Waliopewa kazi ya kuulinda mwili wa YESU kaburini alikolazwa walishudia kwamba wakiwa wamelala, walifika wanafunzi wake Wakamwiiba na kuondoka naye. Kwahiyo, sio maajabu kwa walinzi hawa hawa ambao vitendo vyao vimetendeka mchana kutwa kusikia wakishuhudia uongo.
Kuna taarifa kuwa serikali inapanga kuwashitaki watanzania kwa kesi ya ugaidi, zaidi ya watu 400 wako Osterbay Polisi wakisubiri kupelekwa mahakamani!
@SuluhuSamia@tanpol kama mnalitakia mema hili taifa acheni huo ujinga.
Kama mtaendelea basi tutakutana mahakamani!! #Mo29
@Liberatus80@SuluhuSamia And of course, Samia doesn't fit to be President as she was the Vice President under Magufuli for 5 years and few 3 months there later Constitutional President.
Kongole kwa kuteuliwa kwa Jaji Mteule George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania!
Rais Samia Suluhu Hassan alimtangaza rasmi jana, 13 Juni 2025, na ambapo uteuzi wake utafanywa rasmi kwenye halfa ya kiapo tarehe 15 Juni 2025 kwenye Ikulu ya Chamwino, Dodoma .
Jaji Masaju ana uzoefu mkubwa katika mfumo wa sheria wa Tanzania.
Kabla ya uteuzi huu, alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani tangu Januari 2025 na kabla ya hapo alihudumu kama Mshauri Mkuu wa Sheria kwa Rais na Pia kama Jaji wa Mahakama Kuu .
Amechukua nafasi ya Jaji Mkuu wa awali, Profesa Ibrahim Hamis Juma, ambaye alistaafu rasmi kuhudumu kwa zaidi ya miaka saba tangu uteuzi wake mwaka 2017 .
Changamoto zitakazomsubiri Jaji Masaju:
1. Kuimarisha uhuru na uadilifu wa Mahakama.
2.Kuboresha utendakazi wa Mahakama ya Rufani hadi katika ngazi za Mikoa na kuondoa mkanganyiko wa mgongano wa Maamuzi katika Mahakama ya Rufani.
3.Kuhakikisha usawa na haki kwa watanzania wote kupitia utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama kwa kuboresha zaidi maslahi ya Mahakimu na ,Kanuni ya Maslahi ya Mawakili
4.Kuondoa kabisa mambo ya kiufundi ya kisheria katika mahakama kuu na Mahakama ya Rufani na kuweka Mkazo katika utoaji wa haki.
5.Kuona namna bora ya Tanzania kurejea Mahakama ya Afrika pamoja na namna bora ya kutekeleza Maamuzi ya Mahakama za Kikanda na kimataifa.
6.Kuhakikisha Mahakama inalinda haiba yake kwa wivu mkubwa na kwamba hakuna mashauri yanafunguliwa kabla ya upelelezi kukamilika na zaidi kuifanya Mahakama kuwa Hekalu la haki na kimbilio la wananchi .
“Kongole Jaji Mkuu Mteule Masaju! Tunakuombea mafanikio mema katika kuongoza mfumo wetu wa haki kwa uadilifu na weledi.”
BAK Mwabukusi.
PRESIDENT- TLS