Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana, amesema hayo kwenye mahojiano ya njia ya Simu yaliyorushwa Julai 15, 2026 na Saut Digital.
Fuatilia zaidi https://t.co/T7ylDFpYyk
#JamiiForums#Demokrasia#Sheria#Utawala
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Serikali inaendelea na uchunguzi kuhusu madai ya kutoweka kwa Mwanasiasa Humphrey Polepole.
Kauli ya Katambi inakuja ikiwa ni siku 274 tangu kutoweka kwa Polepole alfajiri ya Jumatatu, Oktoba 16, 2025 katika Makazi yake ya Ununio, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam hadi kufikia leo Julai 16, 2026.
Kupitia mahojiano maalum na AyoTV, Waziri Katambi amesema, “Katika hayo ya utekaji kulikuwa na sura nyingi, sura ya kwanza mambo ya utekaji yalikuwa yanafanyika na Watu wenyewe unakuta ni raia kwa raia labda ni ugomvi, uhasama, chuki ama ubabe na kwasababu wanatofautiana misimamo fulani fulani mwisho inaonekana imefanyika na Watu kutoka Mamlaka za Serikali, utakumbuka juzi mauaji ya James Temba (aliyekatwa kichwa) walisema Serikali imefanya, Super Sami alitekwa wakasema Serikali ila uhalisia ukagundulika sivyo, na mifano mingine mingi kama yule Bonge wa Kimara (Tarimo) haikuwa Serikali”
“Sisemi kwamba natetea tu Serikali, upande pia wa Serikali naweza nikafanya mimi Mwajiriwa wa Serikali kwakuwa nina visa na Mtu lakini sio kwamba nimetumwa na Serikali na wapo Askari ambao wamebainika kufanya makosa na wamechukuliwa hatua, Serikali haiteki inakamata na kumpeleka Mtu kwenye vyombo vya sheria”
Katambi ameongeza kuwa uchunguzi wa masuala ya aina hiyo unahitaji muda wa kutosha ili kuhakikisha haki inapatikana kwa pande zote zinazohusika.
“Ukiharakisha shauri haraka unaweza kuzika haki za Watu na ukichelewesha haki umeinyima pia haki hiyo, kuhusu Polepole taarifa ya mwisho Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilisema vinaendelea na uchunguzi na upelelezi juu ya jambo hilo na hata aliyekuwa anatoa taarifa hiyo niliiona kupitia Ayo TV, alisema inasadikika hakuwepo Nchini lakini kuna taarifa zinasema alikuwa Nchini kwahiyo kama ni kweli au sio kweli upelelezi unaendelea,”.
#MillardAyoUPDATES
Inauma kuona kijana amenusurika kufa kwa kupigwa risasi, lakini maswali bado ni mengi kuliko majibu. Uchunguzi umefikia wapi? Ukweli utawekwa wazi lini? Wananchi tunahitaji uwazi, uwajibikaji na haki. Ukimya hauondoi maswali. #Haki#Uwajibikaji
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amesema hatetereki kwa maneno au propaganda zinazoelekezwa kwake, akisisitiza kuwa mashambulizi hayo hayawezi kubadili msimamo wake.
Akizungumza leo Julai 15, 2026 nyumbani kwake Tarime, Mkoani Mara alipokuwa akiongea na Wanawake wa BAWACHA waliomtembelea kumfariji kufuatia kifo cha dereva wake, Suez Dani Maradufu, Heche amesema anayeshambuliwa ni yule mwenye ushawishi.
“Mchezaji mwenye mpira ndiye anakabwa, mnayoyaona mashambulizi dhidi yangu ni kwa sababu mpira uko hapa, hivyo msiwe na wasiwasi, sina muda wa kujibizana na Mtu, huwezi kuniyumbisha kwa maneno ya mtaani, ya kwenye khanga? Mimi nasonga mbele,” amesema Heche.
#MillardAyoUDATES
Mchungaji Peter Simon Msigwa aliyewahi kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM kabla ya kurejea Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, amesema kwa mtazamo wake falsafa ya 4Rs (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya) iliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan haijafanikiwa kufikia malengo yaliyokuwa yameahidiwa kwa Watanzania.
Katika makala aliyoichapisha leo Jumatano, Julai 15, 2026 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Msigwa amesema, "Serikali hupimwa kwa vitendo, si kwa kauli. Kwa msingi huo, naamini falsafa ya 4Rs imeshindwa."
Amesema maridhiano hayawezi kujengwa bila haki na bila kila upande kujisikia unasikilizwa, akidai hali ya kisiasa nchini imeendelea kuibua maswali kuhusu utekelezaji wa dhana hiyo.
Akizungumzia ustahimilivu, Msigwa amesema, "Taifa lenye ustahimilivu hujengwa na wananchi wanaoamini kuwa wako salama na sheria zinawalinda wote kwa usawa."
Hata hivyo, amedai matukio ya watu kutekwa au kupotea kwa baadhi ya wakosoaji wa Serikali yameendelea kuibua hofu na maswali kuhusu usalama na uwajibikaji.
Kuhusu mageuzi, amesema matarajio ya wananchi ya kupatikana kwa Katiba Mpya na mabadiliko ya mfumo wa kisiasa hayakufikiwa kwa kiwango kilichotarajiwa. "Mageuzi ya kweli hayapimwi kwa ahadi bali kwa mabadiliko yanayoonekana katika mfumo wa utawala na taasisi zake." ameandika Msigwa.
Akihitimisha chapisho lake, Mch. Msigwa amesema viongozi huhukumiwa kwa matokeo ya utawala wao badala ya falsafa wanazozitangaza. "Falsafa yoyote ya uongozi hupimwa kwa matokeo yake. Kwa mtazamo wangu, 4Rs hazijashindwa kwa sababu zilikuwa falsafa mbaya, bali kwa sababu utekelezaji wake haukuendana na ahadi zilizotolewa kwa Watanzania," ameandika.
ASANTENI WATANZANIA!
TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 50 ✌️
Ndani ya saa 96 sawa na siku 4.
Asanteni kwa mwitikio wenu mkubwa. Mpaka sasa, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 50 katika Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334 kwa ajili ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Huu ni ushahidi kwamba Watanzania wanaweza. Safari inaendelea. Kila mchango una thamani. Tuendelee kuchangia hadi tufikie lengo letu la TSh. Milioni 334.
✌️ @Sativa255
Wanaharakati wa mazingira nchini Kenya wametoa wito kusitishwa kwa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha bilionea Aliko Dangote, kwa madai kinaweza kuhatarisha mazingira.
Mradi huo wenye thamani ya USD bilioni 15 hadi 17 na uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta ghafi kwa siku, unahofiwa kuongeza uchafuzi wa mazingira na uzalishaji wa hewa ukaa, na hivyo kuhatarisha maisha ya watu wanaotegemea uvuvi na utalii.
Mara ya kwanza Alicia Lissu aliona namna mumewe (Tundu Lissu) alikuwa tayari kupigania haki kwa vyovyote vile, alikuwa mwanafunzi wa sheria akiwakimbia polisi.
Ilikuwa miaka ya tisini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alicia alikuwa chumbani mwake aliposikia mlango ukibishwa kwa nguvu.
"Tundu alikuwa akihema," anakumbuka. "Aliniambia, 'Nahitaji sehemu ya kujificha'."
Kulikuwa na maandamano ya wanafunzi chuoni, na polisi walikuwa wameitwa kuzima vurugu. Maafisa walikuwa wameleta mbwa.
"Nilivutiwa na ujasiri wake na namna alitaka kujihusisha na siasa za chuo kikuu," anasema.
"Nilimuambia, 'Tundu, unapaswa kuwa mwangalifu. Watu wanaweza kukudhuru'."
Hiyo haikuwa mara ya mwisho Alicia kujikuta akihofia usalama wa Lissu. Zaidi ya miongo mitatu baadaye, anazungumza akiwa nchini Ubelgiji. Maisha ya uhamishoni hayakuwa sehemu ya mipango yao. Vivyo hivyo, kukamatwa mara kwa mara, kushambuliwa kwa risasi 16 katika jaribio la kumuua, na sasa kukabiliwa na shtaka la uhaini.
Hata hivyo, anapotafakari maisha yao pamoja, kinachojitokeza si simulizi ya mwanasiasa aliyekuwa tayari kupoteza uhuru wake kwa ajili ya imani zake za kisiasa. Pia ni simulizi ya mke aliyeshuhudia gharama za kitaaluma na ya kibinafsi ya kuolewa na mwanamageuzi.
"Nilivutiwa na Lissu kwa sababu alikuwa mwerevu sana," Alicia Lissu anasema.
Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza wakati wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria, kabla ya kukutana tena walipojiunga na shule ya sheria Chuo Kikuu.
Walisoma pamoja mara kwa mara katika maktaba na wakawa marafiki wa karibu kabla ya kuwa wanandoa.
"Nilianza kuelewa mtazamo wake kuhusu kila jambo aliloliona kuwa si la haki."
Anaamini mtazamo huo ulitokana na malezi yake na pia kutoka kwa baba ambaye, "alichukia aina yoyote ya unyanyasaji au dhuluma kwa watu wengine".
Aligombea ubunge mwaka wa 1995 lakini hakufanikiwa.
Hata hivyo walipofunga ndoa mwaka wa 1997, Alicia tayari alijua siasa zingekuwa na sehemu muhimu katika maisha yao.
Mwaka 2008, Lissu alianza kuzungumza kuhusu kurejea kwenye siasa na kugombea tena ubunge.
Alicia anakumbuka kuwa hakuwa na hofu sana kuhusu uchaguzi, bali kuhusu kulea watoto.
"Kulea watoto wakati mume wako ni mwanasiasa si jambo rahisi," anasema.
Na kweli alikuwa sahihi.
Kutokuwepo nyumbani kwa muda mrefu kuligeuka kuwa jambo la kawaida huku Lissu akisafiri kote nchini Tanzania kutafuta uungwaji mkono kwa chama chake, Chadema.
"Mwaka mpya wa kwanza tuliouadhimisha tukiwa hatuko pamoja kama familia ulikuwa mwaka wa 2008," anasema.
Kadri mafanikio ya Lissu ya kisiasa yalivyoongezeka, familia ilimuona mara chache zaidi.
Lissu alichaguliwa kuwa mbunge wa Singida Mashariki mwaka 2010 na akajijengea sifa kama mmoja wa wanasiasa wa upinzani wenye msimamo thabiti.
Lakini Alicia anasema hali ilibadilika baada ya hayati Rais John Magufuli kuwa rais mwaka 2015.
Kadiri Lissu alivyoendelea kuikosoa serikali na kupinga sera za rais hadharani, kukamatwa kwake kukawa jambo la kawaida.
Alicia anapozungumzia mumewe, hata wakati kuna sintofahamu kuhusu kesi yake ya uhaini, Alicia bado anamwona yule kijana aliyekuja chumbani kwake chuoni akiwa anahema baada ya kukimbia maandamano ya wanafunzi.
Yule yule aliyeamini kuwa ni wajibu wake kupinga kile alichokiona kuwa si haki.
Usisafishe Pasi kwa Panadol, ni hatari kwa Afya kwani Panadol inapoyeyuka kwa moto, hutoa gesi zenye sumu kama Formaldehyde na Nitrates, ambazo zinaweza kusababisha Miwasho kwenye Macho, Koo na Ngozi, Maumivu ya Kichwa, Matatizo ya Kupumua na kwa muda mrefu, huongeza hatari ya Magonjwa Sugu kama Saratani.
Badala ya kutumia Panadol, tumia njia salama kama kuchanganya Baking soda na maji kutengeneza pasta laini, kisha ipake kwenye pasi iliyo baridi na uifute kwa kitambaa. Pia, unaweza kutumia Vinegar na Chumvi kusafisha mabaki ya uchafu kwa ufanisi.
Afya yako ni muhimu. Epuka kutumia kemikali zisizo salama kwenye vifaa vya nyumbani. Kwa usafi bora wa pasi bila madhara, chagua mbinu za asili na zilizo salama kwa mazingira na afya yako.
kitendo tu cha Mhe. LISSU kuwa Hai Hadi leo ni ishara kuwa MUNGU ni MKUBWA na ANATISHA kama nini🙌🙌🙌🙌🙏🙏
Labda SAMIA na genge lake la udalali wa siasa MSOGA UNITY wanaweza kujizima data na kuona tofauti na tuonavyo sisi
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Serikali ya Tanzania imesikitishwa na ripoti iliyochapishwa leo tarehe 13 Julai 2026 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha “BBC Africa Eye”.
Serikali imelaani vikali ripoti hiyo, ikisema imebeba maudhui ya upande mmoja, yaliyokosa ushahidi thabiti na yenye upungufu mkubwa wa taaluma na maadili ya uandishi habari.
Kupitia taarifa yake, Serikali imebainisha kuwa chombo cha habari cha BBC kimeendelea na mwendo wake wa kuitangaza vibaya Tanzania kwa kutumia pasipo kutoa nafasi ya Serikali kujibu kama kinavyopaswa kufanywa kwa mujibu wa sheria na maadili ya uandishi habari.
#MeaMswahiliUPDATES
ANAANDIKA ASKOFU BAGONZA
UONGOZI UNAOACHA ALAMA
Uongozi wa awamu ya tano uliacha alama. LAKINI njia zilizotumika kuacha alama, pia njia hizo ziliacha alama.
Unatakiwa uongozi unaoacha alama bila kutumia njia zinazoacha alama.
Mwachieni tu. Anazo alama za utawala ulioacha alama. Nimjuavyo, atafanya makosa yatakayopunguza umaarufu wake. Kumshikilia kunampaisha na kuwashusha wanaomshililia.
Mantiki ni hesabu hata kama si kila hesabu ni mantiki.
Kwa nia njema na uzalendo kwa taifa langu.
Mjaluo anasema, “Mwanamke anayemwomba Mungu ili apate mtoto, huwa halali akiwa amevaa jeans”.
‼️ALERT‼️🚨
Hatimaye pesa za project ya kumshambulia Makam Mwenyekiti Mhe. John Heche zimemfikia Joseph Selasini.
Iko hivi jana Joseph Selasini alienda Masaki, nyumbani kwa Mbunge haram wa CCM Ojambi Didas Masaburi kwa lengo moja tu la kurekodi video ya kumshambulia Mhe. Heche, video hizo wamepanga kuziachia siku ya kesho yani July 14, 2026.
Kwenye izo video Selasini kamshambulia sana Mhe. Heche kwa propaganda zile zile za pesa za #ToneTone baada ya kumaliza kurekodiwa akapewa kibunda chake, wakapiga na moja moto, moja baridi kisha akaenda zake.
Kwahiyo kesho mkiona msishangae.
"Naomba nitume salamu na ninaamini hii ni kwaniaba ya Wazanzibar wote na Watanzania, nitume salamu kwa Waziri wa mambo ya ndani Patrobas Katambi, ambaye amefanya tufanye mkutano huu hapa Zanzibar bila sababu, kwa visingizio. Sisi tunachomwambia Waziri wa mambo ya ndani na tunachomuuliza ni kuwa fujo anaiogopa ni sawa, lakini anaogopa mpaka amani?"
"Mtu wa ajabu, vurugu, fujo kuiogopa ni sawa lakini unaogopaje amani? Unatafuta nini? Unachotaka nini? Maana anayefanya vurugu unamdhibiti watu wanakuelewa, huyu anayetengeneza amani naye unamuogopa? Nchi hii tusiiendeshe kwa kubahatisha, kuna mambo mengine ni aibu, ni fedheha kwa Tanzania hii. Tunaenda kama tumepata uhuru jana asubuhi."
'Inashangaza dunia nzima inafahamu kwamba Bunge ni kikao cha wananchi kuichunga serikali yao, serikali iende ikajibu ndani ya Bunge, kinachofanyika bungeni ni majadiliano, ile sio ofisi ya serikali, sio kijiwe cha serikali sasa leo Waziri wa mambo ya ndani amelifanya bunge kuwa kijiwe cha serikali, kuwa ofisi ya serikali, nyie mmepata wapi kusikia?"- Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman.