🤷♂️Wauzaji wa simu original, na accessories zake.Mpya na Used.
🌍Ubungo Mawasiliano,near MamaHood
👨🎓International Business Personel
●IG:Kitonga_Phones
TOYOTA IST
Yeah 2007
Cc 1490
Mileages 98k
FM radio 📻
Excellence Condition
Full Documentary
New Tyre
Sports Rim
#Price 12.5m
☎️0786 518866
KINDLY REPORT 🙏
Naitwa Dr.Anord Christian, wa hospitali ya mkoa Shinyanga. Namuombea msaada huyu binti Neema (22) mzaliwa wa Bukoba lakini mkazi wa Shinyanga kwa sasa.
Historia yake ni ndefu kidogo. Ni yatima aliyelelewa na baba mdogo huko Ifakara Morogoro. Mwaka 2022 mlezi wake alifariki, hivyo akalazimika kurudi Bukoba kwa bibi yake.
Akiwa Bukoba alikutana na kijana mmoja ambaye alimpa ujauzito akajifungua 2024. Baadae alianza kupata maumivu na uvimbe kwenye taya. Mzazi mwenzie alimuaga anaenda Shinyanga kutafuta kazi ili aweze kumhudumia yeye na mtoto.
Uvimbe ulizidi kuongezeka hivyo akalazimika kumfuata mwenzie Shinyanga. Kijana alipoona hali ya uvimbe alimkimbia na hadi leo hajulikani alipo. Baada ya muda alifukuzwa walipokuwa wakiishi kwa kushindwa kulipa kodi. Akaanza kuhangaika mtaani akiwa na mtoto wa miezi 18 na uvimbe ukizidi kukua.
Muuguzi mmoja alimsaidia kumleta hospitalini. Vipimo ilionesha ana saratani ijulikanayo kama “Ameloblastoma” yani seli za “ameloblasts" kukua na kuharibu mfupa wa taya na kusababisha sura ya uso kubadilika.
Akifanyiwa upasuaji anaweza kupona kwa sababu ni saratani isiyosambaa. Tumempa rufaa ya kwenda Bugando, lakini hana uwezo wa kumudu gharama. Maisha yake ni magumu na tumekuwa tukimsaidia yeye na mwanae kuanzia malazi, chakula na matibabu.
Anahitaji upasuaji wa kuondoa uvimbe na sehemu ya taya iliyoathirika (Wide local excision). Kisha kurejesha muonekano (aesthetics) na kazi ya taya (function). Kwa cash gharama inaweza kuwa kubwa lakini akipata bima ya NHIF kifurushi cha juu cha Tanzanite (TZS 2,712,000/=) kinaweza ku-cover sehemu kubwa ya matibabu, zikabakia gharama ndogondogo.
#MyTake:
Maisha ya Neema hayajawa rahisi tangu utotoni. Kufiwa na wazazi na kuachwa yatima, kulelewa na baba mdogo naye akafariki, kurudi kwa bibi Bukoba, kupewa ujauzito, kuugua saratani, kukimbiwa na mwenzie kutokana na ugonjwa. Yote hiyo ni mitihani ya maisha. Hana ndugu wa kumlilia. Sisi ndio ndugu zake.
Tumchangie angalau 5M ili apate matibabu na kiasi kingine kimsaidie kujiuguza. Tuma sadaka yako kupitia M-PESA #0752581983, Tigopesa #0719744954, CRDB #0150633516500, NMB #24110012109 Gifted Hearts Foundation. RudishaTabasamu LetLoveLead.
Habari, naomba utusaidie kupost tumepotelewa na watoto wawili mapacha (msichana na mvulana) wanaoonekana kwenye picha. Wana umri wa miaka 12 wanafunzi wa shule ya msingi Kiembeni, Bagamoyo.
Waliondoka nyumbani tarehe 30/12/2025 saa 12 asubuhi kwenda shuleni (Shule ya Msingi Kiembeni), Kata ya Mapinga wilaya ya Bagamoyo lakini hawakurudi nyumbani. Katika jitihada za kuwatafuta, mabegi yao ya shule yalikutwa vichakani, yakiwa na nguo zao za shule ndani.
Tumetoa taarifa kituo cha Polisi Mapinga na kupewa RB namba MPG/RB/10/25. Yeyote atakayewaona tunaomba apige simu nambari 0655671105 au 0750525452toa au atoe taarifa kituo chochote cha polisi kilicho jirani yake.!
Kuna watu wana historia ngumu na za kustaajabisha mpaka unajiuliza kwanini yeye tu? Mmoja wao ni Mathew Peter Kijiu (40) mkazi wa Yombo-Vituka DSM. Mwaka 2020 akielekea kazini kwenye kiwanda kimoja cha vinywaji maeneo ya Vingunguti alipata ajali akiwa kwenye Bajaj baada ya kugongwa na daladala. Alivunjika mguu, na kwa sababu alikuwa kibarua tu (hana mkataba) hakupata msaada wa matibabu kutoka kwa Mwajiri.
Alijitibia kwa gharama zake hospitali ya Amana. Baada ya miezi mitano alipata nafuu akawa na uwezo wa kutembea japo kwa kuchechemea. Aliporudi kazini aliambiwa nafasi yake imeshapata mtu mwingine, atajulishwa ikiwa kutatokea nafasi za vibarua baadaye.
Akarudi nyumbani, miezi ikapita bila kuitwa kazini. Alipofuatilia akaambiwa bado hakuna nafasi. Akaamua atafute shughuli nyingine ya kufanya ambayo itamsaidia kuendesha familia. Kuna baadhi ya wafugaji wa kuku alikua anafahamiana nao maeneo ya Kitunda, akawaomba wampe mayai kwa mali kuauli. Anachukua mayai, anaenda kuuza, jioni anawalipa, kisha yeye anabaki na faida.
Mwaka 2023 akiwa amepakia mayai kwenye guta, alipata ajali maeneo ya Banana baada ya kugongwa na Suzuki Carry. Mayai yalivunjika na yeye akaumia kichwani. Alikimbizwa Amana lakini ikaonekana kesi yake ni kubwa hivyo akapewa rufaa ya MOI. Alifanyiwa upasuaji na kupona. Hata hivyo alipata changamoto ya kupoteza kumbukumbu mara kwa mara. Alitakiwa kuhudhuria kliniki mara moja kila mwezi kwa uangalizi wa madaktari.
Mwaka 2024 akiwa anashuka kwenye daladala pale nje ya geti la Muhimbili, akielekea MOI kwa ajili ya kliniki, aligongwa na pikipiki na kuumizwa mguu uleule aliovunjika awali. Alikimbizwa MOI na kufanyiwa upasuaji.
Hata hivyo tangu wakati huo bado kidonda ni kibichi na anatembelea magongo. Ameshindwa kurudi hospitalini kutokana na kukosa fedha. Anahofia kidonda hicho kugeuka kansa kwa kuwa kimekaa muda mrefu. Makadirio ya matibabu yake ni TZS 3M.
Ifanye sadaka yako ya kuanza mwaka 2026 iokoe maisha ya Mathew na Mungu aitumie kubariki kazi za mikono yako kwa mwaka huu. M-PESA #0752581983, Tigopesa #0719744954, CRDB #0150633516500, NMB #24110012109 Gifted Hearts Foundation. Rudisha Tabasamu Let Love Lead.