#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 89
Wamesimama Mawakili wa Serikali wanasema tunapinga nyaraka kupokelewa kwasababu hatua hazijafuatwa.
Wanasema Mhe. Lissu hajacontradict anataka ipokelewe.
Mhe. Lissu anawajibu Waheshimiwa Majaji wao wenyewe waliniletea hizi kesi siku ya kwanza leo nimetumia utaratibu huo huo ambao waliusema wao na kuniletea kesi tena wameona nongwa.
Kwanza wanasoma sana kesi ya High Court wakati kesi ninayoitumia mimi ni kesi ya Mahakama ya rufani.
Kwahiyo naomba maelezo ya shahidi yapokelewe.
Wanarudi kufanya rejoinder Mawakili wa Serikali amesimama Igans Mwinuka, anasema Majaji mimi sipingi kabisa alichosema kuhusu kesi ya Mahakama ya rufani nakubaliana nayo kabisa.
Hivyo hata hiyo kesi utaratibu wake ni huo kabisa.
Hajaonesha hizo contradiction ni hayo tu.
Majaji wanaandika hapa kidogo.
Jaji anasema na sisi tunahitaji muda kidogo tuweze kwenda kuandika uamuzi mdogo.
Tutaendelea Jumatatu asubuhi itakuwa ni tarehe 13/10/2025.
Kesi imehairishwa mpaka siku ya Jumatatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 81
Mahakama imeanza muda huu.
Majaji wameingia.
Mheshimiwa Lissu alivyoingia kabla ya Majaji amewaambia Mawakili anzeni kuandaa submission ya No Case to Answer maana hakuna kitu hapa.
Mawakili wa Serikali wanacheka.
Anasema Jaji Ndunguru kuwa sasa kabla hatujaahirisha kulikuwa na suala hapa la kulitolea uamuzi mdogo atasoma mwenzangu hapa Jaji Kiwonde.
Anaanza hapa Jaji Kiwonde. Shahidi alisema habari za vibegi vya kura feki na mshitakiwa alipinga hapa.
Baada ya sisi kutafakari swali la msingi tulijiuliza kama mahakama hii ilishatoa amri ya kuzuia maudhui yaliyoonwa yasitolewe ushahidi.
Mahakama siku ya Jumatatu ilisema masuala yanayohusu vibegi vya polisi na utendaji kazi wa mahakama ya Tanzania.
Hicho ndio tulichokizuia siku ya Jumatatu.
Kwenye kesi hii tumeona shahidi namba mbili anasema alichokiona kwenye mtandao wa Kijamii.
Lakini yule wa kwanza yeye alikuwa anatoa ushahidi kama anafahamu mambo hayo.
Huyu anaeleza alichokiona na sisi tunamwambia asifike mbali aishie kwenye kusema alichoona.
Pingamizi halina mashiko.
Shahidi aendelee kutoa ushahidi wake.
Hiyo ndo ruling mtaelewa wenyewe maana binafsi nimejitaidi kuelewa lakini naona Jaji ananivuruga tu hapa ila ndo Mahakama zetu tutafanyaje.
Haya tuendelee
Job Mrema: Sasa shahidi endelea
Kaaya: Lissu alisema hawa mapolisi mnawaona wana vibegi vya kura
Maneno mengine alisema.. kwakuwa majaji nao ni watu wa Rais na wao ni MACCM. Wanataka wapandishwe vyeo kwenda kwenye mahakama za rufani kuteuliwa kwenye commissions na kwenye tume ndiko kuna hela.
Hayo maneno niliona akisema Mshitakiwa.
Akaeleza tena kwahiyo MAHAKAMANI HAKUENDEKI.
Maudhui mengine aliyotamka ni kwamba NA MIMI NATAKA NITEULIWE KWENYE KACHEO FULANI NCHI HII,
UKisema na mimi unamaanisha nini shahidi?
Jaji anaingilia sasa ndugu MREMA Shahidi anasema hayo maneno aliyasema Lissu wewe ukisema anamaanisha nini akisema NA MIMI unamuuliza hilo swali kwani ni yeye ndio ameyasema huyo si ana quote tu?
Job Mrema: Sawa Mheshimiwa Jaji naomba nisamehewe nilidhani ni maneno yake anasema.
Anaendelea Kaaya: anaanza kusema maneno mengine lissu alisema "Mkutano wetu unasema NO REFORMS NO ELECTION, Wamesema Kitu kimoja sahihi hapa kwamba tunapanga kufanya uasi, ni kweli tunaashiria uasi.
Tutakinukisha vibaya sana, tutakinukisha sana sana.
Kitu nimegundua ni kwamba haya Mapolisi yamekaa huko kituoni kukariri Hotuba ya Mh. Tundu Lissu ambayo yeye hata hakatai hayo maneno wa kila siku ya Mungu wanayarudi tu kama Sara ya Baba yetu.π
Nafikiri hawana kitu cha kukitolea ushahidi.
Eniwei tuendelee
Job Mrema: Ulivyomaliza kusikiliza Video ulibaini nini?
John Kaaya: Nilibaini matamshi yale yana viashiria vya jinai.
Job Mrema: Shida gani?
John Kaaya: Maneno yavibegi niliona yanapotosha umma.
Jaji Kiwonde: sasa mnaona huko mnaanza kuelekea tena kwenye vibegi.
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji huu ushahidi aachwe aendelee kuutoa tu maana nilipinga mkasema ni sahihi aendelee sasa nafikiri asikatazwe acha aseme tu. π
Jaji Ndunguru: Basi aendelee hakuna shida.
Job Mrema: Ieleze Mahakama Shahidi ulikuwa unaelezea viashiria vya makosa kwenye maneno hayo.
John kaaya: Waheshimiwa Majaji pamoja na hayo matamshi niliyosema, pale aliposema kuwa mahakamani hakuendeki kwasababu majaji ni watu wa Rais na ni MACCM niliona taarifa hiyo ina viashiria vya jinai. ππ
Anaendelea pia shahidi kusema kanuni za utumishi wa umma zinakataa watumishi kuwa wafuasi wa vyama vya siasa.
Yani Job Mrema na John Kaaya wamekutana hapa ni pipa na mfuniko. Wanzingua sana yani wanapa uvivu kuandika maana kuna muda wanaongea hivi havieleweki
Kaaya kuna muda anaongea sauti ya chini hadi Jaji anamwambia ongeza sauti ni muoga muoga sijui Polisi wa wapi huyu au ndio mjanja akiwa anapiga doria mtandaoni.
Part 82 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Mwiteni George Bagyemu!
Kumbe familia yake ina historia ngumu?!
Baba yake alikuwa Captain Gervas Rweyongeza ambaye alikuwa miongoni mwa wanajeshi 14 na raia 5 walioshtakiwa na kuhukumiwa katika njama ya kuipindua serikali ya Mwalimu Nyerere mwaka 1982?!
Haya mdau ameshusha data hapa hadi kijiji chao na anamkumbusha George kuwa historia itamhukumu aishi vizuri na watu!
Mi nimetimiza wajibu ππ½
#TutaelewanaTu
@authoroflight01@WarrenH39@AvekiKigwa Sijakuelewa Yan baada ya kuchemsha upime kijiko kimoja ndo unywe au majani yake ndo upime kijiko kimoja ndo uchemshe. ?