Utawala unaonuka damu za watu.
Mnataka kutawala watu kwa kuwajaza hofu, kuua, kuteka, kupoteza, kupiga na kudhuru watu wasio na hatia!!!
Mtatawala kwa mabavu kwa mda gani kabla ya umma kuwaadhibu kwa hasira kali mno.
Huyu mtu mmoja asie na silaha, anashambuliwa na askari zaidi ya kumi kwanini?
Kwasababu ya kuja kusikiliza kesi ya kiongozi wake.
Polisi zaidi ya KUMI wanamshambulia mwananchi mmoja.
Siku inakuja haya yote tutalipiza mara 10 zaidi. Hayawezi kuturudisha nyuma hata kidogo.
TUTAKUWEPO🫵😎
Wanayofanya POLISI nawaambia ni MBOLEA tuu ya kuchochea HASIRA zilizo ndani ya vifua vyetu kulipuka siku moja.
Hakika HAYUPO WA KUTUZUIA siku ikifika, na hiyo siku haipo mbali. Kitu pekee ambacho ninauhakika nacho UKOMBOZI wa hili taifa upo karibu sana.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Simba Day 2025 imekuwa ya kukumbukwa 🦁❤️
Shukrani za dhati kwa #Betway, wadhamini wetu wakuu, na washirika wote waliotuunga mkono. Pia tunawashukuru uongozi na Bodi ya Simba SC kwa juhudi kubwa za kuandaa Simba Day bora kuliko zote.
Na kwa mashabiki wetu wa nguvu, asanteni kwa kulijaza uwanja katikati ya wiki. Mmeonyesha kuwa Simba si timu pekee, bali ni nguvu isiyozuilika. Tunanguruma siku yoyote, muda wowote.
This is Simba #NguvuMoja !
Ogopa matapeli October hatutiki bila reforms, linda kura baki nayo nyumbani isiipoteze kwa kwenda kuitumbukiza kwenye masanduku haramu ya uchaguzi haramu na wa wizi, baki nayo nyumbani wakose cha kuiba! @TumeYaUchaguzi na @ccm_tanzania ndio majizi yenyewe!
Mimi sio mtabiri, sio mganga, wala sio nabii; natumia rationality, logic, pattern thinking, na IQ... Ipo siku 1 Watanzania watashtuka na kugundua kuwa hii sio nchi ya kikundi cha watu wachache... sio siku nyingi sana kutoka sasa.
Kanisa Katoliki nchini Tanzania limetangaza kufanya sala na mafungo siku ya tarehe 23 Agosti 2025 kwa ajili ya kuombea Haki na Amani nchini. Wito huo umetolewa rasmi na baraza la maaskofu la Kanisa hilo hapa nchini (TEC) kupitia barua itakayo sambazwa kila parokia na kila kigango
Leo nimepata fursa ya Kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam
Nimeridhishwa kuwa Wananchi wengi wanapenda kufuatilia na kusikiliza shauri la Kiongozi wao wanaye mpenda na hawaendi Mahakamani kufanya vurugu.
Nimeridhishwa pia na utaratibu uliowekwa na Mahakama kwa kushirikiana na Mawakili husika katika shauri hili ya namna bora ya wananchi kuweza kuingia na kufuatilia shauri kwa Utulivu.
Pia kuna changamoto zilizojitokeza
1. Kuzuiwa kwa baadhi ya wadau wa haki za binadamu kutoka Kenya waliotaka kushuhudia Uendeshaji wa shauri hili. Jambo hili kifanyiwe kazi na lisijirudie kwani tunaweza tukafikiri na kuamini tunasaidia kumbe tuna haribu na kuharibia wengine.
2. Kutokana na Udogo wa chumba cha Mahakama ni vema kuwa na Spika au screen kwenye sehemu ya wazi ambayo wasioweza kuingia ukumbini waweze kufuatilia.
3. Pia Mahakama ione kuwa ni sahihi sasa kupitia mtandao wake waruhusu wadau wengine wa kidijitali kuweza kuonesha mwenendo live wakati wote.
Haki siyo tu itendeke bali idbihirike pasiposhaka kwa kuonekana kuwa haki imetendwa na imeonekana kutendeka.
Upande wa Utetezi
Mpare Mpoki naongoza Jopo la Mawakili
Akisaidiwa na;
Wakili Alute Mugwai
Lugemeleza Nshala
Peter Kibatala
Jeremiah Mtobesya (will join later)
Hekima Mwasipu
Gaston Garubindi
Michael Mwangasa
Jebra Kambole
Pasta Kang'oke
Emmanuel chengula
Deogratius Mahinyila
Michael Lugina
Deus Singa
Edward Heche
Sisty Masawe
Jacob Mugendi
Ferdinand Makoe
Paul Kisabo
Ikoti Lissu
Dickson Matata
Maria Mushi
Elisa Kiiza Prosper
Dorice Kafuku
Mathias Mndimi
Andrew Chima
Happiness Michael
Meshack Makadede.
Nashon Nkungu
Kwa hiyo Samia ameenda kumwambia Kikwete kwamba anapigwa spana na Mzee Warioba
Hivi Kikwete umeshindwa kumwambia Samia kwamba amevuka mipaka na ndio sababu ya kupewa hayo maoni
Samia amepuuza maoni ya watu kila mara hata Maaskofu, vikosi kazi na Wanasiasa wametoa maoni, USA imetoa maoni hata wewe Kikwete ulipewa maoni kuhusu #KatibaMpya kwa nini haya matatizo ya muda mrefu yaonekane mapya ?
Kuna kiburi kikubwa sana kwa watawala kisha baadaye mnasema watu wamevuka mipaka
Wajibikeni kwenye mambo ya Kitaifa
Magufuli pamoja na ukatili wake hakuua watu namna tunaona sasa alitoa kesi za uhujumu uchumi na kupora pesa za watu
Leo mauaji imekuwa mchezo mchezo tu , Magufuli ndio kilikuwa kipimo cha juu cha ukatili , ni misiba imekuwa kila siku
UPDATE KESI YA LISSU
Mheshimiwa Hakimu asubuhi ya leo na jana usiku tuliambiwa mwenenedo wa shauri hili utakuwa kwa mtandao na sio kwenye mahakama ya wazi. Tofauti kabisa na shauri. Hatujapewa sababu yoyote ya amri hiyo na maelekezo hayo ya kwamba tutasikiliza kesi hii kwa utaratibu huu wakati uko kinyume na sheria na Katiba yetu. Tunashangaaa sana kwakweli.
Pia ipo kinyume na Laws and Conventions.
Pia tumeona umma ukipigwa sana hapo nje na Polisi. Wamepigwa na kuumizwa. Sina taarifa kwa sasa wangapi wameuzwa kwa kuvunjwa miguu au style nyingine lakini ninachosema kwa sasa umma umezuiwa kwa watu kupigwa na kudharirishwa hapa mahakamani.
Pia waandishi wa habari wamekatazwa pia kuingia mahakamani na wengine wamekamatwa na kosa lao lilikuwa ni kuripoti kesi hii. Hatuna uhakika nani ametoa amri hiyo ambayo kiukweli kabisa tunasema ni amri ya ajabu.
Kanuni za mahakama ya wazi na open justice kwa ujumla inahitaji umma ufuatilie na kuona nini kinaendelea. Ni muhimu sana shauri kuwa la wazi.
Sasa mtuhumiwa ni mwananchama wa Chama kikubwa kabisa cha siasa. Namuona Wakili Kisabo anamwambia ni Chairman. Anasema yer ni Mwenyekiti wa Chama kikubwa kabisa cha upinzani hapa Tanzania, Chadema. Kwahiyo wapo wanachama na mashabiki wa chama hicho wangetamani kujua nini kinaendelea. Sasa kuifanya kesi hii iwe gizani kwa kuwanyima viongozi, umma na waandishi unaibua maswali yafuatayo.
1. Nani yuko nyuma ya hili zuio
2. Nani katoa hiyo amri
3. Imetolewa lini na kwa malengo gani?
4. Je utaratibu ulifiatwa kutoa hiyo amri.
Na pia tumeambiwa yupo mtu mmoja amefariki kwa kipigo hii leo. Sasa tunajiuliza nani yuko nyuma ya hayo mauaji na matendo ambayo yanafanywa kuwazuia watu mahakamani.
Tunahitaji majibu ya maswali hayo na majibu ya maana katika maswali hayo italeta imani kwa umma kuwa kesi hii inaendeshwa kwa haki, weledi na uwazi. Bila ya kupata majibu hayo hata umma utaiona mahakama kuwa sio eneo salama kwao.
Watu watakuwa hawana imani na Mahakama. Sasa mahakama lazima iseme.
Who made an order, why, when and for what purpose?
Mzee Mpale Mpoki anasema naishia hapa na nasubiri majibu kutoka kwa Mahakama ili umma uwe na imani na mahakama. Namkaribisha mwenzangu.
Anaingia Dr. Rugemeleza Nshala anaanza nae anapiga ngeli hapa.
Kwamba Mahakama imesemwa kwenye Katiba kuwa itakuwa ni huru na haitaamuliwa na watu wengine.
Kutoka Week iliyopita Kamanda Muliro alisema. Hakimu anamuingilia anasema naona unaenda mbali kidogo. Subiri. Mzee amechachamaaa Rugemeleza Nshala anasema wewe andika ndio kazi yako
Mzee anaendelea sasa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar ex salaam alitoa maneno umma usije mahakamani. Sasa kuhudhuria mahakamani na kushuhudia ni haki ya kikatiba na kisheria. Tumesema kifungu cha 186 cha CPA kuhusu umma kuruhusiwa. Sasa anapotokea mtu anajiita Kamanda wa Polisi anatangaza tu.
Na wewe kama member wa mahakama umeshuhudia umma unakatazwa kuingia. Na sisi tuliopo humu tumeingia kwasababu ni mawakili. Kwa kifupi ni kinyume na ibara 13(6) ya Katiba yetu.
Mahakama kupitia ibara ya 107 ndio itakuwa mwamuzi wa mwisho na itaamua kesi bila kujali status ya mtu yeyote. Hiki ndio chombo kimbilio cha wananchi na pia mahakama inapaswa kuwa huru kuamua mambo yake.
Hakimu anasema rudia kifungu anakisoma tena ibara ya 107(3) (b) ya Katiba.
Kwahiyo ninachosema mheshimiwa ni kwamba kesi hizi za jinai kwa mujibh wa Katiba na sheria zinapaswa kusikilizwa kwa wazi na umma ufuatilie kila kitu kwa haki kabisa.
#UpdatesKesiyaTunduLissu
"Tumefanya uchambuzi wa kina wa Kanuni za Uchaguzi na Kanuni za Maadili, na tumeona mapungufu makubwa. Kwa mfano, Kanuni za Maadili zinawalazimisha vyama kusaini makubaliano yanayokiuka Katiba, na kuwanyima haki ya kushiriki uchaguzi. Hili ni uvunjaji wa wazi wa haki za kisiasa!"
"Kwa hiyo, nawaarifu kuwa Chama chetu, kwa kushirikiana na asasi za kiraia, kitafungua kesi za kisheria kupinga kanuni hizi. Tutatumia kila njia ya kisheria na ya amani kupigania haki yetu! Zaidi ya hayo, tunawahimiza Watanzania wote kujiunga na mapambano haya."
"Hatutawahi kukubali kurudi kwenye uchaguzi wa 2019, 2020, au 2024, ambao ulikuwa aibu kwa taifa letu. Tumechoka na viongozi wanaoingia madarakani kwa wizi na jeuri sasa ni wakati wa viongozi wa kura za wananchi! Tuamke."
Mtu mmoja ameandika na kufikiri ,
Ramadhan Mapuri ni mmoja wa wajumbe wanaoitwa wajumbe wa Tume huru ya uchaguzi
1. Amewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM):
2. Amewahi kuwa Waziri wa Elimu (1985–2000):
3. Amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani (2003–2006):
4. Amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini China (2006–2012):
Kwa pamoja tujiulize mtu ambaye alishawahi kuwa na nafasi aliyonayo Amos Makala anaweza kutenda haki kwa vyama vya upinzani? je mtu ambae amewahi kuwa waziri kwa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM anaweza kutenda haki? kwa ufupi tujiulize Mwanachama wa CCM anawezaje kuwa sehemu ya kuratibu, kuendesha na kusimamia uchaguzi wa vyama vingi?
Tunaposema No reforms no election mtuelewe
#Free Tundu lissu Now
Katibu Mkuu @ChademaTz sitakuwepo kwenye kikao cha tarehe 12 Aprili 2025 cha kushauriana na kusaini maadili ya uchaguzi ya 2025.
Ifahamike kuwa mwenye mamlaka ya kusaini maadili ya uchaguzi kwa niaba ya chama cha siasa ni Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu sijateua kiongozi au afisa yoyote kwenda kushiriki kwa niaba yangu katika kikao hicho kitakachofanyika katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi @TumeUchaguziTZ Mkoani Dodoma. #NoReformsNoElection
G 55 ni Kundi la Wazee Makini ,Wazalendo wa Tanganyika na wqloweza kumwambia Mwl.Nyerere Wazi kwamba Serikali 3 Ndiyo suluhisho. Hawa ni mashujaa wa Tanganyika hawakutafuta fursa za Ubunge bali utaifa wao na Haki katika Muungano.
Ni vema watu wote timamu kwa Heshima ya Wazee wetu ikiwemo Jenerali Twaha Ulimwengu,Njelu Kasaka,Philp Marmo,Lumuli Alipipi Kasyupa na Wenzao tuache kutumia jina la G55 ili kulinda historia jadidi ya Tanganyika na urejesho wake.
Hawa walikuwa 55 ndiyo maana waliitwa G55 haiwezekani watu 7 au kumi kujiita G55 ni kubaka na kunajisi historia ya Taifa letu.
Mwanafunzi mzuri kabisa uliyepata Mwalimu Mbaya kabisa wa somo la Dini.
Ndugu yangu Musomage Biblia kwa Ukamilifu siyo kusoma kifungu kimoja na kutimka nacho mbio maandiko yana ruhusu kukataa kutii mamlaka au Mari isiyo na Utu au adili..Baadhi ya vifungu hivyo ni hivi hapa na kwa maslahi yako nitaandika mada pana kuhusu eneo hili ila kwa leo kajisomee
1. Danieli 3: 16-18 (Shadraki, Meshaki na Abednego):
Waliamua kutokubali amri ya mfalme Nebukadneza ya kuabudu sanamu, wakisema:
"Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na moto uwakao... lakini kama sivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa hatutakutumikia miungu yako..."
2. Matendo ya Mitume 5: 29 (Petro na Mitume):
Walipokatazwa kuhubiri jina la Yesu, walisema:
"Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu."
3. Kutoka 1: 17 (Wazalishaji wa Kiebrania):
Waliamua kutomtii Farao aliyetoa amri ya kuua watoto wa kiume wa Waisraeli, kwa sababu walimhofu Mungu.
Kwa mifano hii siyo sahihi kusema kwamba Biblia inasisitiza kutii mamlaka tuu bila kujali hali. Ni lazima kuzingatia kama mamlaka hiyo inafuata mapenzi ya Mungu katika kutenda haki au inakwenda kinyume.
KILA ASOMAYE NA AFAHAMU*
Huu Ni Mfano Halisi Wa TUME YA UCHAGUZI.
*Mechi Kali finally YANGA Vs Simba*
Zawadi ya mshindi ni *Kombe la dhahabu* matrioni ya pesa.
MO Dewji ndiye mteuzi, msimamizi,Mlipaji,muwajibishaji, Mdhibiti na *muapishaji* mkuu wa kamati zoote zinazosimamia Mechi ya Yanga na simba Ili ichezwe Kwa haki.
*Kamati* ya kusimamia Mechi ya Yanga na Simba Ili ichezwe Kwa *Uhuru na haki*
1.M/kiti WA Kamati Kaduguda
2.Refarii mkuu Azim Dewji
3.Marefarii WA pembeni yaani vibendera NI Murtaza Mangungu na Try again
4.Wanaosimamia VAR NI Ahmed Ally na Mwina Kaduguda
5.Wakuu wa Walinzi (Asikari) NI Crescents Magori na Swedi Mkwabi
6.Kamati ya masaa 72 NI DK zawadi kadunda na Sulemani Haroub
7.Wasimamizi wa Mechi yaani makamisaa Hussein kitta na ASHA Baraka
*Isitoshe uwanja umejaa mbigili na YANGA Yuko pekupeku Simba kavaa madaruga*
je Kwa Hali hii YANGA atatoboa? Ata kama ana timu Kali?