British Airways kurejea Tanzania si habari ya kutazamwa juu juu. Wachambuzi kama Fredy Naftali Dk. Philip Daninga na wameangazia faida zake kwa utalii, biashara, ajira na fedha za kigeni. Pia Neil Chernoff wa British Airways ametoa mtazamo wa kampuni. Uchambuzi umezungumza. ✈️🇹🇿
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mama yetu, Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kilichotokeo leo tarehe 21 Septemba, 2026.
Kifo chake ni pengo kwa familia na Taifa kwa ujumla, kwani alikuwa sehemu muhimu ya historia adhimu ya Zanzibar kuanzia wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mapinduzi Matufuku ya Zanzibar na kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Daima tutaendelea kukumbuka, kuenzi na kuheshimu mchango wake katika kuhifadhi kumbukumbu na urithi wetu, pamoja na kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Taifa letu.
Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, familia ya Hayati Sheikh Karume, ndugu, jamaa, marafiki, wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote. Ninawaombea Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
Wakili anapaswa kuwa mwalimu wa sheria kwa jamii, si kichocheo cha chuki. Tofauti za kisheria zijadiliwe kwa hoja, ushahidi na vifungu vya sheria; si kwa lugha inayowagawa au kuwajengea wananchi uhasama dhidi ya taasisi. Heshima kwa sheria ianze kwa wanaoieleza. ⚖️
@DupePC Hakuna anayepaswa kutekwa, kuumizwa au kunyimwa haki. Lakini pia tusihitimishe mtu ana hatia kabla ya ushahidi na taratibu za kisheria kuthibitisha. Chuki huongezeka pale tunapobadilisha tuhuma kuwa hukumu. Tujenge hoja kwa ushahidi, tuheshimu sheria na tuache taasisi husika
@FarahOm91196252@siyagaenock1 Bunge ndilo lenye mamlaka ya kutunga, kubadili au kufuta sheria. Lakini elimu ya sheria haishii hapo: IGP na Jeshi la Polisi wanawajibika kutekeleza sheria kwa kuzingatia Katiba, haki za binadamu na taratibu za kisheria.
Kama tunasema “Tuiamini Tume”, basi tuisome ripoti yake kwa usahihi, si kuipa maneno ambayo haikuyasema. Tume ya Jaji Chande ilibaini changamoto katika mfumo wa Haki Jinai na kutoa mapendekezo ya maboresho. Haikutoa hukumu rahisi kwamba “taasisi zote ni mbovu”
TUME YA HAKI JINAI IAMINIWE:
Naomba kutoa TAHADHARI kwa watanzania kuwa MAKINI na baadhi ya watu WAONGO. Tume ya HAKI JINAI (Tume ya Chande) 👇 ilishatoa RIPOTI kwamba; TAASISI ZOTE ZA HAKI JINAI NI MBOVU. Jamani, TUIAMINI TUME. Wapuuzeni WAONGO WOTE wanaosema KINYUME na TUME.
Wakili @PMadeleka , kwenye kesi ambayo bado ipo mahakamani na inasubiri uamuzi, ni muhimu kutofautisha hoja za upande mmoja na uamuzi wa mahakama. Hatima ya shauri haipaswi kuamuliwa na kauli za nje ya mahakama.
@Mariam899050441 Kauli ya “kifo ni kifo tu” katika muktadha wa kutuma salamu za faraja ina maana kwamba kifo chochote ni msiba na kinaumiza, bila kujali mazingira yake. Ni kauli ya kuonyesha masikitiko na pole kwa wafiwa, si kuhalalisha au kupuuza mazingira ya kifo.
@Baharyy25 Kauli ya Rostam Aziz kuhusu mahakama “kupigiana simu na kupeana maelekezo” ni mtazamo na madai yake binafsi, si sheria wala ushahidi wa kisheria. Mahakama huongozwa na Katiba, sheria na ushahidi unaowasilishwa mbele yake.
@Mariam899050441 Jibu
Kauli ya “kifo ni kifo tu” haimaanishi kwamba vifo havina maumivu. Maana yake ni kwamba kila kifo ni msiba na ni jambo la kusikitisha, bila kujali mazingira yake. Ndiyo maana Rais alisisitiza kutamani hali kama hizo zisijirudie.
@Mariam899050441 🤣🤣 PhD ya kupewa? Hilo liweke pembeni kwanza. Rais mwenyewe alisema anaomba na anatamani yaliyotokea yasitokee tena. Sasa hoja ni ipi tujadili kauli za chama au tupuuze kauli ya Rais? Hoja kwa hoja, siyo kelele.
@Mariam899050441 Nani kasema wako juu ya sheria? Kuna tamko gani rasmi kutoka kwa Mwenezi wa CCM Taifa linalosema hivyo? Kama lipo, litaje au liweke hapa. Tusijenge hoja kwa maneno ambayo hayajasemwa.