@millardayo Sasa hili bonde la Mzakwe limechukua eneo kuuubwaaa wana mpango gani nalo?Bora wagawe viwanja wananchi wajenge na serikali ikisanye kodi kwa malipo ya ardhi
Anaandika Askofu BENSON BAGONZA (PhD)
NILIWAHI KUSEMA; sasa NAJIFANYA KURUDIA.
Mropokaji kama mimi akianza kuishiwa huwa anakumbuka aliyowahi kusema huko nyuma. Nami nimeishiwa, naona nijikumbushe niliyowahi kusema.
Nilisema na kushauri kuwa Mamlaka husika isaini hati yenye mamlaka ya muda maalum (Executive Order), ya kuondoa zuio la kisheria (Declasiffication), la kuchapisha taarifa zinazohusu utawala uliopita hasa kuanzia siku ya kuugua hadi kuzikwa kwa Rais wa Awamu ya tano (JPM). Naamini Sheria ya Usalama wa Taifa inazuia ndiyo maana nashauri zuio liondolewe.
Kwa nini naota mchana hivi?
1. Ulianza uvumi mitandaoni, akafuata CDF Mstaafu, akaja Mpina Bungeni, na sasa kaja “kichaa” Polepole - wote wanazungumzia mambo ya kutisha kuhusu kifo cha Rais na njama za kumzuia aliyepo sasa asiapishwe.
Hatujui kesho ataibuka nani na atasema nini. Mambo ni matamu na rahisi kuyaamini kuliko kutoyaamini. Kimya hakisaidii.
2. Usalama wa Mkuu wa nchi (Hata angekuwa amejiweka kwa nguvu), ni suala nyeti sana. Tukifika hapo tuache tofauti zetu kwa muda na kutafakari. Hata Rais mbaya hatutaki auawe ofisini. Tunataka abaki hai ili siku moja “tumbanange na kumbagaza” kwa ubaya aliotufanyia akiwa ofisini.
3. Uchapishaji wa taarifa hizo utasaidia kutupa uzoefu wakati wa makabidhiano ya madaraka bila kujali ni wa chama gani. Usiri unalipokonya taifa elimu muhimu ya kutusaidia hapo baadaye. Tusidanganyane, hata makabidhiano ndani ya chama kimoja ni mshike mshike.
4. Uchapishaji wa taarifa hizo utapunguza nguvu ya watu binafsi na kuimarisha nguvu ya taasisi ya urais. Hivi sasa watu wachache walio karibu na taasisi hiyo, wana taarifa zinazowapa nguvu hata ya kumtisha rais. Chukulia daktari wa rais, mpishi, walinzi, makarani, madereva, waganga wa kienyeji wa marais, wafanya biashara wakubwa, wanasheria na hata wenzi wa marais. Usiri unawapa nguvu watu na wanalilingia taifa.
5. Taifa letu linakomaa na kurejea tena utotoni ghafla. Kutokana na mmomonyoko mkubwa wa maadili; upo mgongano usioepukika kati ya wanaodhaniwa ni wazalendo na wale wanaodhaniwa si wazalendo. Kila sekta kuna mgongano huu hata ndani ya makundi ya majambazi. Uwezekano wa kuibuka “Polepole Treaty” kila sekta ni mkubwa endapo usiri utaheshimiwa kuliko uzalendo. Kuna baadhi ya watu nawafikiria wakiamua kufanya kama Polepole itakuwaje?
6. Pamoja na “maujinga ujinga” yetu tuliyo nayo, sisi ni taifa na lazima tulilinde. Ifike mahali, raia wajione salama kutuhumu na kubaki ndani ya nchi na wawe salama. Ikiwa kwa kutuhumu, wamevunja sheria, basi washtakiwe. Wanaoshauri kwamba watu wanaotuhumu au kukosoa wasiwe salama, hawawatakii mema wale wanaodhani wanawatetea. Usalama na ustawi wa viongozi wetu wa taifa, ni kupendwa kwa hiari na kuungwa mkono na wananchi.
7. Upo mgongano mkali wa kimaadili. Yaani umeapa kutunza siri halafu unaona uhalifu uliofanywa kwa siri. Kuusema huu uhalifu ni kosa? Hapa ndipo niliposema uzuri wa shetani aletaye habari njema kuliko malaika aletaye habari mbaya.Uhalifu wa kumdhuru kiongozi wetu ni siri ya taifa au siri ya wahalifu?
TUFANYE NINI?
a) Jinai haifi: Tupate Tume huru ili kama Polepole anazusha, wazushi walio njiani warudi nyuma.
b) Kuwa na wakimbizi nje si afya kwetu na kwao. Nalifahamu taifa moja linalosifiwa kuwa na maendeleo lakini miji mikuu ya nchi za Magharibi imejaa mamia ya wakimbizi toka taifa hilo. Kila siku wanachapisha na kuzua mambo mabaya kuhusu rais wao. Kazi ya rais imekuwa kujibu makombora ya wakimbizi wake. Tusifanye masikhara na jambo hili. Siku moja tunaweza kuongozwa na “wakimbizi” wakisaidiwa na wanafiki waliozunguka meza zetu.
c) Upinzani ndani ya CCM ni hatari kwa taifa kuliko upinzani nje ya CCM. Aliyeshauri CCM iendeshwe na dola mchawi wa taifa. Tuachane na maigizo ya uchaguzi na gharama zitumike kulinda raslimali zetu. CCM bila upinzani wa nje inageuka kuwa gulio la kuuza na kununua uongozi. Viongozi wanaopatikana gulioni wanageuka madalali wa raslimali na utu wetu.