Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea tuzo kutoka kwa Askofu Mkuu wa kanisa la Philadephia Gospal Assemblies Dkt. Yohana Simon Masinga kwa ajili ya Rais Dkt. @MagufuliJP
kwa kutambua uongozi wake uliotukuka katika kuwatumikia Watanzania.
Tanzania imekubaliana na Namibia kuimarisha sekta za uvuvi na mifugo.
Makubaliano hayo yamefanyika Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Palamagamba Kabudi, amekubaliana na Naibu Waziri Mkuu wa Namibia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje Netumbo Ndaitwah
Spika wa
@bunge_tz
, Job Ndugai amewataka wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini kuacha mawazo ya kikoloni ya kusubiria kuajiriwa na badala yake waweze kujituma katika kujiajiri maana wanaweza.
Ameyasema hayo katika mahafali ya 22 ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbasi ametaka wasanii wasifungiwe ovyoovyo nyimbo na filamu zao bila kushirikishwa na badala yake, wawe wanaitwa kwa hatua ya kuelezwa kosa lao ili kuwasaidia badala ya kuwaadhibu.
Serikali kupitia Mfuko wa Barabara (Road fund), imesema ipo tayari kupitisha kiasi cha shilingi bilioni 4 kwa ajili ya kumlipa mkandarasi atakaepatikana ili kuboresha miundombinu ya Jangwani, mara baada ya uhakiki wa makisio hayo kukamilika na kujiridhisha.
Balozi wa Ufaransa Clavier akimkabidhi Mhe. Prof Kabudi na barua kutoka kwa Rais Macron wa Ufaransa kwenda kwa @MagufuliJP
kumpongeza kwa kuchaguliwa tena. Ufaransa inatarajia uongozi wake huu wa pili kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Ufaransa.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ambazo zimeshuka ikiwemo petroli iliyoshuka kwa Sh 37.
Wanafunzi wanaofadhiliwa na shule ya St. Jude, Arusha wamesimamishwa masomo baada ya shule kudai imeshindwa kujiendesha kutokana na TRA kufungia akaunti zake ikidaiwa limbikizo la kodi. Awali shule ilisema haiwezi kulipa sababu haifanyi biashara lakini mahakama imeiamuru kulipa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge ametangaza kufanya mkutano wa wawekezaji na wafanyabishara wa mkoa huo ili kubaini changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua.
Kunenge amesema bado mkoa huo unafursa ya kuongeza pato licha ya kutokuwepo kwa rasilimali kama madini.
:: "@halimamdee is strong and patriotic lady today and ever. Wakati utasema" Jafari Michael, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi Mjini kupitia @ChademaTz mwaka 2015 - 2020.