@dalalikiongoz Nitaitumia kufundisha watu twittani maswala ya teknolojia kwa kiswahili, hususan kuhusu simu, compyuta, intaneti na 'trics' ndogo ndogo za kuevolve na AI
Uwe Shabiki wa mpira, uwe Mwanahabari ama Mtu yoyote lazima tujenge utamaduni wa kutojadili MASLAHI ya Mtu mwingine kwa vile tunataka sisi, Wachezaji wanapaswa kujitambua kama hivi kwakuwa maisha ya mpira ni mafupi sana kuliko maisha ya nje ya mpira ambayo ni marefu zaidi.
Kama Simba tunaona KIBU hastahili hicho anachotaka basi hakuna haja ya watu kumwona yeye mbaya waachane kwa amani tu, ila kama anastahili basi apewe bila dhihaka, tusiwe na utamaduni wa kuwafanya wachezaji kusema NDIO kwa kila kitu, wameishi na wameona mifano ya wenzao huko zamani, wanaishi kwa tabu wengi wao.
SHABIKI unapaswa kufahamu mwenye mapenzi na timu ni wewe tu, ila Mchezaji yeye ni Mfanyakazi na wengi hawana kadi za Uanachama hivyo kwako ni starehe ila kwake ni biashara, unataka hii starehe basi ilipie, hampaswi kuingia kwenye mtego wa kumchukia Kibu bali kumpongeza kwa kupigania klabu na sasa ni wakati wa kupigania maslahi yake.
Kama alisaini Simba kwa kiasi kinachotajwa ni Million 200 kutoka Mbeya City, unadhani atabakia hapo? Jibu ni HAPANA! Ukimtoa Shabiki wengine woooote kwenye timu ni wapita njia tu, yupo kazini kwake aheshimiwe kwa kazi yake,huku ni kujitambua tunapaswa kuwapongeza saana Wachezaji wa aina hii.
Mbona klabu zinapowaacha Wachezaji mwishoni mwa mkataba huwa hakuna kelele? Kwanini tunakuwa WABINAFSI sana Wachezaji wakitaka thamani yao? Klabu zikiwaacha sio stori ila wao wakikomalia maslahi ni stori! Mwisho wa siku KIBU hatokula sifa wala mbio bali Pesa huko nyumbani kwake.
Tukianza kutambuana kwa asili sijui wapi umetoka sio afya sana kwenye mpira, KIBU kapewa uraia wa Tanzania sio uraia wa SIMBA, Kibu kapewa uraia na Mamlaka za kinchi kwakuwa ameonekana ana potential hiyo, sasa haipaswi kutumika kama fimbo nae kujiona Mgeni kwenye taifa ambalo limempokea, Utanzania wetu haupo hivyo, dhambi ya Ubaguzi ni mbaya mno.
@AbroadTanzania Mathayo 6:5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
Sina cha kuongeza hapo