TAHADHARI KWA WAAGIZAJI WA MAGARI (USED VEHICLES) KUTOKA UINGEREZA
Ubalozi umepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi waliotuma fedha nchini Uingereza kwa ajili ya kununua magari, lakini hawajayapokea kwa zaidi ya miezi sita, hali iliyosababisha hasara na usumbufu mkubwa.
Tunatoa rai kwa wote wanaokusudia kununua magari yaliyotumika kutoka Uingereza kuzingatia tahadhari zifuatazo:
• Hakikisha kampuni unayonunua nayo imesajiliwa na ipo hai (active) nchini Uingereza. Unaweza kufanya uhakiki kwa kupitia tovuti ya Serikali: https://t.co/G8QpwTkm0i
• Ingia mkataba rasmi wa manunuzi kabla ya kufanya malipo.
• Tumia Letter of Credit (LoC) badala ya kutuma fedha moja kwa moja (TT), hasa kwa malipo makubwa.
• Hakiki historia ya gari kupitia: https://t.co/zQko1lo7rY
• Fanya ukaguzi wa gari kabla ya kusafirishwa (pre-shipment inspection).
Kuchukua hatua hizi ni njia bora ya kujilinda dhidi ya udanganyifu na hasara zisizo za lazima.
Ubalozi unasisitiza umakini na tahadhari katika manunuzi ya kimataifa.
Kuuza akiba ya dhahabu, ni ushauri wa nani? MADURO?
Nataka kuamini ni akili na ushauri wa MADURO kuuza akiba ya dhahabu (gold reserves) ili kumalizia ujenzi. Kwani zaidi ya tozo na kodi ya bia ana mawazo gani mengine zaidi ya kuuza last option of survival?
Mwanzoni mwa mwaka 2010, Benki Kuu za nchi nyingi Duniani ziliacha kuuza dhahabu na kugeuka kuwa wanunuzi wakubwa wa dhahabu. Leo, USA wanayo hifadhi ya dhahabu thamani ya $1.44 Trilioni
Oktoba 2023, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilianza kununua dhahabu kwa ajili ya akiba. Manunuzi ya dhahabu yalilenga kuimarisha nguvu ya shilingi katikati ya changamoto za kidunia. Ghafla mnauza tena?
Wakati nchi nyingine timamu Duniani zinanahifadhi dhahabu kama kinga dhidi ya kuyumba kwa hali ya uchumi wa dunia, mfumuko wa bei za bidhaa, na hatari ya sarafu, sisi tumeamua kuuza akiba ya dhahabu?
Nchi timamu Duniani zinahifadhi akiba ya dhahabu zao kwa sababu mbalimbali ikiwa pamoja na; Safe Haven Asset: Reserve Diversification; Hedging Inflation; Liquidity and Creditworthiness; Confidence Booster;
Lakini siyo kuuza akiba ya dhahabu ili kukamilisha miundombinu iliyokwama. Kwani kuna geopolitical conflict? Kuna njaa kuu hadi mnaona suluhisho ni kuuza akiba ya dhahabu? Marafiki zenu wamekata mirija?
Sababu ya Serikali ya MaCCM kuamua kuuza akiba ya dhahabu ni kukamilisha miradi inayoendelea? Tukitumia ubongo vizuri, tunakumbuka miradi mikubwa inayoendelea pesa ilitengwa na pesa nyingine ni mikopo
Nchi zilizo na akiba kubwa ya dhahabu (highest gold reserves) zinakuwa na uwezo mzuri wa kukabiliana na shinikizo la kiuchumi; zinazo mali zinazoongezeka thamani nyakati za misukosuko ya uchumi.
Miundombinu ni muhimu, ndiyo, lakini kuuza akiba ya dhahabu ni suluhisho la muda mfupi. Tafuteni namna nyingine ya kukamilisha miradi yenu iliyokwama. Halafu, mikopo kwa ajili ya hiyo miradi ilikwenda wapi?
Mvutano wa kisiasa unaoongezeka Duniani, migogoro ya kibiashara, na mabadiliko katika sera za misaada ya nje ya Marekani na Ulaya vitaongeza hali ya wasiwasi wa kiuchumi Duniani., akiba ya kuwasaidia ipo wapi?
Dhahabu ikishaondoka, imeondoka. Miundombinu inaweza kusubiri kama mlivyoisubirisha miaka 64. Ongezeni thamani kupitia uchimbaji, imarisheni ukusanyaji wa rasilimali, siyo kuuza akiba ya dhahabu
Watasha wanajua wakishapata hii rasilimali muhimu watakuja kuuza zaidi wakitengeneza bidhaa zake. MaCCM hampo vitani mnauza akiba ya dhahabu kwa ajili ya kukamilisha miundombinu. Akiba ni tani 6.
Wizara ya Madini Tanzania ilisema hadi kufikia Julai 2025, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilikuwa na hifadhi ya dhahabu tani 6.84 yenye thamani ya $682 milioni tangu ilipoanza kununua na kuhifadhi Oktoba 2023.
Akiba ya dhahabu ambayo Tanzania inataka kuuza ina thamani ya $13.7 bilioni. Ni kiwango sawa na ambacho nchi ya Ukraine iliuza akiba yake ya dhahabu mwaka 2022 ili kustahimili kuwepo vitani na Russia.
Ukraine, 2022 waliuza akiba ya dhahabu yenye thamani ya $12 billion ili kununua bidhaa. Q3 na Q4 2025 akiba yao ya dhahabu ni tani 27.37 ambayo thamani yake ni $3.664 billion. Hawa wapo vitani. Ninyi mpo vitani?
Kwa mwaka 2025 nchi iliyoongoza katika kununua dhahabu Duniani ilikuwa ni Poland, ambapo imenunua tani 67. Poland ni moja ya nchi ambayo iko katika mvutano mkubwa wa kidiplomasia na Russia.
Septemba 10, 2025, drone 19 za Russia ziliingia anga la Poland, 3 zikiangushwa. Russia imesisitiza haikua na nia ya kuivamia Poland. Poland imeendelea kulipinga, na kusisitiza kwamba Russia ina njama dhidi yake.
Hii ni sababu ya Benki Kuu ya Poland kuamua kuimarisha akiba ya dhahabu ambayo ni nyingi kuliko European Central Bank. Akiba yao ni tani 770 na hii inaifanya kuwa nchi ya 10 kwa akiba ya dhahabu Duniani
Tanzania hatupo vitani. Hakuna geopolitical crisis. Hakuna janga la njaa isipokuwa akiba yake ya dhahabu inauzwa ili kuendeleza miundombinu. Miundombinu gani? SGR? BRT? Fedha za mikopo zimekwenda wapi?
Tanzania ni muuzaji mkubwa namba nne wa dhahabu Afrika ambaye hayupo katika orodha ya nchi 10 za Afrika ambazo zinamiliki akiba kubwa ya dhahabu, sasa tumeamua kuuza hata hiyo akiba ya dhahabu iliyosalia
NB; Tanzania tupo katika orodha ya Africa’s largest exporter of gold halafu sehemu za watoto kuhifadhi mavi tunajengewa na mabeberu. MaCCM mnatakiwa kupelekwa motoni moja kwa moja, bila majadiliano.
Kauli ya BoT inachochea maswali zaidi kuliko majibu. Dhahabu “imezidi kiwango” si tatizo, kwani dunia nzima inaongeza hifadhi yake kama ngao dhidi ya hatari za dola, siasa za kimataifa, na mishtuko ya kifedha. Dhahabu si asset ni akiba ya taifa yenye uthabiti. Kuuza kwa sababu thamani imepanda ni sawa na kuuza insurance kabla hatari haijatokea. Central banks makini huongeza dhahabu inapopanda bei, si kuuza
Fedha zinazotokana na mauzo ya dhahabu kwenda masoko ya fedha ya kimataifa ni hatari. Masoko hayo yana currency risk, interest rate risk, na counterparty risk, wakati dhahabu haina issuer risk. Hivyo, central banks hazifukuzi yield, bali zinalinda uthabiti wa taifa. Tatizo si mauzo yenyewe, bali mindset, kuangalia dhahabu kama trading asset badala ya ngao ya taifa. Uchumi wa kweli ni kwa watu wanaoelewa mishtuko ya dunia na dhahabu ni kinga, si mzigo.
TOP 10 AFRIKA – UZALISHAJI WA DHAHABU (Migodini)
Nchi zinazochimba dhahabu nyingi kwa mwaka:
Ghana, Mali, Afrika Kusini, Burkina Faso, Sudan, Guinea, Tanzania, Côte d’Ivoire, Zimbabwe, DR Congo.
➡️ Hizi ni nchi zinazochimba dhahabu nyingi ardhini.
TOP 10 AFRIKA – AKIBA YA DHAHABU BENKI KUU (2025)
🇩🇿 Algeria ~173.6t | 🇱🇾 Libya ~146.7t | 🇪🇬 Misri ~126–128t | 🇿🇦 Afrika Kusini ~125t | 🇬🇭 Ghana ~31t | 🇲🇦 Morocco ~22.1t | 🇳🇬 Nigeria ~21.3–21.5t | 🇲🇺 Mauritius ~12.4t | 🇹🇳 Tunisia ~6.8t
JE BOT INGEHIFADHI DHAHABU NYINGI INGETOKEA NINI?
Mfano BOT ikihifadhi tani 30–50:
✅ Shilingi ingekuwa imara zaidi
✅ Kushuka kwa thamani kungepungua
✅ Imani ya wawekezaji ingeongezeka
✅ Uchumi ungekuwa na “backup” ya kweli
✅ Mikopo ya kimataifa kwa masharti nafuu
✅ Tanzania ingeonekana kifedha kama Ghana/Algeria
✅ Hatari ya misukosuko ya uchumi inapungua
Sio dhahabu unayochimba, ni ile unayohifadhi.
Nchi inauzwa:
1. Bandari DP World
2. KIA
3.Tazara wachina
Sasa reserve ya dhahabu.
Unapoanza kukua , unaanza kuelewa baba yako alikuwa tu mwanamume pia anayejaribu kadiri ya maarifa aliyokuwa nayo kupambana na maisha. Msamahe , kwani pia alikuwa akiishi maisha kwa mara ya kwanza.