@Northern_thugg Inawezekana ikawa Mungu hana dini wala hakuzileta yeye waliozileta walizitumia kutuibia kututawala na kutufanya watumwa,Mungu yupo Imani itakuponya dini zisikuchanganye ukachinjana na ndugu zako
Mashabiki wa Simba wamejitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo kuwapokea Wachezaji wao kutoka Afrika Kusini baada ya kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup).
Wakiwa na bendera, jezi na nyimbo za kuishangilia timu yao, Mashabiki hao wameonesha furaha na heshima kwa Simba SC ambayo imeweka historia kubwa kwa kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo barani Afrika kwa mara ya pili sasa mara mwisho ikiwa mwaka 1993.
#MillardAyoUPDATES