KUTOKA GEREZA LA RUANDA MKOANI MBEYA:
Leo niliwatembelea vijana wa CHASO Mbeya ambao wanatuhumiwa na mashitaka ya ugaidi na kushikiliwa gereza la Ruanda Mbeya.
Vijana wana afya njema. Nimewafahamisha kwamba Chama kilielekeza mimi pamoja na mawakili wenzangu ndani ya Chama kufanya kila kinachowezekana kuhakikisha wanapata utetezi wa kisheria mwanzo hadi mwisho.
Vijana hao ambao ni wanafunzi wa chuo ni Noah Mwalwange anayesoma “Project planning and Management for community Development”
Gwamaka Mboka - anayesoma Mechanical Engineering.
Augustino wasinyo - anasoma bachelor of Laws (LL.B)
Rojas Mpani - anasoma Bachelor of Art and Social work.
Nimepata maelezo yao kwa kina, leo si sehemu ya taarifa hii kwa kuwa yatatusaidia timu ya utetezi.
Yupo pia mwanachama anayejulikana kwa jina la Jasiri Mwasumbi - huyu ni dereva wa bodaboda, ambaye alikodiwa na askari Polisi na kuambiwa ampeleke kituo cha Polisi Meta na akawa amekamatwa hivyo.
Maelezo yake pia, yanahifadhiwa kwa matumizi ya utetezi.
Nimefanikiwa pia kuzungumza na mwanachama mwingine ambaye alikamatwa wilayani Chunya na kufunguliwa kesi huko lakini anashikiliwa Gereza la Ruanda, anajulikana kwa jina la Daniel Philemon. Awali makosa yake yalikuwa ya kimtandao lakini baadaye akapewa kesi ya Ugaidi kama wenzake.
Kesho vijana wa chaso pamoja na Jasiri Mwasumbi wataoandishwa kizimbani ambako kesi zao zitatajwa.
Wakazi wa Mbeya, marafiki wa haki na Demokrasia, kesho tukutane Mahakama kuu tuwape joto vijana wetu.
Tutamfikia kila mwanachama anaye bambikiziwa kesi hizi bila woga, tutapambana pamoja na nguvu ya umma itashinda inshallah!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 329
Job Mrema: Ni sahihi ubaguzi ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania?
Mnyika: Ni sahihi.
Job Mrema: Yale makusanyo ya Tonetone kuna uamuzi ulifanyika kuwa kuna wachache wanufaike na wachache wasinufaike angali wengine wapo?
Mnyika: Sio Ubaguzi. Na ungetaka walipwe wote ukirudi ofisini mshauri Boss wako mwanasheria Mkuu wa Serikali alipe pesa zetu zaidi ya Milioni 400 ili tuwalipe wafanyakazi wetu wote. Hizo posho ni ndogo tu.
Job Mrema: Zaidi ya milioni 39 za Tonetone zimetolewa kati ya Tarehe 18 na 19 August 2026?
Mnyika: Hizo Habari nazisikia kutoka kwako.
Job Mrema: Ikitokea wanachama wa Chadema wamepata ushahidi wakasema kuna pesa zimetoka huoni kiti chako kitakuwa rehani?
Mnyika: Tutasubiri kuona kama kuna aliyeidhinisha pesa kutoka ni nani na kwa sababu gani?
Job Mrema: Kutoa pesa za Tonetone kwa mujibu wa ibara ya 4.1.2 ni kuwaonea?
Mnyika: Anaisoma hiyo ibara. Inasema kukandamiza watu kwa rangi, dini
Job Mrema: Ndio maana wengine hamkuwalipa?
Mnyika: Mimi Katibu Mkuu ndio ninayejua kwamba kwa hali tuliyonayo. Alipwe Mlinzi pekee. Kwasababu yeye yuko ofisini kila siku na sio mfanyakazi mwingine. Wewe unajua nini kuhusu haya mambo kuliko mimi?
Job Mrema: Ibara ya 3.2.4 inasema kama inavyosema hapo?
Mnyika: anaisoma na kusema inasema hivyo.
Job Mrema: Sasa kama hizo fedha chache zimelipwa kwa ubaguzi unasemaje kuhusu hilo?
Mnyika: Sisi hatuna Ubaguzi wenye ubaguzi ni nyie Serikali ambao mmezuia fedha za Chadema. Ndio maana Chadema tunapambana fedha za umma zibaki salama.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kuwa ukiaminika kwa dogo utaaminika kwa kubwa?
Mnyika: Chadema inaaminika kwa dogo na kwa kubwa pia. Ndio maana watanzania wameendelea kuiunga mkono.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 346
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: Wakili wa Serikali Katuga anapenda kutoa mifano ya hovyo kabisa yani, kama shahidi alioa na akaingiliwa na Polisi ni ushahidi unaohusiana na kesi. Ushahidi wangu na ushahidi wa Mnyika unahusu kampeni ya uonevu wa Serikali dhidi yetu na Chama chetu. Kesi hii ni ya uonevu, ni ya uongo ni ya kisiasa na Serikali wamekuwa wanakamata watu na Viongozi wetu bila kufuata sheria, bila kuwafungulia mashtaka kwa nia ya kudhoofisha Chama chetu. Kifungu sahihi ni cha 7 , 8 , 9 cha Sheria ya Ushahidi. Hawa mawakili wa Serikali hawataki Jeshi la Polisi la Serikali wanayoitumikia liwe exposed, uchafu wao wanaoufanya kunyanyasa watu hawataki uwe exposed, sisi hatutakubali maana tumenyanyaswa sana mimi binafsi, Mbowe, Mnyika, Dr. Slaa na viongozi wengine.
Katuga: Anachokisema Lissu ndio maana ya kukinukisha sasa ; sisi tunaomba maelekezo ya Mahakama ila kama ushahidi huo ni wa muhimu kwa upande wa utetezi hatuna shida kwasababu tutapata nafasi ya kuuliza maswali ya dodoso.
Jaji Ndunguru anashauriana na majaji wenzake ameanza na Jaji Kareyamaha leo, kaenda kwa Jaji Kiwonde ngoja tuona, ila wamechukua dakika nyingi sana ni zaidi ya 10.
Jaji Nduguru baada ya majadiliano ya muda mrefu anasema tumesikia hizo hoja, tunaelekeza tuwe focused, wajibu wa prosecution ni kuthibitisha kesi, Mshtakiwa hana wajibu wa kuthibitisha utakatifu wake, shida ni kwamba upande wa utetezi huwa hawana statement kwamba labda ina guide upande wa utetezi. Jamhuri mna haki ya kufanya cross examination na hiyo ndio fair trial.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji tukio jingine la kukamatwa kwako.
Golugwa: Tarehe 08/11/2025 nikiwa nyumbani kwa wazazi wangu Arusha nilikamatwa na Polisi na nilipohoji kwanini wananikamata wakanitajia makosa matatu: ugaidi, kula njama ya kuharibu miundombinu ya umma na mali ya umma, kula njama ya kuwapiga askari wa vyombo vya dola, eti mimi huyu nipange kupiga askari? Shahidi anaongea kwa hisia na kujiuliza swali
Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya hapo?
Golugwa: Nilikaa Central Police Arusha kama masaa mawili na baadae nilisafirishwa hadi Oysterbay Police Dar es Salaam majira ya saa moja usiku, nilikataa kutoa maelezo hivyo niliwekwa lock up. Ilipofika saa nane usiku tena nilitolewa nikaambiwa kutoa maelezo, sikutoa maelezo na niliwaambia aje ZCO Mafwele ambaye nimefahamiana nae akiwa Arusha aje aseme kwa anavyonifaham kama mimi huyu Golugwa ninaweza kuwa gaidi.
Waheshimiwa Majaji kesho yake ZCO Mafwele alikuja akanishawishi nitoe maelezo na wakili Hekima alikuja nae akanishawishi nitoe maelezo, sikutoa maelezo na niliowaona na wenzangu hapo Lema, Boni Yai na John Heche. Tuliambiwa nendeni na kesho yake tulitakiwa kwenda kwa ZCO Mafwele Central Police station na baada ya kuripoti tuliambiwa nendeni na ikawa hivyo hadi leo
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji hatua gani Jeshi la Polisi limeshachukua hadi leo
Golugwa: hakuna hatua yoyote mpaka leo
Mhe. Lissu: Waeleze majaji hii kamatakamata inamaanisha nini kwako
Golugwa: nia yake ilikuwa kunitisha mimi na viongozi wenzangu ili tusifanye kazi yetu ya chama.
Mhe. Lissu: Waeleze ufahamu wako kuhusu matukio ya mimi kukamatwa ukichilia tukio hili lililoniweka gerezani
Golugwa: Mwaka 2012 nakumbuka tulikamatwa wote na kumwagiwa maji ya washawasha na kipigo Arusha, nakumbuka mwaka 2024 tulikamatwa Mbeya ulipoenda kwenye Maadhimisho ya siku ya vijana, tukio jingine lilitokea Arusha ulipokuja kumtetea Lema nakumbuka ulikamatwa, ulipotoa maoni yako kuhusu utawala wa Magufuli pia ulikamatwa uliposema Magufuli ni Dikteta Uchwara.
Part 347 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 345
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: Shahidi endelea kuhusu kilichokutokea 13/05/2025
Golugwa: Tarehe 13/05/2025 nilipokuwa Airport wakati tayari nimeshapewa boarding pass, nikiwa kwa afisa uhamiaji nilifuatwa na watu wawili wakasema twende ofsiini tuzungumze, wakati tunaelekea ofsini kwenye kibaraza walisema niko chini ya ulinzi, mmoja hakuwa na kitambulisho na alikuwa amevaa nguo za kiraia ndio alisema niko chini ya ulinzi, waliniingiza kwenye chumba na kuniacha. Kabla ya hapo walitaka simu zangu na huyu ambaye hakuwa na unifomu wala kitambulisho alizichukua zote.
Waheshimiwa majaji baada ya dakika kama 5 nikiwa kwenye chumba walikuja watu zaidi ya watano mmoja akiwa na bunduki, walifungua mlango wakapekua begi langu na wakachukua karasi mbili ambazo zilikuwa na hotuba ambayo nilipanga kwenda kuzungumza kule kwenye mkutano.
Waheshimiwa majaji pamoja na kwamba niliwauliza kwanini wamenikamata, kwanini wananipekua, kosa langu nini? Hawakunijibu kabisa, walinishusha underground pale airport , mwendo ulikuwa wa kasi sana, walinitukana sana “naomba nisiyaseme maneno haya mbele ya mahakama tukufu” mmoja aoiyekuwa na bunduki aliniwekea kwenye sikio la kulia na akasema “nyie wajinga ndio mnapanga safari zenu kwenda kuichafua nchi huko nje, sasa leo ndio utaelewa”. Sikupigwa ila nililazimishwa kutembea , naomba majaji mniangalie niwaonyeshe
Amani Golugwa anawaonyesha Majaji jinsi alivyoning’inizwa kwa kushikwa maeneo ya maungoni miguu ikawa haifiki chini ameonyesha kwa umaridadi kabisa
Waheshimiwa majaji baada ya hapo niliingizwa kwenye gari nikazungushwa kwa zaidi ya masaa mawili Airport na baadae nikapelekwa Stakishari Police station, niliwahoji kwanini mnanileta huku? Wakasema wewe ndio Lissu huwa anakutuma kwenda kuisema serikali huko nje na kupewa hela chafu kutoka nje hivyo wewe cybercrimes inakuhusu na money laundering.
Golugwa anaendelea kusema ilipofika saa nane usiku watu 10 walikuja kunichukua na walikuwa wote wapya nikawauliza mnanipeleka wapi wakawa hawajui na wakawa wananishangaa, walikuwa na radio call wakawa wanaongea wanasema tuko na mwewe, tulielekea kushoto kutoka Stakishari mimi nikiwa nimelala chini kwenye gari, baada ya muda tulifika Central Police Station Dar es Salaam na yule aliyekuwa anaongea na radio call akamwambia ZCO Mafwele kuwa mzigo huo.
Waheshimiwa majaji sikuwa sawa wakati huo kutokana na magumu niliyopitia na ZCO aliniongelesha kwa lugha nzuri ingawa mimi nilikuwa katika hali ngumu sana maana nilikuwa sielewi hatima yangu na nilipofikishwa tu wakasema cybercrimes na money laundering.
Waheshimiwa majaji niliulizwa kuhusu safari zangu mbili za huko nyuma za Mombasa na waliniambia kuwa nimekuwa nasafiri na kurudi bila kufuata taratibu na sheria za nchi, walinitaka nitoe maelezo, nilihoji sana na sikuwa tayari kutoa maelezo lakini mwishoni nilitoa maelezo na nikatakiwa nilete uthibitisho wa safari ya Mombasa ambayo nilisafiri na familia na wazazi wangu na nilipeleka uthibitisho kwa kupeleka nakala za passpoti.
Mhe. Lissu: mambo yote haya yaliishia wapi?
Golugwa: nilidhaminiwa na viongozi wa chama na nikaambiwa nenda nyumbani kwa amani. Hivyo safari ya kikazi ilivurugika na sikufanikiwa kusafiri.
Mhe. Lissu: waeleze kuhusu ukweli wa tuhuma hizo kama ni kweli au sio kweli
Golugwa; tuhuma hizo sio za kweli
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama kuna sheria inazuia wewe kusafiri kwenda nje ya Nchi
Golugwa: Hakuna sheria
Part 346 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 347
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: Katika Matukio yote ya mimi kukamatwa uliyoyasema, waeleze majaji kumbukumbu zako za mimi kutiwa hatiani kwa kosa lolote nililowahi kukamatwa nalo
Golugwa: sina kumbukumbu yoyote ya wewe kutiwa hatiani kwa matukio yote uliyokamatwa wala kushtakiwa nayo
Mhe, Lissu: Umenifahamu kwa muda gani?
Golugwa: Nimekufahamu kwa miaka 20
Mhe. Lissu: leo nashtakiwa kwa uhaini, kosa kubwa kuliko yote nchi hii, waeleze majaji kwa ufahamu wako uwezekano wa mimi kuwa mhanini kwenye nchi yangu
Golugwa: Waheshimiwa majaji kwa namna ambavyo namfahamu Lissu kwa hiyo miaka 20, ni mtu mwema sana na sioni uwezekano wa Tundu Lissu kuwa mhaini
Hapa shahidi ametiririka sana mpaka Majaji wamefurahi. Jaji Nduguru amesema CV yake Lissu ameshaitoa hapa Mahakamani.
Watu wamefurahi sana hizi dakika za jiooooni kabisa.
Mhe. Lissu: Kwa shahidi huyu nimemaliza maswali
Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama anasema hivi sasa ni saa kumi na moja kamili na kwa vile muda umeisha tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu kamili asubuhi kwaajili ya maswali ya Dodoso kwa shahidi huyu.
Jaji Nduguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi.
Inapigwa High Coouuuuuurt
Majaji wanatoka nje.
Mhe. Lissu anapack makablasha yake huku akiagana na Viongozi, Wanachama na Wafuasi wa CHADEMA waliokuja Mahakamani siku ya Leo.
Naomba Repost yako.
Jaji Mkuu (Mst.) FRANCIS NYALALI kwenye Kitabu Chake; “BUILDING THE RULE OF LAW” alisema; “JAJI HAPASWI KUWA MTOA MATAMKO KAMA MWANASIASA. JAJI NI MTOA HAKI”. Kauli hiyo ya Jaji NYALALI ina UMUHIMU SANA leo kuliko wakati mwingine wowote.
"Hao watu wanaosema kwamba @HecheJohn ananizuia mimi kutoka gerezani ni kina nani?. Waambieni hivi mimi nipo tayari kukaa gerezani mpaka haki itakapopatikana, huo ujinga! ujinga! wa hao wapokea pesa za Lumumba na ukome." Mhe. @TunduALissu
''Mmewaambia Watanzania ninavyowakumbuka? waambieni si muda mrefu nitarudi''
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Mh. Tundu Lissu, inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam. Shahidi wa pili wa upande wa utetezi, Mh. John Mnyika, anamalizia kutoa ushahidi wake kwa kujibu maswali ya dodoso kutoka upande wa Jamhuri.
#FreeTunduLissu
#KatibaMpya
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 335
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: Sasa eleza suala la kampeni za Uchaguzi huo zilikuwaje?
Golugwa: Kampeni za Uchaguzi huo zililenga kuegemea kukipendelea Chama kimoja. Chama cha Mapinduzi.
Mhe. Lissu: Uzungumzie matatizo ya wakati wa kampeni serikali za mitaa?
Golugwa: Kwa wagombea wachache waliopenya. Kampeni ziligubikwa na vurugu na ratiba kwa sehemu kubwa ilitengenezwa kimkakati kuvionea vyama vya upinzani. Na mara nyingi. Mikutano ya Chadema na vyama vingine vya upinzani iliionekana kufanyiwa hujuma kwa kupelekwa maeneo ya mbali na watu.
Mhe. Lissu: Utaratibu wa mawakala wa wagombea ulikuwaje?
Golugwa: Mawakala ambao wanamuwakilisha mgombea na Chama ulihitaji Wakala kwenda kuapishwa kwenye ofisi ya Kata akiwa na Barua ya Chama na baada ya uapisho ule utaratibu uliowekwa ni kwamba siku ya Uchaguzi msimamizi ndie atakaeenda na hati ya kiapo kwenye kituo cha kufanyia Uchaguzi kwahiyo Utambulisho Wakala utapelekwa kwenye kituo atakuta kiapo chake ambacho ndio utambulisho wake.
Mhe. Lissu: Na kilitokea nini?
Golugwa: Mawakala wa Chadema hawakukuta hivyo viapo ambavyo ndio Utambulisho wao. Kwahiyo msimamizi msaidizi kwenye kile kituo akawa watoa mawakala wetu hadi utambulisho wenu utakapopatikana na shughuli za Uchaguzi zilikuwa zikiendelea. Lakini watu wa CCM wao mawakala wake walikuwepo kila kituo na viapo vyao.
Mawakala wetu wakazuiwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura wakawa nje. Nendeni mkafuatilie huko.
Huo muda ambapo mawakala wetu hawapo ndani ndio ushenzi wa kuingiza kura ukafanyika. Niligombana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha saa sita Mchana Mkurugenzi anasema kulikuwa na shida kidogo lakini tumeshasort mambo yote yako sawa.
Mhe. Lissu: Sasa sema matokeo ya huo Uchaguzi kwa kanda ya Kaskazini na Nchi nzima kama unajua. Baada ya Ushenzi wote huu?
Golugwa: Waheshimiwa Majaji kwa nchi nzima CCM walishinda kwa asilimia 99.2 ya Vijiji na Vitongoji na Mitaa yote nchi nzima. Chadema na vyama vya upinzani waliambulia asilimia 0.8 na kwa kanda ya kaskazini walishinda kwa asilimia 98.7.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji tofauti ya Uchaguzi huo na ule wa 2019 kati ya ule wa Magufuli?
Golugwa: Kwa mambo mengi ya hovyo niliyoyaona na yaliyotokea. Katika mzunguko mzima hapakuwa na tofauti yoyote ya mambo yaliyotokea. 2019 suala la kurudisha fomu lilikuwa ni vita.
Part 336 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
LISSU AMECHAGUA HAKI KULIKO UHURU WA VIKAO VYA GIZANI
Kauli ya Tundu Lissu mahakamani kwamba yuko tayari kuendelea kukaa gerezani mpaka haki ipatikane si kauli ya mtu aliyekata tamaa. Ni kauli ya mtu anayejua kuwa kuna vitu vikubwa kuliko uhuru wake binafsi.
Amesema hataki kutembelewa gerezani usiku. Hataki vikao vya gizani. Hataki uhuru unaotokana na makubaliano yasiyojulikana na wananchi. Na amewataka wanaodai kwamba John Heche ndiye anayemchelewesha kutoka gerezani waache siasa za udalali.
Huo ni msimamo mzito sana!
Kwa sababu kama Lissu angekubali vikao vya gizani ili atoke gerezani, Watanzania wangeuliza:
Alipigwa risasi mara nyingi kwa sababu gani?
Aliishi uhamishoni kwa sababu gani?
Alisimamia “No Reforms, No Election” kwa sababu gani?
Alikataa kunyamaza wakati wengine waliogopa kwa sababu gani?
Na leo angekuwa gerezani kwa sababu gani?
Hawezi kulipa gharama kubwa kiasi hicho, halafu mwisho wa safari akubali kubadilisha damu, maumivu na matumaini ya Watanzania kuwa bidhaa ya biashara ya kisiasa.
Kwa Lissu, kutoka gerezani pekee si ushindi. Ushindi ni kutoka gerezani bila kuisaliti dhamiri yake, bila kuwasaliti Watanzania na bila kuhalalisha mfumo alioupinga kwa maisha yake yote.
Huyo ndiye mtu anayelipenda taifa lake. Anaweza kupewa uhuru kwa masharti, lakini anakataa kwa sababu hataki mwili wake uwe huru huku dhamiri yake ikiwa imefungwa. Anajua kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kufunguliwa mlango wa gereza na kuipatia nchi haki.
Martin Luther King Jr. aliwahi kusema:
“If a man has not discovered something that he will die for, he isn’t fit to live.”
Kwa tafsiri rahisi: Mtu ambaye hajagundua jambo analoweza kufa kwa ajili yake, bado hajagundua maana kamili ya kuishi. Kauli hiyo ilitolewa katika muktadha wa mapambano yasiyo ya vurugu na msimamo dhidi ya mfumo dhalimu. National Constitution Center
Lissu ameonesha jambo ambalo watawala wengi hawalielewi: si kila mtu ana bei. Si kila mtu anaweza kununuliwa kwa ahadi ya uhuru, cheo au usalama. Kuna watu ambao wanaweza kufungwa, lakini hawawezi kutekwa dhamiri. Unaweza kuifunga miili yao, lakini huwezi kuyafunga mawazo yao.
Aibu si ya mtu aliyeko gerezani kwa kusimamia anachokiamini. Aibu ni ya watawala wanaolazimika kutumia gereza, vitisho na vikao vya gizani ili kujibu hoja za kisiasa.
Lissu akiwa gerezani lakini akisimamia ukweli wake ni huru zaidi kuliko watawala wanaotembea nje, lakini ni wafungwa wa hofu, madaraka na dhamiri zao.
Historia haitakumbuka tu kwamba Lissu alifungwa. Historia itauliza: Alifungwa kwa sababu gani, alisimamia nini, na wale waliomfunga walikuwa wanaogopa nini?
What a stand!
Huu si ukaidi. Huu ni uaminifu kwa dhamiri.
Huu si ubinafsi. Huu ni upendo kwa taifa.
Huu si udhaifu. Huu ni ujasiri wa kukataa kuuza mapambano mezani gizani.
Unaweza kumweka Lissu gerezani, lakini huwezi kuweka ukweli gerezani.
Sijawahi kufanya video kwa ajili ya Chadema hii ndio ya kwanza.
Chadema tunaomba msituangushe kwenye hili. Watanzania tumezika watu kwa ajili ya haki sio kwa ajili ya Lissu kutoka ndani au kwa ajili ya Chadema kufanya siasi.
Hongereni sana CHADEMA!
Hata siku mkianza kupata ruzuku msiache Tone tone in fact mkiwa madarakanuli FUTENI ruzuku - hii ndo future ya siasa!
Ukiaminiwa unapewa sapoti na jamii!
Na vyama vyote vinatakiwa visipewe ruzuku - mbona briefcase vyama vitakufa mapemaaa?
Eniwei #TutaelewanaTu
Ndugu wanachama wa CHADEMA na Wapenzi wa Demokrasia Nchini.
Chama chetu kimefunguliwa rasmi kufanya shughuli za siasa. Hii ni fursa muhimu katika kuendelea na mapambano ya haki, uhuru na uwajibikaji katika Taifa letu.
Lakini ukweli usioepukika ni huu
hatuna ruzuku hata ya SENTI MOJA.
Hii ina maana kwamba uhai, nguvu na uendelevu wa CHADEMA uko mikononi mwetu sisi wenyewe.
Hatuna budi kuchukua jukumu.
Hatuna budi kusimama.
Hatuna budi kuchangia.
Kila Mwanachama na kila mpenda Demokrasia ana wajibu wa moja kwa moja, kuchangia CHADEMA.
Usione mchango wako ni mdogo.
Usisubiri mwingine achukue nafasi yako. Kila senti unayotoa ni nguzo ya kusimama kwa chama hiki.
Tujenge utamaduni wa kuchangia bila kusukumwa. Tujenge tabia ya kusaidia chama kila wakati. Hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli wa kisiasa na kiutendaji.
Mimi nipo, na nimeanza.
Na wewe pia ni wakati wako sasa.
Chukua hatua.
Anza kuchangia.
Simama na CHADEMA.
Kwa pamoja, tutakijenga chama imara na Yaifa lenye HAKI.
Tuchange tu kwa namba maalumu za CHAMA na Akaunti za Benki ili kujenga uadilifu wa Taasisi Imara.
Mikakati zaidi inakuja baada ya vikao kuanza.
Asanteni.
🚨 Heche akiwa Wasafi juzi kuhusu kususia uchaguzi:
🗣 Manara: Nyie kwenye uchaguzi mnataka mpewe nafasi ila mnasusia uchaguzi, mtapewaje nafasi?
🗣 Heche: Wewe ni Mwanayanga! Kuna muda mlikimbia uwanjani mkasema refa ni wa Simba. Nikuulize, siku wakasema Mangungu ni refa Yanga, mtaingiza timu uwanjani?
CHADEMA ina watu
Watu Wana CHADEMA rohoni
Huyu anafanya hii kazi sio kwa ujira maana ndio Kwanza CHADEMA imefunguliwa
Shughuli kama hii CCM ni mpaka mtu apate asali