VIDEO:
Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku Musukuma, amehamishia dhoruba ya mjadala wa Muungano ndani ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimwomba moja kwa moja Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, kuchukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya mawaziri wake wanaotoa kauli za kibaguzi, akionya kuwa dharau hizo zikitafsiriwa kama msimamo wa serikali zitavunja misingi ya nchi.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027 leo Jumanne, Juni 16, 2026, Musukuma amesema kuwa tangu shuleni waliaminishwa kuwa Muungano uliundwa kwa kuchanganya udongo, lakini kwa sasa vizazi vimeenda mbele zaidi kwa "kuchanganya damu," hivyo siasa za kubagua watu wa Bara hazikubaliki.
Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) amewaalika wabunge wa Zanzibar kutazama maslahi mapana ya nchi badala ya kuendekeza mipaka ya kisekta. Musukuma amesisitiza kuwa kauli inayotolewa na waziri haiwezi kuchukuliwa kama maoni binafsi ya mtaani, bali inabeba taswira ya serikali nzima.
“Mara Sangala mara Sato mara Kambale anayezungumza ni waziri, niwaombe sana sisi hatujui Mzanzibari tunajua ndugu yetu Mtanzania tu, leo hii mheshimiwa mwenyekiti ukija Zanzibar ukija Geita robo tatu ya wachimbaji madini ni Wazanzibari, tunawatibu tunawalisha Sangala na wanakula Sato. Sisi tunatamani na wao kama tumepeleka sato zikaboreshwe kule”, ameeleza Musukuma.
Mjadala huu bungeni umeamshwa kufuatia kauli zilizotolewa hivi karibuni ndani ya Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar na viongozi waandamizi wa SMZ, ambao ni Kaimu Waziri wa Afya, Saada Mkuya Salum, na Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji, Hassan Khamis Hafidh. Viongozi hao walikaririwa wakitoa kauli zilizotafsiriwa na wadau wengi wa siasa kama za kibaguzi, kufuatia msimamo wao wa kuzuia fursa za ajira na kulalamikia utoaji wa huduma za matibabu kwa "wageni".
Social Test: Part 71 - Bibi alinipa tu kwa upendo lakini kwa namna ambavyo alipokea hela niliyompa na jinsi alivyomwaga machozi, nikahisi maisha anayoishi hayako sawa, ikabidi nimtembele anapoishi, kabla ya ku share na ninyi hii video.
_
Kwanza bibi yetu anaumwa na hasikii vizuri, hastahili kuwa barabarani, lakini changamoto za maisha zinamfanya auze ndizi tena kwa kukopa, yani anauza ndio anapeleka hela mahali alipochukua, alikuwa ana watoto nane (8) amezika saba (7), huyo mmoja hana uwezo wa kumtunza, Bibi analala chini, hana godoro wala kitanda, analala kwenye mkeka, nyumba yake haina umeme, wameisha fanya wiring ila hela ya kulipia Tanesco ili wamuwekee umeme hana.
_
Bibi anachotamani ni kupata umeme, mtaji kidogo wa kuuza maharagwe hapo nyumbani kwake ili asitembee, vitu vyote havizidi million moja na nusu (1,500,000) ila tukipata hiyo, tunaenda kumrudishia bibi tabasamu na tumaini na tunakuwa tumemkopesha Mungu, kama umeguswa tutumie sadaka yako yoyote kwa ajili ya bibi yetu.
_
Number za kutuma Sadaka kwa ajili ya Bibi yetu.
Mpesa Lipa Namba: #58240194
Mpesa: #0748618888
Airtel Money: #0695152598
CRDB Bank: #0133000PY6X00
Name: Mafuru Foundation.
_
Mungu awabariki sana. 🙏🏽