Kheri ya Miaka 64 ya Uhuru wa nchi yetu.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hatua hii kubwa. Tunapoadhimisha siku hii muhimu, tukumbushane umuhimu wa kuendelea kulinda tunu za Taifa letu za amani, umoja na mshikamano. Tunu hizi ndizo msingi wa mafanikio ya safari yetu ambayo ni mfano wa kipekee Afrika na dunia kwa ujumla.
Matunda ya Uhuru wetu yanaendelea kudhihirika katika uwezo wetu wa kuamua, kupanga na kutekeleza mipango yenye manufaa kwa wananchi na yenye kulinda maslahi ya Taifa letu. Haya ndiyo matunda ambayo waasisi wa Taifa letu waliyapigania na ambayo daima tutayalinda.
Tuufurahie, tujivunie, tuulinde na tuuthamini Uhuru wetu.
Mungu Ibariki Tanzania.
LIVE: After eight months on the @Space_Station, @JonnyKimUSA is getting ready to return to Earth. Join us as he gives his farewell remarks and climbs into the spacecraft to head home. Hatch closure is scheduled for 5:15pm ET (2215 UTC). https://t.co/zUnml6i8MR
Leo imekuwa siku ya kihistoria kwa nchi yetu ambapo nimezindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la Mwaka 2024). Hatua hii ni utekelezaji wa maelekezo niliyotoa bungeni Aprili 2021, ambapo maboresho haya yamelenga kuiwezesha nchi yetu kuendana na mabadiliko makubwa yaliyotokea kwa miongo miwili ndani na nje ya nchi.
Ninawapongeza wote mlioshiriki kuandaa sera hii, hasa wananchi mliotoa maoni, kwani mmeshiriki katika kujenga hatma ya nchi yenu na mmeweka alama isiyofutika.
Aidha, nimeielekeza Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukuwa hatua za haraka, ikiwemo kutoa ufafanuzi, pindi kauli au matamko yanapotolewa kuhusu nchi yetu ili kudhibiti upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu.
Nchi yetu itaendelea kubaki salama, yenye amani, umoja na utulivu, na hakuna mtu yeyote atakayetuondolea nguzo hizi muhimu.
Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika Nusu Fainali.