Waziri Mkuu: Watanzania tusiende uelekeo wa kuona kuua mtu ni jambo la kawaida
Akizungumza leo Novemba 25, 2026, katika mkutano wa hadhara Ifakara, Morogoro, Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amewatahadharisha Watanzania juu ya mauaji ya watu nchini, na kueleza jambo hilo linaweza kuvunja utaifa.
"Nairudia hii naisisitiza kwa sababu tusifike kwenye mazoea ya kuona watu kuuana ni jambo la kawaida. Mambo haya huwa yanaalika visasi, yanaalika makovu, makovu yasiyopona," ameeleza Dk. Nchemba.
"Na mimi niwaambieni Watanzania, hatujazoea maisha ya kuwindana, wala hatutaweza kuishi hivyo," alieleza zaidi kwenye hotuba yake huku akigusia matukio ya mauaji kutokana na migogoro ya wakulima na wafugaji.
"Narudia tena Watanzania, tusiende uelekeo huo wa kuona kuua ua mtu ni jambo la kawaida tu.Tumerithi taifa lina heshima. Lazima tusiweke mzaha kwenye mambo ya msingi ambayo ni misingi iliyojenga taifa letu hili. Lazima tusiwe na mzaha kabisa kwenye nguzo zilizofanya taifa letu hili likasimama mpaka leo. Tukicheza cheza na misingi, tukacheza cheza na nguzo za taifa letu, tutaua utaifa wetu."
Pamoja na kutoa maagizo ya moja kwa moja kwa Mamlaka mbalimbali kama TAKUKURU, Waziri Mkuu ameeleza kuwa ameitisha kikao na wakuu wote wa mikoa kuangalia mambo hayo.
Where is Twaha Mwaipaya?
The High Court has summoned DCI Director Mohamed Amin to appear in person on 1 December 2026 and account for investigations into the disappearance of the Tanzanian activist.
The State cannot investigate indefinitely without answers. Twaha's whereabouts must be established, the truth uncovered, and those responsible held accountable.
#FreeTwahaMwaipaya #EndEnforcedDisappearancesKE
TAMKO LA CHAMA KUFUATIA MKUTANO WA SAMIA SULUHU HASSAN NA VYAMA VYA SIASA NCHINI NA KAULI YA KUUNDWA KWA TUME YA MARIDHIANO NA UPATANISHI ITAKAYORATIBU MAANDALIZI YA MCHAKATO WA MAREKEBISHO WA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Mtoto wa miaka 13.
Ndoto zake alikua anataka kuwa daktari.
Angel alipigwa risasi na watu wenye uchu wa madaraka na kiu ya damu za watu.
Watu hawa wanaoendelea kuteka kila anaekosoa mfumo wao, wanaua, wanafunga jela kwa kesi za uongo.
Familia nyingi kama ilivyo familia ya Angel wanabaki na majonzi na maumivu yasiyokwisha.
Chuki inaongezeka, uhasama unajengeka wannabe wanafikiri wataua kila Mtanzania anaekemea huu uovu Mpaka wabaki ambao wataogopa kabisa na kukaa kimya wote..
Nafikiri wanajidanganya sana, kila uovu unaofanyika unaongeza chuki, unawapa watu ujasiri wa kupinga mabaya na wengi zaidi watazaliwa kukataa huu mfumo wa kidkteta wa sisi kuishi kama mateka.
Tunakulilia Angela kama wengine wote ambao maisha yao yamekatishwa na yanaendelea kukatishwa bila sababu.
Tunajua uovu wao huu wanataka kutubambikizia sisi, tunajua kesi wanaoandaa dhidi yetu ili kuficha wauaji halisi na kukamata watu wema.
Vyovyote watakavyofanya, tutaendelea kupigania haki ya kila mtu na lazima itapatikana na waliohusika watawajibika.
Pole sana familia ya Angel.
Pumzika kwa Amani Malaika.
“MARIDHIANO” YA VYAMA 14 VYA SIASA :
Licha ya kwamba Vyama 14 vya Siasa hapo 👇 HAVINA UGOMVI NA SERIKALI, lakini vimeamua “KURIDHIANA” ili KUONDOA UGOMVI ULIOPO na hatimae KULIPONYA TAIFA. Hongereni sana Vyama 14 vya Siasa. Pokeeni 💐🥀🌷🌹 yenu.
maridhiano hufanywa na pande zinazotofautiana, kukiwa na mwendeshaji huru. kukusanya watu wanaokusifia kila siku na kuita hiyo sehemu ya mchakato wa maridhiano ni hadaa. ccm/serikali haiwezi kuikwepa chadema, na wadau wengi elfu wasioridhishwa na mwelekeo wa nchi. tuwe 'serious.'
@SuluhuSamia Rais bora ulimwengu mzima, mwenye akili kuliko binadamu wote duniani, hongera sana kwa maono haya. Naamini unafaa kuwa rais wa dunia nzima.