@Savasec Tatizo mnaweka Hisia mbele Hawa kina LISSU, maria, sativa,heche style zao za Maisha ni Biashara kwao na bidhaa inayouzwa ni Raia na matumaini!!
Wakifikia Ndoto zao tayaari
Refe: Fatma karume
Sometimes nawaelewa tu wanaume yaan wanawake wanasahau sana hata ukimtendea wema ni rahisi kukuumiza kuliko mwanaume,Mimi jinsi walivoniumiza hasa wanawake wenzangu nliojaribu kuwashika mkono sina hamu nkikuta mwanamke anagombana na nyoka nasimama na nyoka😏😏😏
Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.
Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.
Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.
Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.
Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.
Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.
Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.
Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.
Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.
Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha. Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.
��You don’t have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.”
Thank you !!
Huyo demu unayemyenyekea na kumuabudu:-
1. Anakunya mavi yananuka kuliko yako
2. Akijamba kinatoa harufu kuliko wewe
3. Atakufa na kuzikwa kaburini kama wewe
Mwisho hana bikra na alishagongwa na wanaume masikini kuliko wewe. Huna haja ya kujiumiza kiuchumi kisa malaya
Sioni tatizo kuona hii picha, ila maumivu yangu ni kwamba kuna vijana wengi nchini walikufa na kupotezwa wakimtetea na kumpigania Mbowe.
If you don't smell something fishy you might be a fish we are looking for!!
HII NDIYO LIBYA ALIYOIJENGA MUAMMAR GADDAFI. 🤝
Thread 🧵
Haya ni baadhi ya mambo ambayo Gaddafi aliyasimamia na kuyatekeleza katika utawala wake wa miaka 42 kwa Libya.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na tovuti za mawasiliano za Libya na Zimbabwe zimeeleza kuwa nchini Libya hakuna mwananchi aliyewahi kulipa bili ya umeme, umeme ulikuwa bure kwa raia wake wote.
Hakukuwa na riba katika mikopo, benki zote Libya zilikuwa chini ya Serikali, mikopo ilitolewa kwa wananchi bila riba ya kiasi chochote .
Taarifa hizo zikafafanua kuwa makazi ni haki ya msingi nchini Libya, Gaddafi aliwahi kusisitiza kwamba wazazi wake hawawezi kupata makazi hadi kila raia apate makazi. Baba wa Gaddafi alifariki dunia wakati yeye, mama yake wakiwa wanaishi katika hema.
Wanandoa wote wapya nchini humo walipata Dola 50,000 kwa Serikali kwa ajili ya kununua makazi yao kuwasaidia kuanzisha familia mpya.Elimu na huduma za kiafya vilitolewa bure. Wakati Gaddafi nachukua nchi asilimia ya waliokuwa na elimu ilikuwa 25, kwa sasa inafikia 83.
Kwa waliotaka kuwa wakulima, walipewa ardhi bure, nyumba katika shamba lao, vifaa, mbegu na mifugo kwa ajili ya kuanzisha miradi.Iwapo kuna waliokuwa hawawezi kupata huduma za elimu na afya wanazostahili, Serikali iliwalipia kwa ajili ya kuzipata nje ya nchi, hizi hazikuwa bure, walitakiwa kuchangia, walipata Dola2,300 kwa mwezi kwa ajili ya makazi na usafiri.
Kwa waliokuwa wakitaka kununua magari, Serikali ililipia kwa asilimia 50 ya bei. Bei ya petroli ilikuwa karibu na bure, lita ililipiwa kwa Dola 0.4.
Libya haidaiwi nje, pia ina akiba inayofikia Dola150 bilioni nje ambayo kwa sasa imezuiliwa.Kwa waliomaliza vyuo, Serikali iliwapatia posho sawa na mshahara wa maofisa hadi watakapopata ajira yenye uhakika. Sehemu ya mauzo ya mafuta ya Libya iliwekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya raia wake.
Kila mwanamke aliyejifungua alipata posho ya Dola5000, mikate 40 iliuzwa kwa dola0.15, asilimia 25 wa Walibya, wana shahada ya chuo kikuu.Kama hiyo haitoshi taarifa hizo zimeeleza kuwa alisimamia mradi mkubwa kabisa wa umwagiliaji, uliopewa jina la Great Man-made River, kuhakikisha maji yanakuwepo kwenye maeneo yote ya nchi yenye jangwa.
Wakati wa vikwazo kwa Serikali yake miaka ya 1980, Libya ilikuwa miongoni mwa nchi tajiri kabisa kwa msingi wa pato la ndani, ikwa na kiwango cha juu cha maisha kuliko Japan. Ilikuwa ni nchi tajiri kuliko zote kabla ya vuguvugu la mapinduzi.
Wastani wa kiwango cha maisha kwa pato la kichwa ni Dola11,314 . Gaddafi amewahi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya safari zake na miradi yake, lakini amefanya mabo makubwa ambayo hakuna dikteta aliyewahi kuyafanya kwa watu wake. Alirejesha pato kwa watu wake, aliwajali.
Usisahau Kunifollow @mudryk_jr na ku,turn on Notification 🔔
>Like❤️
>Repost🔄
>Comment!