NAPOLEON HILL
anajibu hili swali kupitia kitabu hiki👇
"Kwa nini baadhi ya watu wanafanikiwa sana huku wengine wenye uwezo unaofanana wakibaki nyuma?"
Tutakichambua hatua kwa hatua huenda tukajifunza jambo katika haso zetu
Na mchambuz wako Mr cleansheet
Mchambuzi msomi
🧵 uzi
MWANAUME asiye na MAARIFA anaweza kuwa na pesa leo, lakini akakosa uwezo wa kujenga kesho.
Tafsiri ya mwanaume kuwa kichwa cha familia ni kuwa na MAARIFA.
Kichwa kikikosa mwelekeo, familia nzima inalipa gharama.
Wekeza sana KICHWANI bro..
Huduma ya kuziba na kurekebisha meno yaliyovunjika, kutoboka au kuoza, kwa lengo la kurejesha muonekano na matumizi ya jino.
-Hurejesha umbo la jino
-Huboresha muonekano wa tabasamu
-Husaidia kurejesha uwezo wa kutafuna
-Huzuia tatizo kuendelea
Karibu Tukuhudumie 🦷✅😁
Kijana Akaniambia “kaka naenda kwenye interview Lakini najua kazi sitapata” Nikamuuliza kwa nini unaenda na unajua fika hutapata. Alinijibu “nabahatisha”! Lakini mimi nilishamsoma ni mtu mwenye uwezo mkubwa tu. Nikamwambia chukua simu yangu; kisha Nipe majina yako. Nikamwambia Hii kazi utapata na ukipata nipigie simu. Kisha Nikamwambia hakikisha unafaulu mtihani. Hapa Nilikuwa nampa moyo ili tamaa aliyokwisha kuijenga isimfanye akafeli na mtihani. Yule kijana Bahati nzuri alipata kazi ile na simu ya kwanza ikaja kwangu. “Kaka nashukuru kwa kunipambania” aliongea kwa furaha. Nikamwambia umejipambania mwenyewe na Mungu wako; sasa kachape kazi.
Bro to bro
Mara moja moja, tembelea Divorce Court, na ufatilie Divorce case,
Hakuna mwanamke analilia upendo wala kujenga familia,
Wanacholilia ni kuondoka na Mali za Mwanaume, na kumuacha Mwanaume akiwa kwenye Great Economic Depression. Na sababu ingine ni Child support, hivi we kwenye ukuaji wako Ni mara ngapi ushawahi ona Watoto wanasaidia baba zao.
Bro hizo hela Kula, kuwa mnufaika wa kwanza wa Jasho lako,
Hata sijui majaji wa kesi ya Lissu wamelalaje uko waliko! Nimepitia majumuhisho (final
Submission ) kesi ya Lissu, haaaa no this guy is gifted! Watamhukumu kunyongwa hadi kufa kisa alisema ‘tutakinukisha, tutavuruga uchaguzi’….hilo tu ndo wataweza!
Daktari Bingwa na Dada wa Kitawa, Sr. Dkt. Sarah Kahumbya Deogratius, ambaye ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Kardinali Rugambwa, Tanzania, ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Else Kröner Fresenius ya Ushirikiano wa Maendeleo katika Tiba kwa mwaka 2026.
Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha utambuzi na huduma za kifafa kwa watoto wenye ulemavu nchini Tanzania.
Tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka na Taasisi ya Else Kröner- Fresenius-Stiftung (EKFS), inalenga kutambua watu na miradi yenye mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya katika nchi zenye rasilimali chache.
Kwa mwaka 2026, tuzo hiyo imejikita katika huduma kwa watu wenye ulemavu na ina zawadi ya Euro 250,000, sawa na takribani dola za Marekani 286,975.
Taasisi hiyo imemtangaza Sr. Dkt. Deogratius kuwa mshindi wa mwaka huu kupitia mradi unaolenga “Kuimarisha Utambuzi na Huduma za Kifafa kwa Watoto wenye Ulemavu nchini Tanzania”, baada ya kupendekezwa na Evangelisches Krankenhaus Alsterdorf (EKA), taasisi ya afya kutoka Ujerumani.
Sr. Dkt. Deogratius ni Mtanzania, Dada wa Kitawa wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu la Jimbo Katoliki la Bukoba, daktari wa tiba na mtaalamu wa afya ya jamii, ambaye ameunganisha wito wake wa kitawa na taaluma ya udaktari pamoja na uongozi katika sekta ya afya.
Ana Shahada ya Udaktari na amefanya masomo ya uzamili katika afya ya jamii na tiba ya magonjwa ya ndani. Pia amesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika.
Tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Kardinali Rugambwa jijini Dar es Salaam mwaka 2016, Sr. Dkt. Deogratius amehusika katika kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika hospitali hiyo, ikiwemo kuboresha huduma za uchunguzi, uendeshaji wa famasia na huduma za tiba za kibingwa.
Chini ya uongozi wake, hospitali hiyo imeendelea kujenga uwezo wa kutoa huduma kama kituo cha rufaa cha kikanda, huku kazi yake ikipanuka pia katika kuwahudumia watu wenye ulemavu, hususan watoto na watu wazima wanaoishi na kifafa.
Ushirikiano kati ya Hospitali ya Kardinali Rugambwa na Evangelisches Krankenhaus Alsterdorf ya Hamburg, Ujeruman
Katibu mkuu John Mnyika ametokwa na machozi hasa pale Tundu Lissu aliposema kama mnanifanyia hivi Mimi mjuzi wa Sheria mmeniweka Gerezani Mwaka mzima kwa makosa ya uongo.
Vipi kuhusu watanzania wasiojua
Tundu Lissu "Kama mnanifanyia hivi mimi mjuzi wa Sheria, mmeniweka gerezani Mwaka mzima kwa makosa ya uongo."
"Vipi kuhusu Watanzania wasiojua Sheria?" 😭
So pain 😭😭
Askofu Dkt. Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo Kuu la Karagwe, amesema kuionya KKKT kwa madai ya kutonyosha kidole kwa Serikali ni matumizi mabaya ya maonyo.
Askofu Bagonza ameyasema hayo leo Jumamosi, Septemba 26, 2026, kupitia ukurasa wake wa Facebook, akisema KKKT haijawahi kuinyoshea Serikali kidole, hivyo kuionya kwa kutonyosha kidole kunaonyesha matumizi yasiyofaa ya maonyo.
Amesema kutonyosha kidole kwa KKKT hakumaanishi kanisa hilo halina kidole, bali limekumbushwa uwepo wa kidole hicho.
Aidha, amesema KKKT kukosa kidole cha kunyosha au kuogopa kukinyosha hakumaanishi Serikali inakihofia kidole cha KKKT kuliko vidole vingine.
“Kuionya KKKT ambayo haijanyosha kidole ni sawa na kuwafokea wasiokuja kanisani kwa kuwatumia waliokuja kanisani. Ni matumizi mabaya ya maonyo,” amesema.
Askofu Bagonza pia amesema kunyosha kidole na kuogopwa kiasi cha kusababisha wasiokinyosha nao kuonywa, ni sifa njema kwa aliyekinyosha, huku akitoa wito kwa waumini kutogawanywa na Serikali au wale wanaonyosha kidole.
“TUSICHONGANISHWE na Serikali au na wanaonyosha kidole. Tunanyoosha kwa zamu. Tusiponyosha ni juu yetu na Mungu; si juu yetu na Serikali,” amesema.
Katika ujumbe huo, Askofu Bagonza amehitimisha kwa kunukuu Biblia, Luka 12:20, inayosema: “Bwana akamwambia yule mjaluo, ‘Mpumbavu we, usiku huu Bwana anataka roho yako.’”
Yani kwa Kauli na MAELEZO haya ya Mh. Lissu hii KESI imeishia hapa......
Waliitwa kina CDF, IGP wakachimba, Sasa serikali ilitishika vipi kama VIONGOZI hao walishindwa kutoa Ushahidi wa namna walivyotishika ?
Hii kesi imefia hapa....🙌🙌
#FreeTunduLissu