💨Leo ushtue umaskini kwa hii 😂👇
Pandisha picha yako Gemini alafu copy prompt kuna sehemu ya kuedit jina na kazi yako.
“Ultra-realistic 8K full body portrait of [PERSON], wearing a clean and pressed white social shirt with folded collar and a small lapel microphone, dark navy-blue dress pants and polished brown social shoes. Casually and unpretentiously leaning against a smooth light gray studio wall; hands are in pockets and one leg is crossed over the other, with relaxed and confident body language. Add to the wall next to them a prominent vector portrait in black and white of their face and bust - with sharp lines and angles, overlapping polygonal shapes and a minimalist modern graphic style, right below the information: “FULL NAME”, and below the name: “PROFESSION”. 3:4 dimension.”
TUMIA CIU (REMOTE) YA JIRANI YAKO KUWEKA UMEME.
Mara nyingine unakuta CIU yako haifanyi kazi au imepotea na umeme umeisha huna namna ya kupiga simu TANESCO usubifu mafundi waje wakuwekee umeme lakini kuna namna unaweza kufanya ukaweka huo umeme kwa kutumia CIU ya
@Thommunkondya@fabolous069 Ulinunua kiwanja 2-3 years ago kwa gharama let say 7m then after 3years ukaja ukajenga nyumba ya 200m na neighborhood iko na nyumba ya hadhi hiyo. Je issue ni gharama ya kiwanja au neighborhood?
@Desikavishe@bajabiri Nemc ( registration na review cost 4.2m, consultant 4-7m) bado Fire, Osha, Ewura, Vibali vya ujenzi, Hati etc ili asiwe na stress za hapa na pale 350m inatosha na anaweza kupata Pesa ya Standby Generator
@bajabiri ~350m hapo Site uwe nayo na hati iwe mezani. Utafanya EIA, utatafuta kibali Ewura, Osha, Fire etc. Gharama itaongezeka kama components zinaongezeka mfano, Standby Generator, Service bay na Kama Jengo la office linakuwa na vitu vingi
UTARATIBU WA MKRISTU MKATOLIKI KANISANI
•Unapoingia Kanisani, chovya maji ya baraka na kusema:
"Unitakase Ee Bwana uovu wangu wote, ili nipate kushiriki ibada takatifu: Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina!
•Kama Kanisani kuna Ekaristi Takatifu iliyohifadhiwa katika Tabernakulo, piga goti huku ukisali: "Bwana wangu na Mungu wangu". Haya ni maneno aliyotamka Tomaso baada ya kumwona Yesu Mfufuka (Yoh 20:28).
•Ukiinuka sali: "Nitakusifu na kukuabudu katika Ekaristi takatifu"
•Nenda mpaka kwenye kiti, piga magoti huku ukitoa nia yako ya kusali Misa siku hiyo, mfano:
"Ee Mungu, ninaungana na jeshi la mbinguni, pamoja na Bikira Maria, nikiwa na nia ya kumwombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, jirani yangu ambaye hatuelewani na pia familia yetu ambayo haina amani. Kwa Sadaka hii ya Misa Takatifu, mponye mama yangu, leta uelewano na jirani yangu, na pia rejesha amani ya familia yetu pamoja na familia zote ambazo hazina amani"
NB: KILA MISA UNAYOSHIRIKI HAKIKISHA UNA NIA YAKO NA UINGANISHE NA SADAKA HIYO YA MSALABA. USISHIRIKI MISA KAMA MTAZAMAJI BILA KUWA NA NIA YAKO MOYONI.
•Endelea na ibada ya Misa na Kushiriki Litrujia kikamilifu.
NB: Hakikisha unashiriki kikamilifu kwa kuimba, kuitika kwa sauti, kusimama, kupiga magoti nk kwa uchangamfu.
Misa huwa tunashiriki wote kwa pamoja lakini MATUNDA YA MISA kila mmoja anapokea tofauti kulingana na jinsi alivyoshiriki.
Kama ni kwa asilimia, basi sio wote huwa tunapata asilimia zinazolingana za neema kwenye Misa. Kuna wanaopata neema nyingi zaidi, wanaopata kidogo nk kulingana na maandalizi ya moyo na ushiriki hai katika kupokea matunda ya adhimisho lenyewe.
Kama ni bomba linalotiririsha maji, basi kila mmoja wetu ni mtekaji akiwa na chombo chake. Wingi wa maji (Neema) utakaoingia ndani ya chombo (Roho/moyo) utategemea:
1. Chombo chako kipoje wakati unateka hayo maji
2. Nafasi (kama ndani ya chombo nafasi ni ndogo, ndivyo na maji yatakavyoingia machache. Kama nafasi ni kubwa, ndivyo na maji yatakavyoingia mengi. Kama moyo umejaa hauna nafasi, ndivyo na Neema hazitaingia kabisa kwasababu hazina sehemu ya kuingia)
3. Umekiwekaje bombani ili maji yaingie ndani (hapa sasa ndio USHIRIKI HAI katika adhimisho.
Hivyo, tuliza akili na moyo wakati wa Misa, na shiriki kikamilifu Liturujia hatua kwa hatua.
Ndiposa kila mmoja anapokea neema za Misa kwa kadiri ya maandalizi aliyofanya na ushiriki anaoonyesha wakati wa adhimisho.
NB: Utofauti wa kupokea matunda ya adhimisho la Misa haupo kwa mtoaji (Yesu) bali kwa mpokeaji (Anayeshiriki). Utofauti wa maji tunapoenda bombani kuteka, haupo kwa bomba linalotoa maji, bali kwa aina ya chombo na utayari wa mhusika kuteka maji hayo.
Tuendelee
•Wakati wa Kupokea Ekaristi (Komunyo) ukikumbuka kuwa una dhambi kubwa (ya mauti), komunika kwa sala ya tamaa. Usithubutu KAMWE kupokea Ekaristi ukiwa na dhambi ya mauti.
"Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Maana alaye na kunywa, HULA NA KUNYWA HUKUMU YA NAFSI YAKE, KWA KUTOKUUPAMBANUA ULE MWILI. Kwa sababu hiyo wako WENGI KWENU WALIO HAWAWEZI NA DHAIFU, NA WATU KADHA WA KADHA WAMEKUFA." (1 Kor 11:26-30)
Hivyo, usipokee Ekaristi ukiwa na dhambi. Baki upokee kwa tamaa ya moyo. Jisikie wivu Mtakatifu wakati huo, na jitahidi ujitakase kwa kuungama ili adhimisho lingine usikae tena bila kupokea.
•Mwisho, wakati wa kuondoka chovya maji ya baraka na ujibariki. Kwa kuwa baada ya adhimisho huwa tunapaswa kwenda kuishi kile tulichoadhimisha, waweza kusali sala ya binafsi "Unilinde Ee Mwenyezi Mungu, nikapate kuwa mfano katika jamii yangu, na nikushuhudie katika matendo yangu"
Hapo unachovya maji ya baraka na kufanya ishara ya Msalaba "Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina"
Tumsifu Yesu Kristu. Mungu akubariki.