Hongera sana Ndugu Alphonce Lusako kwa kuaminiwa na kusajiliwa kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya.
Alphonce Lusako, ni mmoja wa vijana waliopambana sana katika safari yao ya elimu bila kukata tamaa.
Alifukuzwa chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2011 baada ya kuongoza harakati za kuwatetea wanafunzi waliokosa mkopo wa elimu ya juu. Wanafunzi hao walikuwa wamesajiliwa na bodi ya mkopo, na kusajiliwa chuoni lakini baadae walipata taarifa ya kutopata mkopo kwa sababu ya ufinyu wa bajeti ya serikali, na kwahiyo walitakiwa kujisomesha wenyewe au kuondoka chuoni.
Kwa sababu ya harakati zake za kuwatetea wanafunzi wenzake, Alphonce aliyekuwa mwanfunzi wa BCom & Account, na wenzake 11 walifukuzwa chuoni UDSM.
Alphonce alipambana sana kurudi chuoni bila mafanikio. Alifungua kesi mahakama kuu lakini hakupata majibu yotote kwa miaka 5 ya kesi hadi alipoamua kuondoa kesi ile mahakamani. Mwaka 2016 akiandika barua kwa Rais JPM ya kuomba msaada wa kurudi chuoni lakini hakupata majibu.
Mwaka huohuo wa 2016 aliomba upya usajili wa chuo kikuu UDSM, akasajiliwa kusoma Bachelor of Economic, ingawa alipofika chuoni alibadili kozi na kuanza kusoma Bachelor of Law (LLB). Hata hivyo miezi michache baadae, Januari 2017 alifukuzwa tena chuoni kwa sababu iliyotajwa kuwa 'alisajiliwa kimakosa'
Kuna sheria (au kanuni) ya vyuo vikuu inayozuia mwanafunzi akiyefukuzwa chuoni kusajiliwa tena. Nadhani inahusu vyuo vikuu vya umma. Niliwahi kusoma kanuni hii kwenye 'Prospectus' wakati nikiwa chuoni MUHAS. Nadhani ndio ilitumika kumfukuza Alphonce kwa mara ya pili.
Aphonce hakukata tamaa.
Aliamua kuomba usajili katika chuo kikuu kisicho cha serikali cha TUMAINI, ambako alisoma sheria na kufanikiwa kuhitimu Shahada yake ya kwanza Novemba 2020.
Kwa sasa Alphonce Lusako ni Wakili Msomi wa Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kumaliza Shule ya Sheria (Law School) ya Dar es Salaam. Pia ni Wakili Msomi wa Mahakama Kuu ya Kenya baada ya kuaminiwa na Mahakama hiyo.
Hongera sana Alphonce Lusako.
Kioo cha mapambano ya kutafuta elimu kwa vijana wa Tanzania.
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.
SIRI NZITO YA MGOGORO WA KOREA ๐ฐ๐ท๐ฐ๐ต: JINSI MAREKANI NA URUSI WALIVYO GAWANYA TAIFA MOJA
Endelea nayo ๐งต๐
Korea baada ya mvutano kuzidi ilibidi wahuni 2 raia wa marekani ambao walikuja na idea inayoitwa 38th Parallel.
Kuna utapeli mkubwa sana wa kiimani unaofanywa Tanzania.
Sikiliza vizuri hiki kisa anachokiongelea Mtaka na matokeo ya utapeli wa huyu nabiiโฌ๏ธ.
Hizi ndio tabia za matapeli wa madhabahu Tanzania, wakina Mwingira, Mwamposa etc., haijalishi wamevaa suti, kanzu, au mashuka!!
Nakusabahi @frediejustine mpwa!
Nimechukua muda na nimetafakari ila leo nasema na wewe hapa maana sitakutafuta tena!
Ulinisimulia kuwa ulienda kumsalimia Lissu gerezani na kumwambia chama kinaweza kufutwa mkiandamana, alikujibuje? Hakukuambia kuwa โAcha wafute chama!โ Uliwahi kumwelewa Lissu kwa nini haogopi na hajawahi kupiga magoti?
Mkumbuke Soka na alivyokataa kumpigia magoti Mwamba wenu! If he was asked whether he would do it again angesema โYes!โ
Hii ndo picha yangu ya mwisho nilipiga na Soka na alikuita mpige pamoja maana alikupenda na kukuamini kama rafiki yake! Leo uko front unapambania nini? How could you!?
Soka alijua the price he was going to pay for standing on the right side of history!
Je wewe unajua the price of standing on the side of the Opressor?
Jitafakari! Mungu akuongoze!
With sincere love
Shangazi Maria
Gigy money na mama yake kuna nini? Kinacho endelea mbona wanarushiana maneno makali huko mtandaoni.๐ญ๐๐ฟโโ๏ธ
But anyway kuna haja ya kumuongelea mama yako maneno makali hata kama kakukosea.?
Kama hoja ni kwamba WANAUME TU NDIO WENYE MAMLAKA YA KUBARIKI WATOTO kwa sababu Isaka na Yakobo walifanya hivyo;
Basi tunapaswa pia kuacha kwenda kanisani kuhubiriwa na wachungaji wa kichaga kwa sababu MAMLAKA HIYO WALIPEWA WALAWI tu.
Picha hii ya mwaka 1956 inaonyesha watu wawili ambao baadaye wangekuwa miongoni mwa watu mashuhuri na wenye utata mkubwa katika historia ya karne ya 20 ambao ni Fidel Castro na Ernesto โCheโ Guevara.
Kilichoifanya picha hii kuwa ya kipekee ni kwamba ilipigwa wakati ambapo dunia bado haikuwajua kwa majina waliyokuja kuwa nayo. Wakati huu pichani, Castro alikuwa na miaka 29, huku Che Guevara akiwa na miaka 28.
Castro alikuwa mwanasheria kutoka Cuba, wakati Guevara alikuwa daktari mzaliwa wa Argentina. Wote walikuwa nchini Mexico wakijiandaa kwa jaribio la kuipindua serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fulgencio Batista.
Fidel Castro alikuwa ameingia kwenye harakati za kisiasa Cuba na mwaka 1953 aliongoza shambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Moncada.
Shambulio hilo lilishindwa, Castro akakamatwa na kufungwa. Mwaka 1955 aliachiliwa kupitia msamaha wa kisiasa na akaondoka Cuba kuelekea Mexico, ambako alianza kupanga mapambano mapya dhidi ya Kiongozi wake Batista.
Huko Mexico ndipo alipokutana na daktari kijana kutoka Argentina, Ernesto Guevara.
Guevara alikuwa amesafiri katika maeneo mbalimbali ya Amerika ya Kusini na alikuwa ameanza kuvutiwa zaidi na siasa za kimapinduzi.
Alipokutana na Castro mwaka 1955, mazungumzo yao yalikuwa marefu na hatimaye Guevara akaamua kujiunga na mpango wa Castro wa kupindua Cuba kwa silaha.
Castro na wafuasi wake walikuwa wakifanya mafunzo ya kijeshi kwa siri nchini Mexico. Lakini mipango hiyo iligunduliwa na mamlaka za Mexico.
Mnamo Juni 1956, polisi wa Mexico waliwakamata Castro, Guevara na baadhi ya wanachama wengine wa kundi lao.
Vyanzo vya kihistoria vinaonyesha kwamba walipelekwa katika kituo cha mahabusu cha uhamiaji kilichokuwa katika Gereza la Miguel Schultz, Jijini Mexico City, Basi Na hapo ndipo picha hii ilipopigwa.
Kulingana na kumbukumbu za picha, picha hiyo inaonyesha Castro na Guevara wakiwa katika gereza la Miguel Schultz Julai 1956, na imetajwa kuwa huenda ilikuwa miongoni mwa picha za kwanza kabisa kuwaonyesha wawili hao pamoja.
Jambo la kuvutia zaidi ni kwamba picha hiyo haikuonyesha viongozi wawili waliokuwa tayari wamefanikiwa. Ilikuwa picha ya watu wawili waliokuwa wafungwa, wasiojulikana sana kimataifa, na ambao mpango wao wa mapinduzi ulikuwa karibu kuvurugika.
Baada ya Siku kadhaa, Castro aliachiliwa, lakini Che akabaki, Castro aliachiliwa baada ya takribani mwezi mmoja, huku Guevara akikaa kizuizini kwa muda mrefu zaidi.
Kumbukumbu nyingine zinaonyesha kwamba Castro na baadhi ya wenzake waliachiliwa tarehe 24 Julai 1956, huku Guevara akiendelea kushikiliwa kwa muda zaidi.
Baada ya kutoka, hawakuachana na mpango wao. Badala yake, waliendelea kukusanya silaha, Wafuasi wapya na fedha huku wakijiandaa kuvuka kwenda Cuba.
Mnamo Novemba 1956, Castro na wapiganaji wengine 82 waliondoka Mexico kwa kutumia boti ndogo iliyojulikana kama Granma, kuelekea nchini Cuba.
Walipofika Cuba tarehe 2 Desemba 1956, walivamiwa na majeshi ya Batista. Wengi waliuawa au kukamatwa, lakini kikundi kidogo kilifanikiwa kutoroka na kufika katika milima ya Sierra Maestra.
Miongoni mwa manusura hao walikuwa Fidel Castro, Raรบl Castro na Che Guevara, Na Kutoka kwenye kundi hilo dogo lililonusurika ndipo vita vya msituni vilipoanza.
Miaka miwili baadaye, kila kitu kilibadilika, Mapambano yaliendelea kwa zaidi ya miaka miwili. Hatimaye, tarehe 1 Januari 1959, Batista aliondoka Cuba huku vikosi vya Castro vikichukua udhibiti wa nchi. Castro aliingia Mjini Havana siku chache baadaye.
Na hivyo, watu hawa wawili pichani waliokuwa wamepigwa picha wakiwa wafungwa katika chumba cha mahabusu huko Mexico mwaka 1956, walikuja kuwa sehemu muhimu ya historia ya Cuba na Amerika ya Kusini.
Che baadaye akawa mmoja wa makamanda muhimu wa Mapinduzi ya Cuba, huku picha yake maarufu ya mwaka 1960 ikiwa mojawapo ya picha zinazotambulika zaidi za kisiasa duniani.