COVID-19 ni vita ya 3 ya dunia. Ni vita ya Taifa na pia ni vita ya Familia. Ili tuweze kupambana vizuri na ugonjwa huu ni vema kila familia ikazingatia maelekezo ya wataalam wa Afya nchini Tanzania na Ulimwenguni!
Leo tumepokea LITA 2500 za Sanitizer na ndoo 50 za kunawa mikono kutoka kampuni ya MEGA Beverages Mkoani Arusha. Tumegawa magereza, vituo vya Polisi na vituo vya Afya.
Tutagawa pia Stendi za mabasi, Daladala na Sokoni!
Ni jukumu letu sote kupambana na Korona!