@1960Remija Tuna jamii ambayo haitaki kuelewa na kuukubali ukweli! Tuna jamii kubwa ya wapenda mpira ambayo inapumbazwa na ‘wachambuzi’ wetu wanaoamua nani anafaa na nani hafai. Suala la uwanja ni la kiufundi zaidi kuliko matamko na picha! Watanganyika hawakubali jambo hilo!
@1960Remija Wachambuzi wanatoka mashimoni sasa na picha za uwanja na maneno mengi ya hadaa. Lakini hakuna kati yao anayetaka kujadili ubora wa eneo la kuchezea kwa kutumia data, isipokuwa picha tu. Kama nchi, tumetia aibu na itakuwa na maana kama watu watawajibishwa
Suala la uwanja sio picha na mpangilio wa viti, isipokuwa ubora wa sehemu ya kuchezea. Hapo ndipo hasa hoja ya CAF inapokuja. Mnaoijiita wachambuzi mnapotosha Watanzania kwa kuonyesha picha tu, ni nani kahakiki ubora wa eneo la kuchezea mpaka mnataka mechi ichezwe hapo??
BENJAMIN MKAPA imejengwa Kwasababu ya Simba Sports historia haiwezi Kusahau hii
Na Simba wameifanya Lupaso iwe ngome tishio (Fortless) na haipo team Africa inajisikia vizuri Kukutana na mnyama Lupaso.
RS Berkane wamepata mchecheto,Lakini bahati mbaya huu ni wakati wa mnyama
@1960Remija Kuna tatizo kubwa sana kwenye nchi hii ambalo linaletwa na ‘ujuaji wa kisiasa’. Hatutaki kuheshimu taaluma za watu, ila tunaridhishwa na maneno tu. @MsigwaGerson anatetea kibarua chake, hakuna wakati atasema uwanja una mapungufu sasa hivi sio kidogo.
@1960Remija Unachofanya ni kuonyesha ni kwa kiasi gani wamekosa weledi. Unawaumbua. Jambo ambalo limetawala kila ukurasa wa ‘social media’, jambo kubwa kama hili lenye maslahi kwa taifa, inawezekana vipi wachambuzi wasiandike au kulifanya kama hoja kuu kwenye majukwaa yao? Unawaumbua sana!
@ezekiel_kamwaga Kwanini tumekua wepesi zaidi kulaumu CAF na Berkane na sio mamlaka zetu ambazo ni chanzo cha tatizo? Kwanini tunatafuta huruma zaidi kuliko kuwajibisha waliosababisha tatizo? Hata kwenye hili tunataka ‘busara’ zitumike? Why? How? Huu sio uzalendo, ni ujinga bro.
@INFLUENCERjr Hata akiwa mkali, bado ataonekana wa kawaida kwa sababu ya viwango alivyofikia baba yake. Kila atakachofanya ataonekana ‘wa kawaida’ kwa sababu ya historia ya baba. Kila la heri kwake.
Mzee @jmkikwete anapoongea huchoki kumsikiliza. Ni msimulizi mzuri wa matukio mbali mbali, anayapangilia matukio kwa namna ambayo inakufanya uendelee kumsikiliza. Ni wajibu wetu kama vijana kuwaangalia wazee hawa kwa namna hiyo na kujifunza kwao.
@KukudiT@Sativa255 Mpaka mwaka 2000 matokeo ya darasa la 7 yalikua yanabandikwa ofisi za Halmashauri ya Wilaya, Mji au Mkoa. Haijalishi unatoka mbali kiasi gani, ili kujua kama umefaulu ilikua lazima uwe na ndugu Karibu na ‘Bomani’ akuangalizie matokeo yako au uende kule. TZ hii imetoka mbali!
@Chizzodrama Niliwahi kununua Album moja tu ya msanii wa nyumbani - AKA Mimi ya Ngwair. Hii Nadhani ilikua 2002 au 2003. Na nilikua nikienda shule, naificha uvungu wa kitanda. Za nje, nilinunua copies nyingi kiasi - Backstreet Boys, Westlife, Boyz 2 Men, R. Kelly, Joe Thomas, Craig David etc.