Mwanaume wa kweli anahitaji vitu 3 kwa Mwanamke.
1. HESHIMA.
Mwanaume anayeheshimiwa huongeza nguvu ya kuwajibika.
2. AMANI.
Mwanaume huhitaji sehemu ambayo anaweza kupumua bila vita kila siku.
3. UAMINIFU & SUPPORT.
Support ya kweli humpa mwanaume utulivu wa kupambana na dunia bila kuogopa usaliti nyuma yake.
Choose wisely.
“Kuna dunia na ulimwengu. Ya dunia, mengi yameandikwa; kayasome vitabuni. Ya ulimwengu, mengi yamehifadhiwa katika mioyo, kumbukumbu na vinywa vya wale waliofunuliwa. Utayapata kwa kukutana na kuzungumza na watu.” — Togolani Mavura
Ndugu Zangu Mimi Nalala Ila kumbukeni kua
Kuna Nyakati kwenye Maisha Ukweli hua wazi kias kwamba huhitaji Mjadala Mrefu ili kujua nini cha kufanya
Maamuzi Magumu hayahitaji vikao
Mara nyingi Watu hupoteza Muda
wakitafuta Maoni mengi
ilhali ndani yao Tayari wanajua Jibu Sahihi
Mahali utakapopata Amani, baki hapo, hata kama hakuna kiti, kaa chini tu, kwa sababu jambo muhimu kuliko mengine ni Amani.
Linda Amani yako. Chagua Watu, sehemu, na Maisha yanayokupa Utulivu wa Moyo. Maana mwisho wa siku, Amani ndiyo msingi wa Furaha ya kweli.
Kati ya Pesa na Afya, kipi hasa kinapaswa kutunzwa ili kisaidie maisha ya Uzeeni? Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi anaelezea vizuri suala hili.
Video: Mwananchi Digital
"Ukitaka kuondoa hofu kwenye maisha yako, kaa na watu wa rika, jinsia, imani, utamaduni na hali tofauti, tembea sehemu tofauti tofauti, sikiliza zaidi na soma vitabu ukianzia na vitabu vitakatifu." ~Togolani Mavura.
"Mitandao ya kijamii haiumbi tabia ya mtu, bali hufichua hulka yake. Ni kama dirisha linalosahaulika wazi na kutuwezesha kuona undani wa mtu." ~Togolani Mavura.
"Kila mtu ana mapungufu yake na vilema vyake. Kinachofanya tusione mapungufu na vilema vya watu wengine ni sababu wanao watu wanaowafanya tuwaone wamekamilika kwa kuwavumilia mapungufu yao ama kuyasitiri. Muhimu uwajue wanaokukamilisha maishani na waenzi waendelee kukusitiri."
"Kujua unachotaka ni jambo moja, kujua njia bora na wakati sahihi wa kukiendea ni jambo lingine na pia ni la muhimu zaidi. Mara nyingi katika maisha tunafeli si katika lile la kwanza bali hili la pili." ~Togolani Mavura.
Mwanaume.
Mwanamke anapofikia hatua ya kukuacha huwa ANASAHAU kumbukumbu ya ulichomfanyia.
Kwa lugha rahisi, mwanamke anaekuacha ana-DELETE chochote ulichomfanyia.
Kumpa pesa na kumtimizia kila kitu, isiwe kigezo cha wewe kuwa na EXPECTATIONS nae 100%.
Muhimu ni KUWEKEZA zaidi kwako.