Advocate, specializing in litigation & civil law | Legal expertise across Dar es Salaam & Dodoma | Committed to justice, integrity, and client advocacy.
Kwa wale wenye tabia ya KUSIMANGA MAWAKILI, tambueni kwamba; kwenye mfumo wa HAKI JINAI, tatizo ni DPP na POLISI na SIYO MAWAKILI. Msikilizeni Rais MAGUFULI 👇. Punguzeni UCHAKUBIMBI 😂😂
Leo tunaanza kusikiliza kesi ya maombi ya kumuondoa Uwakili Rais wa TLS Mwabukusi, kwa kwasbb ya kauli ya wito wa Mawakili nchi nzima iliyopitishwa kwenye AGM juu ya kutaka kuachiliwa kwa wakili Tundu Lissu.
Kama kawaida tuko pamoja na mawakili nchi nzima kusimama na Rais wetu
Kanuni ya 5 ya Kanuni za MAADILI YA MAAFISA WA MAHAKAMA (G.N. No. 1001 of 20/11/2020) Inahusu USAWA (Equality). Leo baadhi ya MAJAJI na MAHAKIMU wanawabagua WANAHARAKATI na kuwaona kama WAHALIFU. Huo ni UTOVU WA MAADILI.
Baada ya RAIS MKAPA kupanda Kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi - Kisutu kutoa ushahidi kwenye Kesi ya Profesa Mahalu, pengine Nchi inaweza kushudia Mtu mwingine kutoka kwenye Mhimili wa Nchi, JAJI MKUU, akikwea Kizimbani kutoa ushahidi Kesi ya Wakili Madeleka. Ngoja tuone.✍🏽
Nimeshangaa sana kuona GERALD HANDO na wenzake, “WAKUCHAMBUA MAGAZETI” kwa namna ya KUSHABIKIA UOVU aliofanyiwa KAZUNGU na MADHILA aliyopitia MADELEKA. Hivi HANDO ungekuwa ni WEWE umeumizwa MAKALIO, ungechambua gazeti kwa KUSHABIKIA UNYAMA huo?
Katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna kesi kubwa tano (5) zinazohusika na mashtaka ya uhaini zilizowahi kufikishwa na kusikilizwa katika Mahakama za Tanzania. Nitawapitisha
1.Kesi ya Uhaini ya 1970 (Tanganyika)
Walioshtakiwa walituhumiwa kupanga njama za kuipindua serikali ya awamu ya kwanza iliyokuwa inaongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kumrejesha madarakani Oscar Kambona
Katika Kesi ya Uhaini ya mwaka 1970 (Republic v. Grey Likungu Mattaka and 6 Others), jumla ya watu 7 walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kupanga njama za kuipindua serikali
Upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 22 na vielelezo 118. Barua, kanda za sauti (tape recordings), nyaraka za kibenki zikionyesha miamala ya kifedha iliyodaiwa kutoka kwa Oscar Kambona
2.Kesi ya uhaini ya 1973/1974 (Zanzibar);
Kufuatia mauaji ya Rais wa Kwanza Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, 07 Aprili 1972. Abdulrahman Mohamed Babu na wenzake 80 walishtakiwa. Kesi hii ya uhaini ilikuwa na mashahidi zaidi ya 50
Mashahidi walihojiwa mbele ya Mahakama Maalum ya Zanzibar. Mahakama ilitoa hukumu ya kifo kwa washtakiwa 34 (baadhi wakiwa mahakamani na wengine in absentia, akiwemo Babu)
Nyerere alikataa kuwarejesha Za’bar akihofia wangenyongwa bila kupata ya kusikilizwa. Ushahidi mkubwa ulitegemea maelezo na nyaraka za kiusalama zilizokamatwa wakati wa msako
3.Kesi ya Uhaini ya 1983–1985 (Tanganyika)
Kesi hii ni kufuatia jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililoshindikana Januari 1983 dhidi ya iliyokuwa serikali ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kesi iliendeshwa mbele ya Jaji Nassor Mzavas
Washtakiwa walikuwa ni Kapteni Hatti Maghee, Kapteni Christopher Kadego, Kapteni Vitalis Mapunda, Zacharia Hans Pope, Pius Lugangira (Uncle Tom) na raia kama Christopher Ngaiza
Kesi hii iliweka rekodi kwa kusikiliza mashahidi 133 na kuwasilisha vielelezo 225, ikijumuisha silaha, ramani za kijeshi (ikulu na uwanja wa ndege), zana za mawasiliano (radio za upepo, nyaraka za siri
4.Kesi ya Uhaini ya 1997–2000 (Zanzibar)
Viongozi na wanachama 18 wa CUF walikamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uhaini, wakituhumiwa kupanga njama za kuipindua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Salmin Amour
Kesi hii haikufikia hatua ya kusikiliza mashahidi au kuwasilisha vielelezo mahakamani. Mchakato uliahirishwa mara nyungi miaka mitatu (1997–2000) kupisha upelelezi na mabishano ya kisheria
Novemba 2000, kabla ya mashahidi wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wa Zanzibar alitumia mamlaka yake kisheria kufuta mashtaka yote (nolle prosequi)
5.Kesi ya Uhaini ya 2025-2026 (Tanganyika)
Katika kesi inayomkabili Tundu Lissu, upande wa Jamhuri unadai kauli alizozitoa kuhusu kuzuia uchaguzi zililenga kuvuruga uendeshaji wa uchaguzi na kupindua au kuzuia mamlaka ya Serikali
Kesi inasikilizwa Mahakama Kuu Tanzania (Masijala ya Dar es Salaam) chini ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde
Upande wa Jamhuri ulipanga kuleta mashahidi 30 na vielelezo 11. Hadi wanafunga ushahidi wao, Jamhuri hawajaleta kielelezo chochote katika kutetea ushahidi wa mashahidi wao hao 17
Kielelezo cha upande wa Jamhuri ilikuwa ni video kutoka ‘Jambo TV’ Tundu Lissu akizungumza hadharani na watia nia CHADEMA. Kielelezo hicho kilikataliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania
Maajabu katika kesi hii ya uhaini
Tundu Lissu anashtakiwa pekee yake katika uhaini. Tundu Lissu anashtakwia kwa kusema maneno bila kula njama na vitendo. Hii ni mara ya kwanza kwa kesi ya uhaini kuwa na mshtakiwa mmoja
Ili mahakama iseme kuna kesi ya kujibu, sheria inataka upande wa mashtaka uwe umeweka msingi thabiti unaoonyesha vipengele vyote vya kosa (ingredients of the offense) vimetimizwa
Tusubiri hiyo 21 August 2026, Jopo la Majaji litaamua nini. Kama kutakuwepo na kesi ya kujibu (Prima Facie Case) tutashangaa sana. Tutasubiri kusikia wametumia misingi gani ya kisheria
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.