Mimi si mshabiki wa mpira, lakini baada ya PSG kuichapa Arsenal, nimegundua noise pollution si tatizo la viwanda pekee. PSG walifanya usafi wa mazingira hadi mtandaoni.
Jana kuna mahali nilipita nikawakuta dada fulani wamevaa jezi za Arsenal. Walikuwa na kelele na kujiamini kuliko hata zile za “Oktoba tunatiki”. Kila dakika walikuwa wanatoa uchambuzi, utabiri na walikuwa wamepiga pamba kwa kiwango cha juu kabisa. Bado kidogo ningejifanya na mimi ni mshabiki wa mpira tena Arsenal. Naamini PSG hawakushinda mechi tu… walishusha pia decibel za mijadala ya mitaani. 😄 Sasa turudi kwenye FREE TUNDU LISSU na KATIBA MPYA ni SASA.
Hili nalo ni kosa ambalo natuhumiwa kulifanya kwa mujibu wa Msajili. Sasa narudia tena kusisitiza, ofisi za Serikali si duka la wazazi wenu wala mali ya familia zenu. Mkipewa mamlaka ya umma, mnapaswa kuvumilia kukosolewa, kuulizwa maswali na kuwajibika kwa maamuzi yenu. Kama hamtaki kusemwa, kuhojiwa au kuwajibika, acheni hizo ofisi mrudi mkakae na wake zenu, waume zenu na familia zenu. Mamlaka si kinga dhidi ya uwajibikaji. Na hili linamhusu kila mmoja wenu, hususani pia na wewe Msajili
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam leo, Alhamisi Mei 28, 2026 imeifuta rasmi na kuiondoa mahakamani hati ya kesi ya madai iliyofunguliwa na kiumbe aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Issa Mohammed na wenzake dhidi ya bodi ya wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, iliyokuwa inahusu usawa katika mgawanyo wa mali za chama kati ya Tanganyika na Zanzibar.
NB; Kesi hii ndiyo MaCCM waliotumia kuzuia shughuli za CHADEMA kwa siku 310.
Bodi ya Ithibati mtakuwa tayari endapo Waandishi wakianza kuchambua na kujadili mambo muhimu ya nchi hii kwa uwazi?
Kama ni NO basi michezo na burudani ndiko mahali sahihi .... waachwe waandishi waendelee !!
NOT YET HEALED. STOP YOUR MOCKERY ON THE LIVES OF OUR BELOVED.
Here we are with Chairman James Mbatia a man who was stripped of his chairmanship through deceit by the so called “healing Masters”.He is not healed.
On my right hand is my younger brother Abdul Khareem, and my younger brother Mdude Mpaluka Nyagali is on the far left.
Mdude’s children have not healed.
Mdude’s wife has not healed.
Mdude’s sister has not healed.
Mdude’s friends have not healed.
It is deeply irresponsible and insensitive to joke about people’s lives. We reject slogans of “Never Never Again” or " Dumb Close Claim of Sovereingty " until our brother Mdude Mpaluka Nyagali is returned to us and all Issues of enforced Disapearences and October 29 massacre have been fully addressed and investigated.
If you hear anyone claiming that “we have been healed,” know that such a person is a manipulator and should be ignored.
There can be no healing in TANGANYIKA without:
TRUTH, JUSTICE, AND ACCOUNTABILITY.
BAK MWABUKUSI
SHAMBANI, BUSOKELO.
#TajiriLaKihaya
Ni Ukweli Usiopingika kwamba WANAHARAKATI WANALIPWA….
hasa waliopo Nje ya nchi kwa huku kwetu na kuna foundations kibao tu za HUMAN RIGHTS ACTIVISTS karibu kila Nchi duniani kote….
ila Kwa yaliotokea Oct 29. haikuhusiana na Malipo haya wala msukumo wa wanaharakati…
Wananchi wenyewe tu walichoka… kuna raia waliandamana hata hawana SmartPhone… wengine hawapo hata mitandaoni…
Yaliotokea ni matunda ya Udhalimu wa Viongozi wetu….
Huwezi zuia chama kikuu cha Upinzani chama kinachoPendwa zaidi Tanzania nzima- KUTOSHIRIKI UCHAGUZI MKUU…
Umfunge Mgombea Urais wa Chama…anaependwa zaidi na Vijana…
Alafu u expect ZERO REACTION… HAIWEZEKANI!
Tusijifiche kwenye malipo ya FORD FOUNDATION…
Hawajaanza leo kulipwa… wanalipwa toka enzi… kila mtu analifaham hili… wanalipiwa RENT, CHAKULA na UPKEEP ZOTE na hata Kutoa Elimu, yale ma space nk. Ni kazi kama kazi zingine tu. Wengine wanaotaka kuongeza Elimu… wanapewa ufadhili!
Hili lipo wazi… na sijui kwa nn WANAHARAKATI wanalificha hili,hawataki lijulikane!
Ila haihusiani kivyovyote vile na yaliotokea Oct 29th.
Tuliweke hili sawa!
Watanzania, Wauwaji wameaanza kampeni kubwa ya kuwasema Wamarekani ili wakae pembeni watuache Watanzania peke yetu ili wao waendelee kutupiga risasi na kututeka na Samia Suluhu aendelee kushikilia nchi illegally.
Sasa tusikubali, lazma na sisi wananchi tuanze kampeni kabambe ya kumuomba @POTUS atusaidie…. Watanzania Trump ndio nafasi yetu ya mwisho kupata haki bila kuendelea kupigwa risasi na CCM.
Wabunge haram na bosi wao wanajua Wamarekani na @realDonaldTrump wakichukua hatua kwenye issue ya October 29 basi haki itapatikana Tanzania, na haki ikipatikana Tanzania CCM hawana uhakika wa madaraka, hii ndio sababu wanapambana juu chini tusipate msaada wa nje. Sasa tusikubali.
STOP USING PROPAGANDA OVER THE LIVES OF TANGANYIKANS.
No nation is oppressing us. Our problems are the result of our own ignorance and cruelty.
We have abandoned accountability founded on the rule of law and the Constitution, and have turned ourselves into untouchable gods.
We cannot continue killing and attacking thousands of people and then claim to be sovereign; that is ignorance born out of a lack of understanding.
Sovereignty in any nation exists within civilized limits recognized by the international community.
IF WE ARE NOT READY TO HOLD OURSELVES ACCOUNTABLE, THEN THE INTERNATIONAL COMMUNITY WILL HOLD US ACCOUNTABLE.
Truth, Justice, and Accountability are the only foundations upon which this nation can be rescued from its current crisis.
BAK MWABUKUSI
Kwanza kabisa ukisikia mtu KATEKWA na kapona utekaji mpe pole na kuwa mfariji. Habari za kuanza kukosoa anayosema kuhusu utekwaji wake inaumiza sana.
Mimi nilipotekwa na nikaanza kusimulia utekwaji wangu ilikuwa ni kama MOVIE na wapo wengi walijua natunga story. Mimi nilitaja mpaka SAA kila tukio nililokumbuka na kusimulia.
Chawa wakalipwa kuaminisha watu kuwa mimi SIKUTEKWA ni ishu zangu na “Washkaji”, “mambo ya mapenzi”.
Siku zilivyoenda UKWELI ukajitenga na MAFWELE niliemtaja tangu siku ya kwanza akajulikana kuwa ndie MTEKAJI MKUU wa taifa.
Na leo ukiambiwa wanaoteka watanzania ni POLISI hakuna anaekataa maana USHAHIDI wote unaonyesha ni wao.
Maswali kadhaa ambayo huji kupata majibu ni haya na ndio ishara kwamba wao ndio watekaji.
Maswali hayo ni yafuatayo;
1. Kwanini hakunaga ripoti za majibu ya uchunguzi ya kuhusu UTEKAJI?
Achana na ishu yangu SATIVA watakuambia sijatoa ushirikiano, vipi kuhusu UTEKAJI wa mzee KIBAO? MDUDE? SOKA? Kuvamiwa kwa Father KITIMA?
2. Pingu zinazotumika kwenye utekaji kiuhalisia nani anayo mamlaka ya kumiliki PINGU nchini kisheria?
3. Matumizi ya SIRAHA za moto kwenye matukio ya UTEKAJI kisheria nani anayo mamlaka ya kumiliki silaha kisheria?
4. Kuhusu magari wanayotumia kuteka watu kwanini mengi hayana Plate number na mengine yana plate number ZA nchi jirani?
Haya magari kwanini hayazuiliwi kwenye vizuizi vya vyombo vya usalama (Check points) zilizopo barabara nyingi nchini?
5. Mtu kama MAFWELE alietajwa kwenye utekaji wangu mimi SATIVA kwanini mpaka leo hajahojiwa kwa UTEKAJI wangu na badala yake kapandishwa cheo huko kwenye upolisi?
Haya ni maswali machache ambayo kila mwenye akili timamu anajua WATEKAJI ni polisi na hawa WATU HAWAWEZI KUJICHUNGUZA KUMALIZA UTEKAJI NCHINI.
Sir TIVA
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
HABARI MBAYA
Msaidizi wa Mhe. Lissu @daviddjumbe ametekwa usiku huu na maofisa wa Usalama wa Taifa ambao walikuwa na silaha za moto.
Jumbe ametekwa akiwa nje ya geti la nyumbani kwake , maeneo ya Bunju Dar es salaam.
Wananchi waliokuwa wanakimbiza gari iliyomteka, wameiona ikiingia kwenye nyumba za Usalama wa Taifa zilizo maeneo ya Mbweni.
#FreeDavidJumbe
02
Hata kabla ya sheria nyingi kuandikwa,dhamiri tayari ilikuwa imeanza kushtaki.
Ndiyo maana ukweli mkubwa ni huu:Unaweza kuwadanganya watu kwa muda.Unaweza kuikwepa sheria kwa muda.Lakini ni vigumu sana kuikwepa dhamiri yako mwenyewe milele.
Kwa sababu dhamiri ya mwanadamu…ni mahakama ambayo haifungwi milele.
Kuna watu wanatembea huru leo,
lakini akili zao zimekuwa magereza yao.
Watu waliovikwa medali,
waliosifiwa majukwaani,
waliosalimiwa kwa heshima kubwa—
lakini usiku wanashindwa kulala wakiteswa na kumbukumbu
ambazo hawawezi kuzizika.
Kwa nini?
Kwa sababu kuna tofauti
kati ya kile kilicho halali
na kile kilicho sahihi mbele ya ubinadamu.
Mtu anaweza kuwa anafuata amri…
lakini bado akawa anasaliti utu wa mwanadamu.
Historia imejaa askari waliokuja kukiri baadaye:
“Tulikuwa tunafuata maagizo.”
Lakini dunia imejifunza kwa uchungu:
uovu hauwi haki
kwa sababu tu umeamriwa na mamlaka.
Na leo hii,
onyo langu linaenda kwa kila kiongozi,
kila taasisi,
kila afisa,
na kila mwanachama anayelinda mfumo bila kuhoji:
Tusijenge taifa
ambalo utii ni muhimu kuliko dhamiri.
Kwa sababu taifa likifika hapo,
watu huacha kutetea ukweli
na kuanza kutetea mamlaka.
Na mamlaka yanapoanza kuogopa uwajibikaji, kufichiana
(cover-up)huanza.
Na cover-up inapoanza,
haki huanza kufa.
Na haki ikifa,
taifa linaweza kuonekana lina amani kwa nje
lakini ndani linaoza taratibu.
Ndugu watanzania wenzangu
Taifa lenye afya si taifa lisilo na wakosoaji.
Taifa lenye afya
ni taifa ambalo ukweli bado unaweza kupumua.
Uzalendo si kulinda makosa.
Uzalendo wa kweli
ni kulipenda taifa lako kiasi cha kuthubutu kukemea
kile kinacholiharibu.
Watu hatari zaidi katika jamii yoyote
sio tu wale wanaofanya maovu
bali wale wanaoyahalalisha,
wanaoyatetea,
au wanaonyamaza
kwa sababu wahusika ni “wa upande wao.”
Leo nauliza:
Tunataka kuwa taifa la namna gani?
Taifa linalotawaliwa na hofu?
Au taifa linalotawaliwa na haki?
Taifa la watu wanaotii bila kufikiri?
Au taifa ambalo dhamiri bado ina thamani?
Kwa sababu ipo siku,
vyeo vitaondoka.
Serikali zitabadilika.
Vyama vya siasa vitapita.
Lakini historia itabaki.
Na historia haina huruma
kwa viongozi waliochagua mamlaka
kuliko ubinadamu.
Tusije tukawa taifa
linalozika ukweli kwa kina sana
mpaka vizazi vijavyo virithi ukimya wetu kama mateso yao.
Kwa sababu…
Hatia haina kaburi.
Rev Peter Simon Msigwa
Iringa
HONGO zilizotolewa Kahama kudhibiti mkutano wa Chadema:
1. NMB walikuwa wanagawa majiko ya gas bure.
2.Bodaboda walipewa leseni bure.
3. Mama ntilie wamegaiwa Michele na unga.
Watanzania wa wamechukua wamekwenda mkutanoni.
Geita msg zilitumwa ktk simu wa watu. Haikusaidia.