"Ni rahisi kudhani matatizo aliyonayo mtu mwenye uwezo zaidi yako ni madogo kuliko tatizo lako kubwa. Uyaonayo madogo kwake yaweza kuwa ndio makubwa kwake. Ukimlilia shida na akakuambia hawezi kukusaidia, usimkasirikie." ~Togolani Mavura.
"Usikwepe hatua katika ukuaji wako! Katika kila hatua, stadi unazojifunza, watu utakaokutana nao, hadhira utakayotengeneza, ujuzi utakaoupata katika eneo lako na matatizo utakayokumbana nayo vyote kwa pamoja vina nafasi ya kuamua hatma ya mafanikio yako." ~Togolani Mavura.
"Kila mtu, akichukua njia sahihi, akajiwekea malengo sahihi, na akajiwekea nidhamu ya kuyafanyia kazi na akafanya ibada anayo nafasi ya kufanikiwa kwa namna yake na wakati wake." ~Togolani Mavura.
"Duniani kuna viumbe-watu. Machoni ni nadhifu, mioyoni ni dhaifu, upenuni ni watu ila kizani ni mwitu, sura zao ng'avu ila ndimi zao sumu." ~Togolani Mavura.
SAFARI YA KING DIDIER DROGBA.
🧵
Wakati Anaenda Port Bouet Airport
Pale Abidjan Mwaka 1982 Alikuwa na Miaka 5 Tu, wazazi wake Ilibidi Waandike Bango "Didier Drogba Meet Michael Goba In FRANCE"
ilikuwa ni Safari Ya Matumani kwa Kijana alietoka katika Familia Ya Hali Duni Kwenda
Ripoti ya Kamati Kutathmini Ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje imeshauri jina jipya la Wizara liwe Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa ili kuakisi nia ya Serikali kutumia Diplomasia ya Uchumi katika kujenga Ushirikiano wa Kimataifa kwa kuwa jina la Mambo ya Nje haliakisi vizuri majukumu ya Wizara
Imeshauri pia Wizara ihamishwe na iwe chini ya Ofisi ya Rais katika hatua ya mpito pia iundwe Wizara kamili itakayoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki kutokana na ongezeko la Nchi za Jumuia, kukua kwa Uchumi kwa Nchi Wanachama na kuenzi heshima ya #Tanzania kuwa Makao Makuu ya Jumuia
Soma https://t.co/K7Tr700MvU
#Diplomacy #Governance #JamiiForums
@MarekaMalili Ndo maana mwnanetu johnsena kalge alikataaaga ujinga wa kuajiliwa private akaamua anunue beg na pefume. 10 tu na akas tro na kupiga kowi kiatu chake pia akanunua chepe tusimjue kitaa bas jama akavuta. Mguu kw mguu mtaa kw mtaaa siriaz. Saa iz ana nyumba kali mbez kw pefume2
Sema hizi sekta binafsi 🙌🙌
Unaona watu wanaenda kazini kila siku, wanavaa vizuri, wanapendeza na nyuso za kusmile, kumbe mtu 6 months hajapata salary 🙌.
"Kama ilivyo kwa mikosi, baraka nazo huja kwa msururu. Kama ambavyo tunaufurahia na kuuvumilia msururu wa baraka hadi mwisho, tunapaswa kuvumilia na kuupokea msururu wa mikosi hadi ufike mwisho." ~Togolani Mavura.