Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu amependekezwa rasmi kuwania Tuzo ya Sakharov ya Mwaka 2026, ambayo ndiyo heshima ya juu zaidi inayotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa watetezi wa haki za binadamu na uhuru wa kufikiri duniani.
Uteuzi huo wa kihistoria umetangazwa rasmi leo, Septemba 15, 2026, na kundi kubwa na lenye nguvu zaidi la kisiasa ndani ya Bunge la Umoja wa Ulaya la The EPP Group (European People's Party).
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na chama hicho kupitia kurasa zake za mawasiliano, EPP ilieleza kuwa uamuzi wa kumteua Lissu umetokana na mchango wake usio mithilika katika kupigania haki, utawala wa sheria, na mifumo ya vyama vingi vya siasa nchini Tanzania, huku wakimwita "kielelezo cha ujasiri."
Waliongeza kuwa Lissu amekuwa sauti imara ya demokrasia na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania, akisukumwa na dhamira ya kuona nchi yake inafuata misingi ya kidemokrasia hata pale maisha yake yalipowekwa hatarini
Tuzo hii ya Sakharov iliyoanzishwa mwaka 1988 kwa heshima ya mwanasayansi na mpinzani wa Sovieti Andrei Sakharov, hutolewa kila mwaka kwa watu au makundi yaliyojitolea kulinda haki za binadamu na uhuru wa kimsingi. Tuzo hii ina thamani ya kifedha ya Euro 50,000 (zaidi ya Shilingi milioni 150 za Kitanzania) na hutolewa rasmi mwezi Desemba katika ukumbi wa Bunge la Ulaya uliopo Strasbourg, Ufaransa.
Tangu kuanzishwa kwake, imekuwa ikitolewa kwa viongozi na wanaharakati walioonesha ujasiri wa kipekee duniani, ambapo hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini ndiye alikuwa mshindi wa kwanza kabisa wa tuzo hii kabla hata hajawa Rais.
Baada ya uteuzi huu wa Septemba 15 uliofanywa na EPP Group, mchakato unaingia hatua ya mchujo wa makundi mbalimbali ya kisiasa ndani ya bunge hilo. Kamati ya Mambo ya Nje na Kamati ya Maendeleo ya Bunge la Ulaya zitakaa mwezi Oktoba kupiga kura na kupata wateule watatu wa mwisho (top 3 finalists).
Baada ya hapo, Rais wa Bunge la Ulaya na wakuu wa vikundi vyote vya kisiasa watakutana kumtangaza mshindi mkuu wa mwaka 2026, ambaye atakabidhiwa rasmi tuzo hiyo mwishoni mwa mwaka.
Ndani ya masaa 48 tumefikia 10% ya 340M.
Hiki chama ni dude kubwa sana. Licha ya makelele yote wananchi wameamua kufanikisha hili na hakuna wa kuturudisha nyuma.
Hakikisha unarepost ujumbe huu unafikia maelfu ya Watanzania watimize haki yao ya kikatiba kuchangia MABDILIKO YA KWELI KWENYE TAIFA LETU.
#FreeTunduLissu
#KatibaMpya
REPOST 500
"Chadema Kanda ya Kati ina taarifa na ushahidi wa awali unaojumuisha vielelezo vya picha, Video na mawasiliano ambayo ni sambamba na miamala iliyotumwa kutoka kwa hao wanachama wa Chama cha Kikaragosi kwenda kwa wanachama wa Chadema. Wapo wanachadema wengi ambao wamepokea fedha na ushahidi huo tutauweka hewani lakini kwasasa tumekabidhi vielelezo kwa mwanasheria Mkuu wa Chama ili waweze kupitia kwaajili ya hatua nyingine za kisheria. Tuna mawasiliano ya namba zinazotumima kuwapigia Viongozi wa Majimbo, wengine wamepokea fedha na hawajapokea wito."-Katibu wa Chadema Kanda ya Kati Bi. Ashura Masoud.
KYELA, MBEYA, TANZANIA.
CHADEMA ni tumaini lililoletwa na Mungu na sasa ni mali ya kila mwananchi. Popote unapokanyaga nchini, bendera ya CHADEMA inapeperuka kwa kishindo huku ikileta tabasamu na matumaini mapya kwa wananchi. Wana-Kyela wanaipenda CHADEMA kwa dhati ya mioyo yao! #FreeTunduLissu ✌🏾
“Nakutakia upendo mwingi, rafiki yangu—nakukumbuka sana. Bado wewe ni miongoni mwa akili bora kabisa ambazo nchi hii inazo. Ninaendelea kukuombea—Mungu akupe ujasiri, nguvu na ustahimilivu wa kushinda changamoto zote zilizo mbele yako.”
Nduli Idd Amin Mama si alisema kwamba wamekubaliana na Ruto
Kuwa Ruto atawashughulikia Wanaharakati wa Tanzania waliopo Kenya.
Halafu Idd Amin Mama yeye atawashughulikia Wanaharakati wa Wakenya wakija Tanzania sasa imekuaje tena leo Ruto kampa za uso Idd Amin Mama tena kwenye uwanja wake wa nyumbani?
Kitaalam hii inatwaje?😂😂😂
Hii ni Nchi au ni nini? Yaani huyu anaweza kukurupuka kutoka nyumbani kwake na kupanga watu wanatakiwa kula au kutokula au watu wauziwe au wasiuziwe chakula!!!!
Tumefikaje hapa? Hawa wana utofauti gani na wakaloni? Huo unaoitwa uhuru ni upi kama OCD ndio anapanga hata matumizi ya mtu kufanya.
Wahuni ambao wamewahi kukamatwa, kushtakiwa na kuhukumiwa vifungo gerezani kwa makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Sh27 Bilioni ili kuachiwa huru walitakiwa kukiri kosa Mahakamani na kuingia makubaliano ya kulipa fedha (plea bargain) leo wapo uraiani wanapambana wa ‘wajane’ kuwahamisha katika makazi yao. Pameharibika sana.