By sea, road and rail - our Second Life Container is following the DP World Tour in its mission to grow the game of golf. With our European multi-modal capabilities helping it on its way.
#DPWorldTour#SmartLogisticsToATee
Maelfu ya safari za Ndege zimechelewa na matukio ya michezo kuahirishwa kwenye pwani ya Mashariki nchini Marekani baada ya moshi uliotokana na moto wa mwituni ulioanzia nchini Canada kuendelea kusambaa na kuifunika miji kwa moshi wa njano na kahawia unaotoa harufu ifananayo na mbao zinazoungua.
Maafisa nchini Canada wamesema huu umekuwa moto wa mwituni mkubwa kuwahi kutokea na watalaamu wamesema moto huo unaweza ukaendelea kwa wiki kadhaa na moshi wake utatapakaa kulingana na upepo.
Moto huo umeunguza takribani ekari milioni 9.4 nchini Canada na kulazimu takribani watu 120,000 kukimbia makazi yao kwa sababu za kiusalama.
Msimu wa moto wa mwituni umeanza mapema kwenye ardhi iliyo kavu kuliko kawaida na kusambaa haraka huku moshi wake ukimwagika kuelekea pwani ya Mashariki mwa Marekani pamoja na Magharibi ya kati.
Jijini Manhattan, maduka yameuza visafisha hewa pamoja na barakoa zote, na idadi ya watu wanaotembea wakiwa wamevaa barakoa ikikaribia kulingana na kipindi cha Uviko19.
Maafisa wa afya wamewaonya watu walioko kwenye maeneo yaliyoathirika na moshi huo kuwa kukaa sana maeneo ya nje kunaweza kuwaletea matatizo ya kupumua.
#KitengeUpdates
Serikali ya Dubai, Viwanja vya Ndege na mashirika ya Ndege ya ndani yapo kwenye majadiliano ya namna ya kuendeleza mpango wa kupanua Uwanja wa Ndege wa Al- Makhtoum kuwa mkubwa kuliko yote duniani.
Mradi huo ujulikanao kama Dubai World Central (DWC) ulizinduliwa mwaka 2014 lakini mipango na majadiliano yalisimama kwa muda kutokana na sababu mbalimbali likiwemo janga la corona.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al-Makhtoum unatarajia kuwa mkubwa kwa mara nne kuliko viwanja vya Los Angeles ( LAX) na New York ( JFK) vikiunganishwa.
Ujenzi huo unatarajia kugharimu dola za Kimarekani Bilioni 33 na kukamilika mwaka 2050, vilevile utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 255 milioni kwa mwaka.
Uwanja huo una ekari 35,000 tofauti na Uwanja wa Kimataifa wa jijini Los Angeles wenye ekari 3500 na JFK wenye ukubwa wa ekari 4930.
Awamu ya kwanza ya ujenzi huo inatarajia kumalizika kufikia mwaka 2030, ambapo tayari uwanja huo utakuwa na sehemu ya kifahari ya kuchezea gofu, kituo cha biashara na maonyesho pamoja, eneo la makazi na hoteli.
#KitengeUpdates
PUUZENI UPOTOSHAJI UNAOSAMBAZWA KUWA BANDARI YA DAR ES SALAAM IMEUZWA.
Ni hivi;
1. Kilichotolewa ni tangazo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka maoni ya wadau kuhusu azimio la Bunge la kuridhia mapendekezo ya Serikali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendelezaji wa kiuchumi na kijamii unaolenga uendeshaji na uboreshaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Na ni ushirikiano wa miezi 12.
NA SIO KUIPATIA KAMPUNI YA DP WORLD (Dubai World) BANDARI YA DAR ES SALAAM KWA MIAKA 100, AMA KUUZWA KWA BANDARI KWA MIAKA 100 KAMA WAPOTOSHAJI WANAVYODAI.
Wapuuzeni, Serikali ipo makini kulinda maslahi ya nchi na chochote kitakachofanyika, kitafanyika kwa uwazi na mtajulishwa.
@ExMayorUbungo Uwekezaji wenye tija unaruhusiwa Serikali haiwezi pekee yake kushindana bandari ni competitive part. Kama unatatizo na hilo panda dau tukupe wewe mkataba, nothing personal i just saying.
Mnamo Juni 5, 2023, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mwaliko wa Wadau wote kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge la mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023.
Kufuatia Taarifa hiyo kwa Umma iliyotolewa kupitia tovuti ya Bunge, kumekuwa na upotoshaji katika mitandao ya kijamii kwamba "Serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya uendeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka mia moja (100)".
Kufuatia kusambaa kwa taarifa hizo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawajulisha Wateja, Wadau wa Kitaifa na Kimataifa na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizo sio sahihi, ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu ya kukwamisha mipango thabiti ya Nchi katika kuongeza ufanisi wa Sekta ya Bandari Nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.
Taarifa sahihi ni kuwa, Azimio la Bunge linahusu Mkataba ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia na Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi kumi na mbili (12) kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliana na Serikali ya Dubai kuhusu maeneo ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika uboreshaji na uendelezaji wa Sekta ya Bandari Nchini Tanzania.
Ushirikiano wa Dubai na Tanzania una lengo la kuongeza ufanisi wa huduma za Bandari Nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia maeneo ya uwekezai katika mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka Bandari Tanzania kwenda Nchi za jiraní ambazo zinatumia Bandari zetu.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawaomba Wateja, Wadau na Umma kutambua kwamba, jitihada zote na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuvutia uwekezaji Nchini hususan kwenye maeneo ya Banadari, zinalenga kumaliza changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli, mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika Bandari zetu.
#KitengeUpdates