Kumjua Mungu Ni Kujua Kila Kitu,Kujifunza Kuhusu Mungu Ni Kujifunza Kila Kitu,Kumpata Mungu Ni Kupata Kila Kitu,Kwa Sababu Mungu Ni Kila Kitu.
MSISITIZO:Mungu Ni Siri Ya Vitu Vyote.
Good Morning🌄Ladies And Gentlemen🫂
Biblia Imeandika vitu vingi sana lakini kama ingeandikwa kwa maneno mawili Tu basi yangekua Imani na Upendo.
Akili hu solve yale yanaonekana kwa macho ya nyama.. lakini Imani ni kuwa na hakika na yale yasiyo onekana.
Unakuwa vipi na hakika na yasiyo onekana?
Mtumaini Bwana📌
Kabla hujaenda kwa mganga, kabla hujaanza kuilaumu serikali na uchumi, kabla ya kujihisi kuwa una bahati mbaya, au mazingira yako… angalia watu wanaokuzunguka kwanza.
Jitenge na watu wenye negative mindset.
Watu ambao kwa kila wazo jipya wanaona tatizo.
Kwa kila ndoto wanaona hatari.
Kwa kila fursa wanaona sababu za kwanini haitafanikiwa.
Kwa sababu ukweli ni kwamba, kuna watu hawataiba pesa zako.
Hawataiba simu yako.
Hawataiba mali zako.
Lakini watakuibia kitu hatari zaidi…
Watakuibia maono yako.
Watakuibia ujasiri wako.
Watakuibia imani yako.
Watakuibia ule moto wa kuamini kuwa maisha yako yanaweza kubadilika.
Utaenda kwao ukiwa na ndoto kubwa.
Ukiwa na hamasa.
Ukiwa na wazo ambalo linaweza kubadilisha maisha yako.
Lakini baada ya dakika chache za mazungumzo, utaondoka ukiwa na mashaka kuliko ulivyofika.
Si kwa sababu ndoto yako ni mbaya.
Bali kwa sababu wao wamezoea kuona ukuta kila mahali.
Na ukikaa nao muda mrefu, utaanza kuona dunia kwa macho yao.
Utaanza kuona ugumu kabla ya kuona uwezekano.
Utaanza kuona sababu za kushindwa kabla ya kuona sababu za kujaribu.
Ndiyo maana unatakiwa kujizunguka na watu wenye mtazamo chanya.
Watu wenye akili za ukuaji.
Watu wanaoona opportunity pale ambapo wengine wanaona obstacles.
Watu ambao badala ya kukuuliza “ikishindikana je?”
Wanakuuliza “ikifanikiwa je?”
Watu ambao badala ya kukuonyesha sababu za kuacha, wanakusaidia kuona sababu za kuendelea.
Kwa sababu dunia hii imejaa matatizo kwa kila mtu.
Lakini watu wanaofika mbali si wale wasiokutana na matatizo.
Ni wale wanaojifunza kuona fursa ndani ya matatizo hayo.
Kumbuka…
Ukikaa na watu wanaolalamika kila siku, nawe utaanza kulalamika.
Ukikaa na watu wanaoogopa kila kitu, nawe utaanza kuogopa kila kitu.
Ukikaa na watu wanaoona fursa kila mahali, nawe utaanza kuona fursa kila mahali.
Kwa hiyo kabla hujaamini kwamba bahati imekukataa…
Kabla hujaamini kwamba dunia imekukalia vibaya…
Kabla hujaamini kwamba maisha hayapo upande wako…
Angalia kwanza watu unaowasikiliza kila siku.
Kwa sababu mara nyingi tatizo halipo kwenye uchumi.
Halipo kwenye serikali.
Halipo hata kwenye mazingira.
Tatizo lipo kwenye sauti zinazokuzunguka kila siku na namna zinavyoumba mtazamo wako wa maisha.
Ukiijua Biblia vizuri basi Huenda ukawa ume solve 80% ya changamoto za dunia.
Imagine imeandikwa
"Siku ya heri uwe na furaha, na siku ya taabu ufikiri."
Sio siku ya Taabu uhuzunike, La hasha! "UFIKIRI"
Kwa Lugha nyepesi kabisa ni kuwa Always there is a Way out.📌
Mara nyingi katika maisha yetu tunapitia nyakati ambazo zinaonekana kama mwisho wa safari.
Ndoto zinakufa, mipango inaharibika, biashara zinaanguka na milango inafungwa.
Lakini simulizi ya Lazaro linatukumbusha kuwa kile kinachoonekana kuwa mwisho kwa mwanadamu kinaweza kuwa mwanzo mpya kwa Mungu.
@thatsjoems Ukitoa Ushabiki
ukimchanganya Dembele na Olise kwa pamoja hawawezi fikia Uwezo wa Mbappe.
Vitu mnavyo ona ni vya ajabu kwa Olisse Leo, mbappe alishavifanya sana zaidi yamiaka 10 nyuma, tena akiwa Bwana mdogo kabisa wa miaka 17 huko.
Mafanikio na kufeli ni ndugu wa Baba mmoja..
Kinacho mtofautisha mtu aliyefanikiwa na asiyefanikiwa ni kwamba mmoja alitumia kufeli kama msingi wa kumjenga kuwa Imara zaidi.
Na mmoja alitumia kufeli kama nyundo ya kumbomoa zaidi.
Katika Maisha Kila Mtu Anaweza Kufeli, Na Kila Mtu Anaweza Kufaulu. Hivi Vitu Huenda Kwa Zamu Tusichekane Pale Tunapofeli Cha Umuhimu Tupeane Moyo"
Good morning ladies and gentlemen 👊🏾
Yesu mwenyewe kabla hajawaponya wale vipofu aliwauliza nyie mwaamini kwamba naweza kufanya hili?
Wakamwambia Naam bwana, kisha akasema kadri ya imani yenu na mpate na macho yao yakafumbuka.
Maana yake ni kwamba Unachoamini ndivyo kitavyokua. Miujiza yako huanzia ndani yako📌
Hata siku moja usijaribu kulidharau wazo lako ambalo unaliona dogo,lichukue liamini kisha anza kulifanyia kazi na mwisho litakupa matokeo kwa ukubwa.
Usijidharau,nabii wa kwanza kwenye maisha yako ni wewe mwenyewe.
Kwa lugha nyepesi
Ni kwamba hata kama umeandikiwa changamoto hazikosekani katika safari yako ya mafanikio.
Njia pekee ya kufanikiwa ni kutokata Tamaa, na silaha pekee itakayo kusaidia kutokata tamaa ni Imani.
Amini na Itakua, ni suala la muda Tu champ📌
Kwa Lugha nyepesi Biblia inajaribu kuelezea ni namna binadamu Tuna uwezo mkubwa wa kufanya chochote tunachotaka.
Ila uwezo huo Umefungwa na hofu na hofu huondolewa na Imani.
Amini Itakua📌
Imani ni kuwa na hakika na yale yasiyo onekana.
Kwa lugha nyepesi ni kuwa Imani ni kutokata Tamaa haijalishi changomoto zipi unapitia.
Nb: Amini Itakua... One day yes📌