Asante Mungu kwa kutuletea huyu binadamu kwakweli amesimama kanyoka sana bila kujali yatakayo mkuta kwani amemua kusimama upande wetu wananchi kutusemea.
CHANGIA CHAMA TONE TONE KWA NAMBA 0744446969 CHAMA KINAHITAJI MICHANGO ILI KIWEZE WATENDAJI WAKE WAWE KAZINI MDA WOTE.
Kinacho katazwa ni kutoa maelezo ambayo yataingilia mahakama katika kutoa maamuzi. Wakili ni afisa pekee wa mahakama aliyekaribishwa na mahakama kwa kulipia ukaribisho huo. Kama uwepo wa wakili unalipiwa kwa nini akatazwe kuongelea shauri lake ?
@Mwabuk2Boniface@Advocate_Jebra
Hii DUNIA Ikisha kutambulisha kama Mwanaume huwezi kukwepa gharama “
-gharama ya mafanikio.
-gharama ya Mahusiano&familia.
-gharama ya Utafutaji.
Kila kitu kitakuhitaji wewe bila uruma
STAY STRONG 💪.
Watanganyika, Tuamke Sasa!
Tusiendelee kumruhusu Muuaji Samia kuiharibu nchi yetu. Ameanza kuingia hofu ya kushindwa kumweka madarakani rais atakayemlinda pindi atakapo ondoka madarakani. Ndiyo maana sasa anatafuta kila njia ya kujitengenezea kinga ili asiwajibishwe huko mbeleni kwa makosa na madhambi anayoyafanya.
Bila kujali chama au itikadi, tuendelee kusimama na Dkt. Nchimbi, ambaye anaunga mkono #KatibaMpya, anapinga ugaidi na uhalifu wa kisiasa unaofanyika kwa maelekezo ya Muuaji Samia.
Kwa mustakabali wa Tanganyika, sharti tumuunge mkono Mtanganyika mwenzetu Dr Nchimbi kwa nguvu zote!
Kiongozi anayestahili kujiuzulu na kuwajibishwa ni Muuaji Samia.
#KatibaMpya #FreeTunduLissu
Heche Ahoji Ukimya wa CCM Kuhusu Utekaji, Asema Demokrasia Inahitaji Uwajibikaji
Akizungumza katika kikao na viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Jumatatu, Agosti 3, 2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. John Heche, amesema mazingira ya siasa nchini yamebadilika kwa kiasi kikubwa, akieleza kuwa ushindani wa hoja uliokuwa ukitawala miaka iliyopita umeacha nafasi kwa matukio ya utekaji, mauaji na ukandamizaji wa wanasiasa pamoja na wanachama wa vyama vya siasa.
Heche alisema jambo linalotia wasiwasi zaidi ni ukimya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho amesema hakijatoa kauli ya kulaani matukio hayo licha ya viongozi na wanachama wa upinzani kukumbwa nayo. Alisema kulinda haki za msingi za raia ni wajibu unaopaswa kutekelezwa bila kujali tofauti za kisiasa.
Akimjibu Katibu wa NEC, Organizesheni wa CCM, Paul Matiko Chacha, aliyesema CHADEMA ya sasa haina nguvu za upinzani kama ilivyokuwa wakati wa Freeman Mbowe, Agustino Mrema, Profesa Ibrahim Lipumba na Dk. Wilbrod Slaa, Heche alisema changamoto si nguvu ya upinzani bali mabadiliko ya mazingira ya kisiasa. Kwa mujibu wake, ushindani wa zamani ulijengwa zaidi kwenye hoja na sera, tofauti na hali ya sasa ambayo imegubikwa na vitendo vinavyotishia uhuru wa kisiasa.
Ukimya wa CCM umeendelea kujadiliwa katika matukio mbalimbali yenye maslahi ya umma. Hadi sasa, chama hicho hakijatoa tamko la wazi kuhusu kutoweka kwa Balozi Humphrey Polepole, jambo ambalo limeibua maswali kuhusu msimamo wa CCM katika kulinda haki za msingi na utawala wa sheria.
Wakati huohuo, mjadala mwingine umeibuka kufuatia mwitikio hasi uliomkabili Dk. Emmanuel Nchimbi baada ya kuzungumzia kwa msisitizo umuhimu wa #KatibaMpya. Kauli zake zimekosolewa na baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM, licha ya chama hicho kueleza mara kadhaa kuwa suala la Katiba Mpya limo ndani ya Ilani yake. Hali hiyo imezua mjadala kuhusu nafasi ya viongozi kujadili kwa uhuru ajenda za mageuzi zinazotambuliwa na chama chao.
Kauli za Heche zinaongeza wito wa uwajibikaji kwa viongozi wa kisiasa. Wananchi wanatarajia kuona misimamo iliyo thabiti katika kulinda haki za binadamu, kulaani utekaji na vitendo vingine vinavyokiuka utawala wa sheria, pamoja na kuunga mkono mijadala ya mageuzi ya kitaifa kwa uwazi na bila hofu. Demokrasia huimarishwa pale hoja zinapopewa nafasi kuliko ukimya, na pale haki zinapolindwa bila kujali tofauti za kisiasa.
@ChademaTZ2@ccm_tanzania
#FreeTunduLissu #TanganyikaMpya
VIDEO:
Mwanaharakati na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Martin Maranja Masese (MMM) amewashukia wale wote wanaobeza mwenendo wa uongozi wa sasa wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake wa Taifa Tundu Lissu
Kupitia chapisho lake aliloweka kwenye mitandao yake binafsi ya kijamii, MMM amehoji, kwamba wakati Freeman MBOWE akiwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa wale wasiokitakia mema chama hicho walikuwa wanaikashfu CHADEMA kuwa haina demokrasia ndani yake, na wengine walienda mbali zaidi na kukiita kuwa 'Chama cha MBOWE'
Hata hivyo, MMM anasema baada ya Tundu Lissu kuingia madarakani kama Mwenyekiti Mpya watu walewale wamegeuka tena na kusema bora uongozi wa MBOWE.
#BREAKING: OLEPOSE AKINUKISHA! 'WOTE TUKUTANE KORTINI KESI YA LISSU'
Mwanaharakati wa haki za kibinadamu na mwanachama wa chadema Isaya Ole pose ametoa wito kwa wanachama na wananchi kufika katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Jumatatu, Agosti 10, 2026, kuanzia saa tatu asubuhi, ili kufuatilia mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
MORE: https://t.co/TZMHkLIw6b
‼️NDULI IDD AMIN MAMA AMEPANGA KUM'NDUGAI EMANUEL NCHIMBI‼️
Mliokaribu na Emanuel Nchimbi mwambieni akae rada maana Nduli Idd Amin Mama na mwanae Abdul wanataka kumuondoa kihuni kama walivomuondoa Job Ndugai kwenye uSpika wa Bunge.
Nduli Idd Amin Mama anataka kumng’oa Nchimbi kwenye uMakam haram wa Rais kwasababu ya ile kauli ya Nchimbi ya kusema kwamba “Watanzania piganieni KATIBA MPYA maana hata Nduli Idd Amin Mama na yeye anataka KATIBA MPYA.”
Nduli analalamika kwa vibaraka wake kwamba kwanini Nchimbi amsingizie yeye kwamba anataka Katiba Mpya wakati alishawambia kwenye vikao vyao huko ndani kwamba hataki kusikia mambo ya Katiba Mpya???
Hata huko kwenye korido zao, machawa wa Nduli wanasema Nchimbi ni msaliti, anasifia Wanaharakati ambao Nduli anawaona kama Alshabaab na kwamba Nchimbi anapush agenda za wapinzani wao ili aonekane mwema wakati ndani ya Chama chao walishakubaliana kwamba hawawezi kuruhusu mchakato wa Katiba Mpya kwasababu wanahofia kupoteza madaraka.
Ndo maana hata juzi kati wakati Nduli anaongea na tule tuvyama twa kwenye briefcase alisema kwamba
“TUTAFANYA MABADILIKO KWENYE KATIBA”
Hakusema kwamba wataanzisha au kufufua mchakato wa Katiba Mpya kwasababu hana/hawana huo mpango hata ile kauli ya Ridhwani Kikwete aliyoitoa juzi kati kwamba tuwapuuze wanaodai Katiba Mpya haikuwa bahati mbaya, anajua kwamba huo ndo msimamo wa Nduli pamoja na Chama chao.
Sasa turudi kwenye issue ya Nduli kutaka KUM'NDUGAI Nchimbi, iko hivi baada ya Nchimbi kuzungumza kuhusu Katiba Mpya na mjadala kuwa mkali sana mitandaoni, Nduli Idd Amin Mama alituma baadhi ya Wastaafu wakazungumze na Nchimbi wajifanye wanamshauri ili akubali kujiuzulu na sababu waliyompa Nchimbi ni kwamba eti kwasababu kuna baadhi ya mambo hakubaliani na Nduli hivyo wao wanaona ni bora ajiuzulu, Nchimbi akawagomea.
Baada ya kugoma ndo wakaitisha kikao chao cha Halmashauri Kuu ambacho kilifanyika Zanzibar kwenye iko kikao Nchimbi alishambuliwa kama mpira wa kona na hoja za Wajumbe waliokuwa wanamshambulia walikuwa wanasema, kwanini aseme Wananchi wapiganie Katiba Mpya wakati walishakubaliana kwamba hakuna mambo ya Katiba Mpya??
Badada ya mashambulizi, mwisho wa siku Nduli akasema kesi ya Nchimbi ipelekwe huko kwenye Kamati ya Maadili, aitwe ahojiwe na achukuliwe hatua, kwa msiomfahamu Kamati ya Maadili ya CCM Mwenyekitiki wake ni Mzee Wasira 😀 ambae akiwa na Idd Amin Mama anasema Nchimbi miyeyusho, akiwa huko gizani ambako Nduli hayupo anasema Nduli ni uwezo wake kiuongozi ni mdogo sana ila hawana namna maana ndo Mwenyekitiki wao so inabidi wamnafkie tu.
Nduli na washauri wake baada kugundua kwamba huko kwenye Kamati ya Maadili mchakato wake unaweza usiwape matokeo ambayo wanataka, wameona bora watumie njia ya mkato.
Wamepanga kuwapa pesa baadhi ya Wabunge haram ili watakapo anza vikao vya Bunge vinavotarajia kuanza hivi karibuni, kila wakisimama kuchangia watakuwa wanamshabulia Nchimbi na kushinikiza ajiuzulu sababu zao zitakuwa zile zile kwamba ni msaliti na anamdharau Nduli Idd Amin kwasababu ni Mwanamke na Spika haram anajua kuhusu mchongo mzima maana kashirikishwa na wamekubaliana mjadala utaanzia Bungeni
Then Viongozi wa CCM pamoja na uvisisiemu ambao watapewa maokoto watapokea kijiti kisha wataanza rasmi kufanya press za kumshambulia Nchimbi huku wakimshinikiza ajiuzulu.
Kama asipojiuzulu, wamepanga kudraft barua na kuweka sahihi yake ili ionekane Nchimbi kajiuzulu yeye mwenyewe, kama walivomfanyia Job Ndugai kwenye uSpika.
Nduli anataka kuweka mtu ambae atakuwa anampigia makofi na kumsifia hata akijamba.
Sasa wale mnaolilia maridhiano kwamba hayo maridhiano ndo yatawapa KATIBA MPYA endeleeni kusubiria boti airport, Idd Amin Mama na Chama chake hawana mpango wa kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya ndo maana mnaona Nchimbi anashambuliwa
Watanzania wenzangu, KATIBA MPYA tutaipa kama ikifika mahali Watanzania wote bila kujali itikadi wala dini zetu, tukaamua kusimama na kupambana huku tukimtanguliza Mungu, njee ya hapo tutasubiri sana
Chadema sio tu kwamba ni kikuu cha kisiasa Tanzania.
Chadema ni imani ya Watanzania.
Asanteni Sirari kwa mapokezi ya heshima kubwa.
Endelea kuchangia chama.
Hi Watanzania, kwa sasa niko busy mnooo na jambo la msingi, very soon mtajua nilikuwa busy na kitu gani.
So kwa sasa I’m not focused kwa kudai haki huku kwenye social media, nipo busy napambana kiundani zaidi..:.:
Soon wote mtajua what was keeping me busy. And it will be great news to Tanzanians, GOD WILLING.
Zimebaki Siku 7 tu kuelekea Siku ya Vijana Duniani.
WEZESHA KUPITIA
Mixx By Yass
Namba: 0710 845 999
Jina: BAVICHA TAIFA
CRDB PLC
Namba: 0152293590500
JINA : Bavicha Taifa
Mlihongwa pesa na Madalali wa SIASA ili mumtukane Mhe. @HecheJohn, mkafanya press za kutosha, sasa hivi pesa zimeisha ndo mnarudi kwenye Chama kuomba msamaha, ifike mahali hawa wasaliti hata kama wanasamehewa ila wasipewe Uongozi.🤦🏾♀️
TAARIFA YA RATIBA YA MIKUTANO YA HADHARA YA MAKAMU MWENYEKITI BARA MH. JOHN HECHE NDANI YA MKOA WA MARA
1. Tarehe : 6/8/2026- SIRARI.
2. Tarehe: 7/8/2026 -SHIRATI
3. Tarehe: 8/8/2026- MUSOMA MJINI.
#KATIBAMPYA#FREETUNDULISSU
Askofu Dkt. Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, amewataka baadhi ya wana CCM kuacha kauli na mijadala inayoweza kushusha heshima ya viongozi wakuu wa nchi, hususan baada ya kuibuka kwa maneno mbalimbali yanayomhusu Makamu wa Rais.
Askofu Bagonza amesema siku chache kabla na baada ya vikao vya CCM vilivyofanyika Zanzibar Julai 28 na 29, 2026, baadhi ya wana CCM wamekuwa wakitoa kauli ambazo, kwa maoni yake, zinavuka mipaka ya heshima inayostahili kwa viongozi waliopo madarakani.
Katika ujumbe wake, Askofu Bagonza amesema ni hatari kwa watu kujenga dhana ya kuwepo kwa mgogoro kati ya Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu bila kuwa na uhakika wa kile kinachoendelea.
Amesema hata kama kuna hisia za kutokuelewana miongoni mwa viongozi hao, si busara kwa watu wa nje kukimbilia kutoa hukumu au kujiona wanafahamu zaidi kuliko viongozi wenyewe.
“Ukijiweka mbele halafu wao wakapatana? Utaomba hifadhi Malawi?” alihoji Askofu Bagonza katika ujumbe wake.
Amesema kauli mbalimbali zinazoelekezwa kwa Makamu wa Rais haziwezi kutafsiriwa kama zimetokana na jambo moja pekee, bali ni sehemu ya mjadala mpana unaoendelea kisiasa nchini.
Aidha, amewataka wanaoshiriki mijadala inayogusa uhusiano wa viongozi wakuu wa nchi kuwa makini na lugha wanazotumia, akisema kuna uwezekano wa mazingira ya kisiasa kubadilika na maneno yanayotolewa leo yakawa mzigo kesho.
“Usitumie neno ambalo utakosa pa kuweka uso wako baada ya kinachoitwa mgogoro kuisha,” amesema.
Askofu Bagonza amesema nafasi ya Urais na Umakamu wa Rais haziwezi kutenganishwa kwa namna ya kuleta dharau kwa upande mmoja, akisisitiza kuwa kumshambulia Makamu wa Rais ni kugusa pia taasisi ya Urais na kinyume chake.
Amesema mfumo wa mgombea mwenza ulianzishwa baada ya mjadala mkubwa wa kisiasa uliokuwa ukiongozwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, katika kipindi cha changamoto za Muungano, hivyo viongozi na wananchi wanapaswa kujifunza hekima iliyotumika wakati huo.
Katika hoja nyingine, Askofu Bagonza amesema mjadala kuhusu Katiba mpya nao umeibua makundi mawili anayodai yanazuia mchakato huo; akiwataja baadhi ya wana CCM wanaompinga mwanasiasa anayetoa matumaini ya Katiba mpya na baadhi ya wapinzani wanaotaka mchakato huo uanze kabla ya kufanyika kwa maridhiano ya kweli.
Amehoji kuwa Rais na Makamu wa Rais ni viongozi wa Watanzania wote baada ya kuingia madarakani, hivyo si mali ya chama pekee.
“Rais na Makamu ni mali ya Watanzania wote. Wakiishapishwa si mali ya CCM pekee,” amesema.
Akizungumzia nafasi ya Makamu wa Rais, Askofu Bagonza amesema kuwa Makamu ni mwanasiasa, msaidizi wa Rais na mwakilishi wake ndani na nje ya nchi, akisisitiza kuwa ni Rais pekee mwenye mamlaka ya kutathmini namna anavyosaidiwa.
Pia amewataka viongozi hao kutambua kuwa wanaongoza nchi iliyopitia majeraha mbalimbali na kwamba kipaumbele kinapaswa kuwa kulinda maslahi ya taifa kuliko maslahi binafsi ya kisiasa.
Katika suala la vijana, hususan kizazi cha Gen Z, Askofu Bagonza amesema mjadala wao haupaswi kuishia katika kuunda wizara, bali unahitaji mikakati mipana ya kuwasikiliza na kuwapa nafasi ya kushiriki katika ujenzi wa taifa.
Amesema dunia imeendelea kuweka mikakati kwa vijana na Tanzania inapaswa kujifunza kusikiliza kizazi hicho badala ya kutumia mbinu za zamani katika kushughulikia changamoto zao.