Kuna nyimbo nikizisikia huwa zinanikumbusha mbali sana, Lakini kwa miaka yote huwezi wataja malegend wa muziki upande wa wanawake bila kumtaja lady jaydee "angelic voice" ana sauti unique inayoweza kuyatoa majini baharini🙌🙌
ARUSHA: Joseph Mrindoko ambaye ni mmoja wa 'memba' wa Kundi la Wachokonozi ameyasema hayo katika mahojiano na Mtangazaji Khalifa Said wa The Chanzo, Julai 30, 2026.
Zaidi https://t.co/M0f2lXswbC
#JamiiForums#Uwajibikaji#HakiZaBinadamu
Salamu Maria umejaa neema. Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Naye Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu. Utuombee sisi wakosefu. Sasa, na saa ya kufa kwetu, Amina🙏
CAF is probably waiting to see which direction the wind is blowing before pretending to be disgusted by what FIFA president is doing. They’re corrupt to the core. The biggest threat to Football after infantino is CAF.
Anaandika Wakili @Advocate_Kisabo
Leo, Julai 27, 2026, nimemtembelea Mhe. Tundu Lissu Tundu Antiphas Lissu Gereza la Ukonga. Mbali na kunipa maelekezo kuhusu maandalizi ya nyaraka za submissions katika kesi yetu, kufuatia kukamilika kwa maswali ya dodoso Julai 23, 2026, Mhe. Lissu amesisitiza kwamba watu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashitaka ya ugaidi wanapaswa kupata uwakilishi wa kisheria na kutembelewa mara kwa mara magerezani ili kuwafariji, kufuatilia ustawi wao na kujua maendeleo ya kesi zao.
Amenieleza pia kwamba hakuna hata mmoja anayepaswa kusahaulika, wote wanapaswa kutetewa na mawakili.
Nilienda na Wakili Deogratias Mahinyila Deogratius Mahinyila lakini hakuruhusiwa kuingia baada ya maafisa wa Magereza kudai kuwa jina lake halipo kwenye orodha ya mawakili wanaoruhusiwa kumwona Mhe. Lissu.
Mhe. Tundu Lissu anawasalimieni sana Watanzania. Pokeeni salamu zake.
REPOST 200
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amebainisha kuwa ni vigumu kwa mtetezi wa amani kuwa adui wa haki, au mtetezi wa haki kuwa adui wa amani, kwani mambo haya mawili yanategemeana.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania @thrdcoalition unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Julai 24, 2026, Dkt. Nchimbi amewahimiza Watanzania kuacha kuogopa kutamka neno haki kwa sababu maneno yanazaa matendo ya kuitekeleza haki hiyo
Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa anatamani kuona Tanzania ambapo kila mwananchi anajisikia fahari ya Utanzania wake, amani, na usalama akiwa ndani ya nchi yake. Amesema ingawa kuna utofauti wa itikadi za kisiasa, dini, na makabila, ni muhimu Watanzania watambuane kwa utaifa wao kwanza ili kila mmoja awe na hamu ya kuchangia maendeleo ya nchi.
"Naomba mtoke hapa mkijua kwamba fursa tumeipata ya kupata Katiba mpya kabla ya 2030, kupata katiba mpya ambayp itatumika mwaka 2030 katika uchaguzi Mkuu. Narudia kutumia maneno magumu tukomae hapo. Na ninaongea na wapinzani wote, naongea na CCM, Naongea na upinzani, naongea na asasi za kiraia nawaambia wanaCCM Katiba mpya ni kwa faida ya vizazi vijavyo, nawaambia Vyama vya upinzani kuwa Katiba mpya ni kwa faida yenu, watoto wenu, wajukuu na vizazi vijavyo. Nawaambia asasi za kiraia kwamba Katiba mpya ni kwa faida ya Nchi yetu, tupigane wote kupata Katiba mpya."
.... Tukishafika hapo, kasi ya maendeleo na mabadiliko kwenye nchi yetu itakuwa kubwa kuliko tunavyofikiri. Tukishaanza kuogopa kusema haki ni msingi wa amani, unaanza na kuona haya kutekeleza haki, maneno yanazaa matendo,tunapoanza kutamka maana yake tunaanza kuelekea kwenye kulitekeleza, hakuna mashindano ya nani anaanza, haki ni msingi wa amani. Haiwezekani mtetezi wa amani akawa adui wa haki au mtetezi wa haki akawa adui wa amani, halifikiriri na ni jambo muhimu la kujiepusha nalo." Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.