Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema nchi yake haitakubali kamwe kuachana na haki yake ya kuendeleza mpango wa kurutubisha urani kwa matumizi ya kiraia, akitoa msimamo huo katika hotuba yake mbele ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Septemba 23, 2026.
โJamani nina kwetu, Nina kwetu na niliaga vizuri, na ndio maana wa kwetu wapo hapaโ. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akiwasili mahakamani leo Alhamisi Septemba 24, 2026.
RAIS SAMIA AONGOZA DHAMIRA YA AFRIKA KUTOKOMEZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa uongozi wake mahiri katika kusukuma mbele ajenda ya Afrika ya kutokomeza vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto, huku bara hilo likikabiliwa na karibu asilimia 70 ya vifo vya akina mama duniani na takribani theluthi mbili ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano.
Akiwa Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, Rais Samia anaongoza ajenda ya โMalengo Matatu ya Sifuriโ (Three Zeros) inayolenga kufikia sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto mchanga, pamoja na sifuri ya watoto wasiopata chanjo.
Ajenda hiyo imepewa msukumo katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Wakuu wa Nchi kuhusu Afya ya Mama, Mtoto Mchanga na Mtoto, iliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), ukiwakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wa taasisi za Umoja wa Afrika, mashirika ya kimataifa ya afya na washirika wa maendeleo.
Akiwasilisha ujumbe wa Rais Samia katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema ukubwa wa changamoto unahitaji Afrika kutoka kwenye ahadi na kuelekea katika hatua madhubuti zinazoweza kupimwa kwa maisha ya wanawake na watoto yanayookolewa.
Amesema, pamoja na hatua ambazo Bara la Afrika limepiga, Afrika bado inachangia karibu asilimia 70 ya vifo vya akina mama duniani na takribani theluthi mbili ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano, huku sehemu kubwa ya vifo hivyo ikiwa inaweza kuzuilika.
Makamu wa Rais amesema msukumo wa Rais Samia unalenga kuimarisha mifumo ya afya ya nchi za Afrika, kuongeza ufadhili wa ndani, kuboresha huduma za dharura na mifumo ya rufaa, kuongeza upatikanaji wa wahudumu wa afya wenye ujuzi na kuhakikisha takwimu zinatumika kufuatilia matokeo na kubaini maeneo yanayohitaji hatua zaidi.
Akielezea uzoefu wa Tanzania, Makamu wa Rais amesema uwekezaji katika huduma za afya ya msingi na za dharura kwa mama na mtoto mchanga, pamoja na kuimarishwa kwa mifumo ya rufaa ikiwemo M-Mama, unaonesha namna uongozi wa kisiasa, teknolojia na utoaji wa huduma kwa wananchi vinavyoweza kuunganishwa katika kuokoa maisha.
Hatua hizo zimekwenda sambamba na kuongezeka kwa wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 51 mwaka 2015 hadi asilimia 81 mwaka 2022, mafanikio yanayoonesha uwezekano wa kubadili mwenendo wa vifo vya mama na mtoto pale uwekezaji unapounganishwa na utekelezaji katika ngazi ya jamii.
Makamu wa Rais alisema ajenda anayoiongoza Rais Samia pia inatoa uzito kwa suala la Afrika kujitegemea katika afya, akisisitiza kuwa mafanikio hayapaswi kupimwa pekee kwa uwezo wa bara kugharamia, kuzalisha au kununua mahitaji yake, bali pia kwa uwezo wa kuhakikisha huduma muhimu zinamfikia kila mama na mtoto kwa wakati na mahali wanapozihitaji.
Katika kufanikisha hilo, nchi za Afrika zimehimizwa kuimarisha uwajibikaji wa kisiasa, kuongeza uwekezaji wa ndani katika huduma zinazookoa maisha na kuhakikisha rasilimali zinafika hadi katika ngazi ya utoaji huduma.
โDhamira ni kuhakikisha hakuna mama anayepoteza maisha kwa kukosa usafiri, damu, mhudumu mwenye ujuzi au huduma ya dharura; hakuna mtoto mchanga anayefariki kwa kukosa huduma inayoweza kuokoa maisha yake, na hakuna mtoto anayebaki bila chanjo kwa sababu mfumo wa afya haukuweza kuifikia familia yake,โ amesema Mhe. Ndejembi.
Makamu wa Rais amesema kulinda uhai wa mama na mtoto si suala la afya pekee, bali ni uwekezaji katika rasilimali watu, uchumi na mustakabali wa Afrika, pamoja na kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Bara la Afrika.
William Ruto anapopata nafasi ya kuongea huwa hafanyi makosa ameongelea Afrika na changamoto zake huyu kweli ni kiongozi, ila wetu alikuwa anasoma tu yaliyobandikwa
Ruto kwenye speech ni mnyama sana huyu ndio maana wakenya huwa wanasema usimpe muda wa kujieleza Ruto ๐๐๐๐๐
Shida mnasahau haraka sana, hakuna Kiongozi mkubwa nchi alishawahi achia madaraka kwa kupenda au kutokupenda akatoka tu hadharani! Na hii hata kwenu ilitokea kwa Mbowe! Alijifungia muda mrefu.
So mwambieni Lissu, Nchimbi yuko mapumziko, kama alivyokuwa Mbowe wakati amemshinda kiti cha Uenyekiti? Au mlikuwa mmemfungia ndio mnataka fananisha? Mwacheni baba wa watu apumzike zake.
Wewe tu mtu wa kawaida ukiachwa mtiti lazima ujifungie ndio iwe cheo kikubwa kama Makamu wa Rais! Nawaambia tena Mke wake yuko na anaendelea na life lake tena kwa vicheko kabisa, na huko kanisani mnako Uliza anaenda! Mfixuuuu!!
Ila nyie hamko seriously, kwahiyo kesi ya Lissu mmeiacha ๐, Lissu nae basi CCM C Yule, unaamishaje narrative ya kesi yako!! ๐ ๐ ๐
#HABARI Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, ameonya kwa mara nyingine tena wafanyabiashara wa kigeni kufanya biashara zao katika Soko la Kimataifa la Kariakoo na kujifanya machinga huku wakiwa na magodauni nje ya Kariakoo.
Akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na machinga leo Septemba 24,2026 katika Soko hilo, Chalamila amesema raia wote wa kigeni wanaofanya hivyo ni wadukuzi wa uchumi (Economic Hackers), huku akiwataka wote waende ndani kabla hawajachukuliwa Sheria akitumia neno "Watakipata Cha moto".
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
HABARI:
Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Revocatus Chipando โBaba Levoโ, amemtakia heri ya kumbukizi ya kuzaliwa Kiongozi Mstaafu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, anayefikisha miaka 50, huku akikumbusha uhusiano wao wa kisiasa uliopita.
Soma zaidi instagram ya jamiivoice