#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 23
Wakili wa waleta maombi John Seka anaendelea kumdodosa Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Andrew Shaban Ntamamiro (Bwana jela)
John Seka: Moja ya sheria ni sheria ya magereza ambae umeisomea na kuibobea?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Kanuni za magereza je?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nazo ni muhimu sana. Zinatumika.
John Seka: Kwenye kanuni hizo unapaswa kutii kanuni ya 13 ya uendeshaji wa kanuni za Magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ibara ya 29(1) inasemaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Kila mtu anayo haki ya msingi ya kufaidi haki za binadamu kama zilivyofafanuliwa ibara ya 12 hadi 28 ya Katiba hii.
John Seka: Ni nani na nani wana haki ya kufaidi haki mbalimbali?
Ntamamiro (Bwana jela) : Watu wote.
John Seka: Hata wewe?
Ntamamiro (Bwana jela) : hata mimi.
John Seka: Hata Tundu Lissu:
Ntamamiro (Bwana jela) : Hata Lissu.
John Seka: Hata Kisabo?
Ntamamiro (Bwana jela): Hata Kisabo
John Seka: Hata Maduhu na Nashon
Ntamamiro (Bwana jela) : Hata Maduhu
John Seka: Nashon Je?
Ntamamiro (Bwana jela): Hata Nashon.
Watu wanacheka. Wanamuona zamwamwa sijui 😂😂😂
John Seka: Haya rudi ibara ya12 sasa kule.
John Seka: soma ibara 29(2) na useme inasemaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : kila mtu ana haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria.
John Seka: Hadi Lissu akiwa mikononi mwako Ukonga?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sahihi
John Seka: Nenda Kanuni ya 13 ya kanuni za Magereza na utuambie miaka 31 ya uzoefu wako ni lini uliifahamu kanuni hii?
Ntamamiro (Bwana jela) : Tangu nilipoanza Kazi.
John Seka: Isome kwanza.
Ntamamiro (Bwana jela) : mfungwa atapewa haki ya kuongea na wakili wake kwa faragha lakini awe anaonekana lakini sio kuwasikiliza.
John Seka: Umeielewa kweli hicho kifungu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio mfungwa atapewa nafasi ya kuongea na wakili wake na kufanyika kwa kuona lakini sio kusikiliza.
John Seka: Kuna haki ya mfungwa na kuna haki ya mshauri wa kisheria kwenye kanuni hiyo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Haki ya mfungwa kusaidiwa kupewa nafasi ya kuongea na mshauri wake wa kisheria yaani Wakili.
Ntamamiro (Bwana jela): Ndio
John Seka: haki ya pili ni ya mawakili kupata fursa ya kuongea na mfungwa kwa faragha bila ya kusikilizwa ni kutazamwa tu.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Hii haki huwa unasomewa au ni uzoefu? Hii kanuni ya 13.
Ntamamiro (Bwana jela): Sijaelewa swali.
Seka: ili uwe na ujuzi huo wa kutazama bila kusikiliza kuna chuo kinachofundisha? Au ni uzoefu wa kazi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Katika uzoefu wa kazi unasema hapa natazama na sisikilizi.
John Seka: Kwahiyo utekelezaji wa jambo hili unategemea mtu na mtu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hakuna standard zilizowekwa.
John Seka: Kwenye nyaraka zako na maelezo yako ulikuwa unasema simamia? Maana yake ulikuwa unasema simamia lakini wasisikilize.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ukubwa wa Chumba cha Ofisi yako ukoje?
Ntamamiro (Bwana jela) : wakutosha tu.
John Seka: Huwezi kukadiria?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
Jaji: Ofisi yako hujui ina ukubwa gani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wakutosha.
Jaji: Tunatosha wote humu ndani tukija ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hamuwezi kuingia.
Jaji: Bado unasema ni ukubwa wa kutosha?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio
Jaji: Haya jibu swali sasa.
Anasimama Nalindwa Sect. 93 ya Prison Act inasema ramani ya gereza isitolewe. Ukubwa wa hizo ofisi ni hatari.
Jaji Mruma: Hakuna ramani ya gereza wala kifungu hakisemi hivyo. Shahidi jibu swali tunataka sana kujua ukubwa wa ofisi yako ni jambo muhimu sana.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni ofisi iko umbali kutoka hapa nilipo hadi hapo kwako.
John Seka: Sasa ofisi yako ya kaimu wako Recha ni ofisi ya nani kubwa?
Ntamamiro (Bwana jela): Yakwangu ndio kubwa.
Part 24 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Kesi ya uongo ya mgogoro fake wa mali, ni kesi ya Msajili wa vyama..
Marehemu mama Komu alituelezea namna ambavyo Sisty Nyahoza, Msajili msaidizi akiwa na mtu anaitwa Salehe Bohora, walivyomfuata nyumbani kwake na kuomba aweke jina kwenye kesi..
Marehemu Mama Komu alituambia hata malipo ya mawakili yalilipwa na Salehe Bohora na bwana Sisty, kwa mujibu wa mama Komu huyu bwana Salehe alitumwa na Rais.
Mtakumbuka pia kuna mtu alijiita Mwenyekiti wa Chadema Mwanga.. huyu nae alikua analipiwa mpaka mahali pakukaa na ofisi ya msajili, kupitia ofisi hiyo hiyo ya msajili walidai kutotambua uongozi halali wa Chama, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na wajumbe wa kamati kuu ya Chama.
Hii kesi ilifunguliwa siku hiyo hiyo ambayo Mwenyekiti wetu alikamatwa na kupewa kesi ya uhaini.
Kesi hii ilipangwa kwa Jaji mwingine awali lakini katika mazingira tata ikapelekwa kwa jaji Mwanga.
Jaji Mwanga tangu awali alionekna wazi kutofuata sheria, kuendesha Kesi kibabe na kudharau kila hoja iliyotaka upande wetu… alikua na maelekezo ya wazi na alionesha upendeleo uliovuka mipaka..
Kupitia kesi hii shughuli za Chama zilizuiliwa kinyume cha sheria kwa siku 309, Mpaka mahakama ya rufani ilipofuta zuio fake..
Kupitia Hilo zuio watu wetu walipigwa mara nyingi na polisi kila walipojaribu kufanya shughuli za chama.
Tutakumbuka siku ya wanawake duniani namna wanawake wa Bawacha walivyopigwa mpaka kanisani kwasababu ya zuio hili haramu..
Mali za Chama zimeharibika, Mimi pamoja na Katibu mkuu tulifunguliwa kesi ya contempt of the court. Kutokana na Amri hizi hizi.
Jaji Mwanga alipuuza hukumu ya mahakama ya rufani ambayo ilikua inamlazimisha kutokifungia Chama chetu..
Nani atalipia maumivu, usumbufu, matatizo ya makusudi, nani atalipia hasara zisizolipika za kuzuia chama mda wote huu kufanya kazi zake..
Tunafurahia leo, lakini Fikiria damage zote hizi hazikutakiwa kuwepo, zilifanywa kwa makusudi kwa manufaa ya Samia na Ccm.
Bado msajili anatufuata fuata na kutuandikia barua baaada ha maumivu yote haya aliyotusababishia..
Kama ilivyo kesi ya uongo ya kumtesa Mwenyekiti wetu ndivyo zilivyo zote hizi ni kwa manufaa ya Samia wala sio Nchi..
Tuacheni tufanye wajibu wetu wa kisiasa. Hatutapiga magoti wala kununuliwa.
Leo naomba niweke MASLAHI yangu wazi. Kuhusu tarehe 29 OKTOBA 2025, Mimi NAIAMINI CCM na VIONGOZI WAKE WOTE kwa KAULI na MATENDO yao. Hata mtu ANIWEKEE BASTOLA KICHWANI, Mimi SIWEZI KUMUAMINI Jaji CHANDE. Hongera sana DR. MIGIRO kwa KUKAZIA UKWELI hapo 👇
Kwa umoja huu Wauwaji waliofanya mauwaji makuu ya 29 okt 2025 haponi hata mmoja. Haki haiwezi kupotea hata ipite miaka mingapi lazima waliouwa maelfu ya Raia Wema wawajibishwe.
“KUINGIA BARABARANI” siyo kosa ambalo POLISI wamepewa MAMLAKA KISHERIA ya KUUWA WATU. Kazi ya POLISI ni KUKAMATA watu ambao WANAVUNJA SHERIA na SIYO KUUWA WATU. Kimsingi, POLISI AKIUWA WATU kinyume cha SHERIA, anakuwa ni MHALIFU TU kama WAHALIFU WENGINE.🥲
Sometimes 1996,
Rashid Salehe anahamia jijini Dar Es Salaam akitokea kisiwani Pemba.
Rashidi akafungua duka la vipuri vya magari mtaa wa Sikukuu Kariakoo
Duka liliitwa SERA AUTO PARTS
Miaka miwili baadae Rashid akageuka kipusa akisakwa na maafisa wa TRA
Kila nikitazama hizi video za Oktoba 29, huwa najiuliza hawa Polisi ni binadamu kama sisi?
Unawezaje kumfanyia binadamu mwenzako Ukatili wa kiwango hiki?
Kamwe hatuwezi kusahau huu Ukatili wa Nduli Idd Amin Mama pamoja na washirika wake maana pamoja na mateso yote haya bado wakauwa Watanganyika wenzetu zaidi ya elfu kumi.
Tundu Lissu ambaye yupo ndani ya kuta za gereza Ukonga asingeweza kwa njia yoyote ile kumtafuta Dr. Chakwera
Kwa hiyo hapa hoja ya nani alimtafuta mwenzake it’s obvious ni Chakwera ndiye aliyemtafuta Lissu ama kwa maelekezo, au utashi binafsi.
Kauli ya Lissu “Nipo tayari kwa mazungumzo nikiwa huru”
Kwa wasioelewa hii ni lugha yangu kisheria kuhusu makubaliano.
Makubaliano yanayotambulika kuwa halali kisheria ni yale yanayofanyika under FREE and genuine consent. Neno FREE hapo linasimama likimaanisha FREE from COHESION or UNDUE INFLUENCE
Lissu anaamaanisha kuwa, kwa yeyote anayetaka kuzungumza na yeye kuhusu lolote, asifanye hivyo wakati Lissu kwa kutumia ukosefu wa Uhuru wa Lissu kama UNDUE INFLUENCE kuchagiza maamuzi yake.
Kwa hiyo kwa ambao hamjaelewa, Lissu bado amekaza kutuuza kwa mazungumzo yenye ushawishi wa kumpa Uhuru.
Lissu anataka UHURU KWANZA ndipo umpelekee hoja mezani aamue kukubali au kutokubali akiwa HURU.
Lissu hajataka akatokee Ikulu.
Anataka atokee kwenye malango ya Ukonga. Sio kwa huruma, bali on merit either kwa serikali kufuta kesi yake yenyewe ambayo mpaka sasa wameipakisha basi kwa Pilato bila sababu, au hukumu ya NOT GUILTY.
Nimeona mnajimu mmoja wa mizimu anatafsiri tofauti ikabidi niweke sawa.
Yours,
The Hoofman
Hii inaitwa Red Herring , mkakati wa kuingiza hoja ya pembeni ili watu waache mada kuu na jambo la msingi katika jamii. Wakati mwingine huitwa pia manufacturing consent , kutengeneza jambo kwa umma kwa njia ya udhibiti wa taarifa muhimu.
Kwa lugha rahisi, ni mkakati wa kuhamisha umakini wa watu kutoka kwenye suala nyeti kwenda kwenye jambo lingine (mara nyingi la hisia, burudani au mgogoro) ili kupunguza shinikizo, uchunguzi na mjadala.