Magufuli tried to eliminate him yet he miraculously survived 16 bullets in his body. Samia and her government hates him because he talks the truth, he reveals the evils of their despotic governance. @bbcswahili@EU_Commission@usembassytz@UNHumanRights@_AfricanUnion
Leo tarehe 26 Julai 2026 mimi PETER MADELEKA natangaza rasmi KUACHANA NA SIASA ZA ACT WAZALENDO.Nafanya hivyo ili nipate MUDA WA KUTOSHA kuungana na WAPENDA HAKI wote katika KUPIGANIA HAKI na USTAWI wa nchi yetu.Tanzania yenye HAKI Inawezekana kama kila mtu ATATIMIZA WAJIBU WAKE.
@Jambotv_ Ndo unaelewa huko ndani wapo wapuuzi wachache kabisa ndani ya @ccm waopinga 99% ya matakwa ya watz na wanaokwamisha kila mapendekezo ya katiba mpya na reforms zingine.
VIDEO:
"Nikiambiwa kuna jambo tu kama Makamu wa Rais waambie Watanzania, nitasema pambaneni mpate katiba mpya, katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, katiba yenye muafaka katika taifa, katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajiskia fahari kujitambulisha mimi natoka Tanzania, katiba inayojali maisha", - Dkt. Nchimbi.
Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Julai 24, 2026 akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania @thrdcoalition unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania imepewa siku 30 na Kikundi cha Mawaziri cha Jumuiya ya Madola (CMAG) kutatua suala la kuzuiliwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa na kisheria, na kuwaachia huru watu wengine wanaoshikiliwa kwa sababu ya kutumia kile kilichotajwa na Jumuiya hiyo kama haki zao kwa amani.
Maelekezo hayo yametolewa Julai 10, 2026 katika mkutano wa pamoja wa dharura wa CMAG ulioambatana na kutolewa tamko hilo ambalo limetaka pia kufanyika kwa jukwaa la mashauriano linaloshirikisha vyama vyote vya siasa Tanzania ndani ya siku 90 ili kujadili mageuzi ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, masuala ya mahabusu na uwajibikaji, na ndani ya siku 60 irejeshe uhuru kamili wa matumizi ya mitandao ya kijamii.
CMAG pia imeamua kuendelea kuiweka Tanzania kwenye ajenda yake rasmi, ikisema pamoja na hatua chache zilizopigwa tangu maamuzi ya mkutano wake wa Desemba 5, 2025, bado yapo maeneo muhimu ambayo hayajatekelezwa. Kikundi hicho kimetaka kuondolewa kwa vikwazo vinavyohusu uhuru wa kukusanyika, kujieleza, shughuli za asasi za kiraia na vyombo vya habari, kufanyika kwa mazungumzo ya kisiasa kati ya vyama, pamoja na kuwepo kwa uwajibikaji kwa wahusika wa matukio ya vurugu na fidia kwa waathirika pale inapostahili.
Hata hivyo, Serikali ya Tanzania kupitia kauli za viongozi wake wa ngazi ya juu imekuwa ikisisitiza mara kadhaa kuwa haiwezi kuingilia mwenendo wa shauri la Tundu Lissu kwa kuwa suala hilo liko mahakamani, wamekuwa wakieleza kuwa Tanzania ni nchi huru na yenye mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake ya ndani hasa utawala wa nchi, utekelezaji wa sheria na masuala ya ndani ambayo yanaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za Tanzania, bila kushinikizwa au kuamuliwa na mataifa au taasisi za nje.
Tamko hili limejiri baada ya mkutano huo kupokea ripoti ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kuhusu ziara ya Mjumbe wake Maalum nchini Tanzania, Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera (Rais mstaafu wa Malawi) ya mwezi Aprili, 2026. Wakati wa ziara hiyo, Chakwera alikutana na Rais Samia Suluhu Hassan, viongozi wa Serikali, viongozi wa vyama vya siasa, wawakilishi wa asasi za kiraia, viongozi wa dini, Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Wakati na Baada ya Uchaguzi wa Oktoba 29 pamoja na wadau wengine.
CMAG imekubali kukutana tena kwa dharura mwezi Septemba 2026 kupokea ripoti ya maendeleo kutoka Tanzania. Katika mkutano wa Novemba 2026, CMAG itafikiria kuchukua hatua zaidi iwapo hakutakuwa na maendeleo yaliyotarajiwa.
Aidha CMAG imesema Jumuiya ya Madola iko tayari kutoa msaada wa kiufundi kwa maombi ya Tanzania na itandelea kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU), SADC, EAC, na Umoja wa Mataifa (UN).
Tanzania sio mali ya CCM na magenge yake ya kihuni. Tanzania ni watanzania na sisi ndo wenye maamuzi ya hatma ya nchi yetu @ccm_tanzania@bunge_tz@TZMsemajiMkuu
@War_Radar2 In the same manner, Russian army couldn't produce and fly drones except experts from Iran, couldn't have enough missiles and soldiers except from North Korea and China. And this any expert can confirm. You sow wind and expect breeze?
Pamoja na kuwa Tanzania ina haki ya kuwa na mahusiano ya kirafiki na nchi yoyote duniani kwa kadri inavyowezekana, kwa maoni yangu safari ya kuelekea Moscow imefanyika katika wakati ambao si muafaka kisiasa na kidiplomasia.
Katika kipindi ambacho Marekani na Umoja wa Ulaya tayari wameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa nchini Tanzania, hususan baada ya matukio ya Oktoba 2025, malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na kuendelea kushikiliwa kwa viongozi wa upinzani, jambo la mwisho ambalo Tanzania ilihitaji ni kutuma ujumbe unaoweza kutafsiriwa kama kuhamisha mwelekeo wake wa kimkakati kutoka kwa washirika wake wakuu wa maendeleo kwenda Moscow.
Tatizo si kwenda Moscow.
Tatizo ni kwenda Moscow wakati Washington na Brussels wanaanza kuhoji mwelekeo wa kisiasa wa Tanzania.
Diplomasia sio suala la hisia; ni suala la muda, mazingira na maslahi ya taifa.
Ukweli ambao hatupaswi kuuficha ni kwamba kwa sasa Russia haiwezi kuchukua nafasi ya Marekani na Umoja wa Ulaya katika maendeleo ya Tanzania.
Takwimu zinaonyesha wazi:
Marekani imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika kipindi cha 2020–2025.
Umoja wa Ulaya umechangia takribani dola bilioni 3.2.
Russia imechangia karibu sifuri katika Official Development Assistance (ODA).
Haya si maoni. Hizi ni takwimu.
Wakati mwingine katika siasa tunajidanganya kwamba washirika wanaweza kubadilishwa kwa urahisi. Historia inaonyesha sivyo.
Marekani na Umoja wa Ulaya hawatoi fedha pekee.
Wamekuwa nguzo muhimu katika:
mapambano dhidi ya UKIMWI na malaria,
chanjo na mifumo ya afya,
elimu,
maji safi,
kilimo,
uwekezaji wa sekta binafsi,
teknolojia,
mafunzo ya wataalamu,
na upatikanaji wa masoko ya kimataifa.
Pengo litakalotokana na kupungua kwa ushirikiano huo haliwezi kuzibwa kwa picha za viongozi kukutana au mikataba michache ya kisiasa.
Mataifa hayajengwi kwa alama za kidiplomasia; yanajengwa kwa maslahi halisi ya wananchi.
Swali ambalo viongozi wanapaswa kujiuliza si kama tunaweza kuwa marafiki wa Russia.
Swali ni:
Je, Russia inaweza kuchukua mzigo wa afya, elimu, uwekezaji, biashara na maendeleo ambao Marekani na Umoja wa Ulaya wameubeba kwa miongo kadhaa?
Mpaka sasa, jibu la ukweli ni hapana.
Hatari kubwa zaidi si kupoteza misaada.
Hatari kubwa ni kupoteza imani.
Mataifa yanaweza kuishi bila misaada kwa muda fulani.
Lakini ni vigumu kuishi bila imani ya wawekezaji, masoko ya kimataifa, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo.
Fedha za dunia zina tabia moja:
Hukimbilia kwenye utulivu, uwazi wa kisiasa na taasisi zinazoaminika.
Ndiyo maana nchi yenye busara haiharibu madaraja kabla haijajenga mengine.
Na hata kama imeamua kujenga daraja jipya kuelekea Moscow, ni hatari kubomoa madaraja yaliyoiunganisha na Washington na Brussels kwa zaidi ya nusu karne.
Kwa sababu katika siasa za kimataifa, si kila rafiki mpya ana uwezo wa kuchukua nafasi ya rafiki wa zamani.
Na katika wakati ambao Tanzania inahitaji uwekezaji zaidi, ajira zaidi, teknolojia zaidi na masoko zaidi, taifa linapaswa kuwa makini sana lisije likachanganya uhuru wa kidiplomasia na kujitenga kidiplomasia.
Uzalendo wa kweli si kupiga picha na mataifa makubwa; uzalendo wa kweli ni kuhakikisha maamuzi ya leo hayaleti gharama ambazo wananchi wa kawaida watazilipa kesho.
"Hakuna ukoo wa familia iliyoteuliwa na mungu kuongoza wenzake ni lazima watu waridhie kikatiba na kisheria" DR KITIMA
Haya mambo hatupaswi kuyasahau tunapojadili watu kujitawala, mwenye nia ya kutawala anatakiwa apitie kwenye mchakato huru na wa haki wa kuridhiwa na wananchi.
BREAKING: VIDEO MPYA. NEW VIDEO EVIDENCE OF THE VIOLENCE THAT TANZANIANS ENDURED DURING THE INTERNET BLACKOUT UNDER SAMIA SULUHU ORDERS.
WATANZANIA AMBAO MLIKUWA MNAOGOPA KUACHIA VIDEO, PLEASE NITUMIENI ILI DUNIA IONE ILI TUPATE MSAADE WA NJE!!!!! WhatsApp +1 424 537 3057
Nimefikiri na kutafakari kwa muda mrefu baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki, utu na dhuluma dhidi ya uhai wa binadamu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025. Siwezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya tena.
Kwa dhamira yangu binafsi, leo nimejiondoa rasmi kutoka CCM na kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za CHADEMA.
Kwa Watanzania wote, na wanachama wa CHADEMA wale walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wangu wa awali, naomba radhi kwa dhati pale nilipokuwa kinyume na matarajio yetu ya pamoja katika safari ya kutafuta haki, utu na demokrasia ya kweli.
Naam, binadamu hukosea, lakini dhamira inapozinduka ni wajibu kusimama upande unaouona kuwa wa kweli na wa haki.
Asanteni Sana.