Na ufisadi, wizi, rushwa, na mengine tulijifunzia hapa hapa.
Viranja walianza ka kujimegea top layer kwanza, kisha wengine wote.
Ili upate nafasi ya kufanya kazi jikoni ambako kuna uhakika wa msosi mzuri, ulihitaji kuhonga kwanza.
Ili uchaguliwe kuwa kiongozi wa meza mwenye jukumu la kuchukua na kugawa chakula, ulihitaji kuhonga.
Ni kipindi pia tulijifunza kuiba kupitia nafasi zetu za kiuongozi pasipo kuchafua mikono yetu.
Yani wakati unagawa chakula jikoni tayari umeshaandaa wasela kama 10 hivi. Unatoa portion ya ziada kwa kila mmoja kisha mali zinaenda kukusanywa nje. Ndani unaonekana msafi kumbe jizi lililokubuhu.
Ndio kipindi tulichofundishwa upendeleo pia. Wapo tuliowapa portion ndogo na wengine kubwa; wapo tuliwapa portion mbaya na wengine nzuri. Wasela wetu tuliwapa vizuri, wengine walikula mabaki.
Ndipo tulipojifunzia ubabe wa madaraka pia. Kiranja aliweza kuamua tu kuwa leo hauli kwa sababu jana ulimnyima blue band na ikawa hivyo.
Ndipo tulipojifunza kuwa viongozi hawastahili kuishi kama wanaowaongoza. Wao hawakula messini, hawakugombania chakula, etc.
Hii ndio ilikuwa hidden curriculum ya elimu yetu na ilifanikiwa kutengeneza character ya majizi kuliko elimu ya darasani.
Nimetoka gereza la mahabusu Segerea kuwaona wanachama wetu Mwalimu John Pambalu, Colletha ntyidicha na Pendo kileo. Mungu ni mwema wako imara sana na imani yao haijatikisika. Moyo wangu umelowa Machozi pale Pambalu aliponiuliza "Mwaipaya amepatikana?"
WATU WANAJADILI HUKUMU YA YESU NA HAWAKUWEPO KWA PILATO:
Jaji Mkuu GEORGE MASAJU anapaswa kufahamu kwamba; WATU WANAJADILI HUKUMU YA YESU NA HAWAKUWEPO MAHAKAMANI, LAKINI WANAMLAUMU PILATO. Kwa hiyo, kujadili HUKUMU YA TUNDU LISSU, siyo KOSA.๐๐
Kama unaamini serikali hii ya CCM, chini ya Samia inaweza kuleta KATIBA yenye tija kwa nchi, itakayoweka misingi ya usawa na uhuru wa kisiasa, uhuru wa mahakama, kupunguza madaraka ya Rais, kama unaamini hivyo utakuwa una funza kichwani.
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.
Wasanii wenu wanakuja na bonge la kampeni la Afcon. Na wimbo wamefanya kwa kutumia pesa za walipa kodi.
Wasanii wenu na influencers ndio wanaenda kutumia kuitoa nchi nzima kwenye reli kwa kuitumia Afcon ili huku nyuma wauwaji waendelee kujimilikisha nchiโฆ.
Tusikubali kufanywa wajinga na wasanii kwenye hii AFCON.