Timu ya Wataalamu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Prof. Joseph Ndunguru, leo imetembelea vipando vya mazao mbalimbali katika Maonesho ya 33 ya Siku ya Wakulima (Nanenane 2026), yanayofanyika katika Viwanja vya John Malecela, Nzuguni, Jijini Dodoma.
Ziara hiyo imelenga kubaini visumbufu vinavyoweza kuathiri mazao pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Wakulima na Washiriki wa maonesho hayo kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Wakati wa ziara hiyo, Wataalamu hao walibaini uwepo wa visumbufu katika vipando vya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na kuchukua sampuli za mimea kwa ajili ya uchunguzi wa haraka kwa kutumia teknolojia ya Portable DNA Sequencer.
Teknolojia hiyo huwezesha Wataalamu kubaini kwa usahihi chanzo cha tatizo na kupata majibu kwa wakati, hatua inayosaidia kutoa ushauri sahihi kwa Wakulima, hatua hiyo inaonesha dhamira ya (TPHPA), ya kutumia teknolojia za kisasa kuimarisha afya ya mimea, kudhibiti visumbufu na kulinda uzalishaji pamoja na usalama wa mazao Nchini.# MillardAyoUPDATES
HESHIMA KWA HAYATI MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE (Baba wa Taifa wa Tanzania), HESHIMA KWA TANZANIA.
//
Pichani ni matukio mbalimbali katika uzinduzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, Angola, tarehe 01 Agosti, 2026.
Hospitali hiyo imepewa jina la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama heshima na ishara ya kutambua mchango wake katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, hususan nchi za Kusini mwa Afrika, ikiwemo Angola.
Hospitali hiyo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Angola Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço leo tarehe 01 Agosti, 2026.
Picha ya 4 ni Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akipokea zawadi ya picha ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya hafla ya uzinduzi wa hospitali hiyo Jijini Luanda.
@HildaNewton21 Huo ni uongo. Prof. Kabudi ni miongoni mwa watu wachache sana katika nchi hii wenye akili. Tumhukumu kwa mengine kama binadamu sio masuala ya taaluma
@623de4f5f8f048e@fbuyobe Hongera sana kama bado unakumbuka vizuri. Mwaka 2000 nilikuwa Form III tukisoma hivyo vitabu kwa ajili ya kujibu mitihani ya English Literature. Umuofia Kwenu!!!!!! Yaaaa… kwenu… yaa
@Deeh1926@ayubu_madenge Yes… as pamoja na George Washington, Thomas Jefferson na James Madison, James Monroe alikuwa influential sana akiwa Rais wa Marekani kiasi kwamba mji mkuu wa Liberia Monrovia ulipewa jina kwa heshima yake
@DukeDizzo@Dr_DGwajima Hahaha umejaribu kumtoa kwenye reli lakini Mama hajatoka. Mwisho umekubali na kunyoosha mikono. Heko kwa Mh.@Dr_DGwajima maana angekuwa mwingine hapo angepanic na kujibu hovyo
Yanga wameeandika barua imejieleza sana, May be TFF watumie ubabe tuu ila wanakila haki za Kupata point 3, ni aibu Kubwa team kama ya Simba inasema Imezuiliwa na Mabaunsa, Kwahiyo Simba haina walinzi wala mabaunsa.
Yanga mshikilie hapo hapo we need respect kwenye League yetu.