INAENDELEA HAPA…
So, tunaendelea tulipoishia, au siyo?
8. Kama wewe hauna urithi wa biashara, asset ama mtaji kama nilivyokuwa mimi, basi njia yako ni ngumu zaidi. Tumia akili, elimu, uzoefu na maarifa yako yote kubuni wazo linalofaa. Ukiishakuwa na wazo na ukajua unahitaji nini, sasa utajua unapataje mtaji. Mtaji hupatikana kwa kuweka akiba ama kukopa.
9. Njia ya uhakika zaidi na rahisi zaidi ni ya kuweka akiba yako Mwenyewe kuliko ya kukopa, maana siwezi kukushauri uitwishe mzigo wa madeni biashara yako changa. Itakufa kabla ya kushamiri. Kwanza, wakopeshaji huwa hawapendi kukopesha biashara mpya kabisa.
10. Kama una mshahara/kipato cha say 1,000,000/-, ugawe mara tatu; anza ku-save 400,000/- kila mwezi, 300,000/- Pango na mahitaji ya jumla, na 300,000/- matumizi binafsi ya kila siku. Hii 400,000/- unaweza kuweka kwenye scheme ya Fixed Deposit ama UTT Liquid funds.
10. Usiwe na haraka sana na maisha. Una mwezi mmoja kazini, hata haujathibitishwa, ushaanza kuwaza upange nyumba upande wako, uoe, uwe na kiwanja, uwe na shamba, uwe na mradi, uwe na mademu wawili, ukae bar kila siku baada ya kazi, ununue vitz, paso ama subaru - kila siku unakesha mtandaoni ku-search magari used! Badala ya kuishi gheto na wasela, mkajipikia na kwenda kazini kwa daladala, badala ya kuvaa kadet, mashati yako meupe/blue na blazer zako za mtumba, tai ya mtumba, unataka uishi maisha sawa na Meneja wako!
11. Wakati wa kujitafuta, kama una mwanamke basi awe ni mchumba wako - atakayekuelewa hali yako na atakayekuwa tayari kukuvumilia. Ishi modest life. Usijikweze ili uweze kuweka akiba, la sivyo utaona 1m haitoshi, na hata kama mshahara wako ni 2m bado hautotosha!
12. Ukiisha-save, badala ya kuwahi kununua gari ya kutembelea (liability), ama kiwanja cha kujenga nyumba (liability), nunua kiwanja ama shamba ambalo utajenga asset yenye kuingiza hela - kwenye ile idea yako uliyochagua!
13. Ukinunua shamba/kiwanja, hakikisha unasajili unapata hati. Ili ukijenga chochote hapo, kama ni godown la kutunzia mazao, mabanda ya kuku, bata, Sungura etc, ama mazizi ya ng’ombe, basi yawe asset zenye kukufanya uweze kukopesheka.
14. Uzuri wa kujenga, utakuwa unajenga taratibu- tofali baada ya tofali, mpaka utakamilisha. Siku ukikamilisha utakuwa umepata dhamana itakayokuwezesha kukuza mtaji wa biashara yako.
15. Ukiwa unaanzisha biashara yako sajili ‘vehicle’ (kampuni) kisheria kabisa.
16. Kama haujaajiriwa, unaweza kuanzia shambani, mgodini, kiwandani, jitahidi tafuta cha kufanya kwa kutumia nguvu zako, elimu, ujuzi, maarifa yako, chochote kinachopatikana nyumbani.
17. Tabia njema, uaminifu, uadilifu, uchapakazi, ubunifu na kujitoa hufanya njia ya mpiganaji kupata ahueni. Usitangulize pesa/ujira kwanza, imarisha urafiki na mahusiano mazuri na watu. Vaa hizi values, utanishukuru baadaye. Kuna uhaba mkubwa wa watu wazuri wenye tabia njema, ukiwa mmojawapo, lazima utatobowa tu!
#HK #Fighter #NjeYaBox #NasimamaNaSamia #NasimamaNaMama