@fadhilikangusi Mtazamo wangu mwanaume ni muhimili wa familia, kama hana courage basi familia nzima inakosa muelekeo. Sasa ukienda kuishi ukweni apo lazima ukose courage, familia yako nzima inakua chini ya baba mkwe. Hapo sijazunguzia swala la kipato na namna ya huduma za nyumbani zinavotolewa.
Kuna wakati huwa tunapokea upendo mkubwa sana kutoka sehemu ambayo hatuitarajii. Kwa sababu sisi hatuna upendo kwao kama walio nao kwetu sisi basi hatuoneshi hata kujali na kuheshimu ule upendo wao kwetu. Siku tukija kutambua thamani yao tayari wao hawana muda nasi.