yangu mnayajua vema je, zinapoanza hizo stori za rushwa huwa mnatoa wapi taarifa ili kwa pamoja tuwavizie tuwakamate mubashara? Kuna PCCB na kuna bango letu hapa chini na kuna namba yangu moja kwa moja sms 0765 345777.
Sasa tuache kulalamika, waleteni wababaishaji wote kwa wakati muafaka tuanze pamoja hadi tuwatie hatiani. Rushwa haikubaliki. Sawa ndugu?
Tunasoma habari za Yesu zinazoeleza alivyozaliwa, alivyokuwa na hekima akiwa kinda wa miaka 12 lakini hatuambiwi alikuwa wapi mpaka alipotimiza miaka 30. Katika kipindi cha miaka 30 hatusomi kokote Yesu alikuwa wapi akifanya nini.
Kuna wanaoita kipindi hiki ‘ukimya’ wakiamini kuna kitu kikubwa Yesu alikuwa anakifanya kimya kimya. Wengine wanasema Yesu alikuwa shule—maana ni wazi alijua kusoma na kuandika ingawa biblia haikuona sababu ya kutupa ufafanuzi. Wengine wanafikiri huo ‘ukimya’ ni kipindi Yesu anaishi maisha ya kawaida kama mtu mwingine yeyote. Kama ni kweli basi huenda majirani walianza kuamini kijana hana ‘maisha’ na huenda angeishia kurithi randa na misumeno.
Hata hivyo, tunachoweza kujifunza ni kwamba kile kipindi cha ‘ukimya’ tusichoambiwa chochote kumhusu, Yesu alikuwa akijiandaa na kazi kubwa itakayooneka kwa miaka mitatu tunayoijua. Yesu alihitaji miaka 20 ya ‘kupotea’ kuja kufanya kazi kubwa kwa miaka mitatu. Kile ‘kimya’ kiliibuka na mshindo wa kazi iliweka historia kwa miaka zaidi ya 2000.
Elimu yetu imekuja kuwafanya wale waliokuwa vipanga kuwa desperate na maisha.
Vipanga wengi wamekuwa watu wenye huzuni sana, elimu imewapa matunda yaliyooza na hawajui watamuuzia nani.
Mitaa inawacheka, familia zinawalaumu na jamii haijali kuhusu wao.
Wengi wamepoteza matumain
3. THE FEARLESS ORGANIZATION
Unatumia raslimali nyingi kuajiri watu wenye uwezo mkubwa lakini unawanyima fursa ya kutumia uwezo wao. Kwa nini? Nini hufanya watu katika taasisi kuogopa kusema mawazo yao, kushindwa kuuliza maswali muhimu na kuogopa kabisa kutoa ushauri ambao ungeweza kuisaidia taasisi kujifunza, kujirekebisha na hata kukuza ubunifu?
Kitabu hiki, kwa kutumia tafiti na visa halisi, kinaelezea namna gani tabia za viongozi huchangia kufanya watu wenye akili na uzoefu kunyamaza, wakiogopa kutoa uzoefu wao na wakati mwingine kukunja mikono hata katika mazingira ambayo mambo yanaharibika.
Kitabu kinafafanua maana ya ‘woga’ na namna unavyojitokeza katika mazingira ya kazi na kisha kuonesha hatua zinazoweza kuondoa utamaduni wao woga katika taasisi. Kubwa nililojifunza ni kwamba, kimaumbile, woga ni akili. Watu kunyamaza na kushuhudia mambo yaende vile yanavyoenda kunamaanisha wanajihami na kiongozi wao—na hii haiwezi kuwa dalili nzuri kwa kiongozi. Kama kuna sifa muhimu anayoihitaji kiongozi ni uwezo wa kuwafanya watu waamini ni salama kusema.
Hata hivyo, kitabu hiki hakijaeleza kwa nini viongozi hufikia kuona ni bora watu wanyamaze kuliko kuambiwa ukweli wanaouhitaji kukuza taasisi zao. Kitabu hiki kinamfaa yeyote anayetamani kuchukua hatua za kugeuza woga kuwa ujasiri. Kama wewe ni kiongozi, huenda mwaka huu unahitaji kusoma kitabu hiki.