Kuhama chama cha siasa sio kosa ila kuhama na kuzunguka majukwaani kuwaaminisha watu kilikuwa ni chama cha hovyo ni kujichoresha, jenga hoja ni value gani una add kwenye chama ulichohamia. Ni sawa na kuachika ila kutwa kumzungumzia Ex wako aliyekufundisha mapenzi
Hakuna mtu huwa anajisahau haraka kama Nape…
Bahati nzuri nilikua nae bungeni wakati Magufuli ameshughulika nae, alikua anatia huruma sana .. leo kasogea kwenye meza ya chakula ameshiba na anawatapikia Watanzania.
Kitu kimoja ninamshukuru kwamba amesema ukweli kuwa, Nchi hii hakuna uchaguzi.
Kinachonishangaza ni kwamba, inawezekanaje Watanzania wakakubali dharau, Matusi na kejeli ya kiwango hiki…
Bila kujenga uwezo wa wananchi kusimamia rasilimali maendeleo yatabaki kuwa msamiati kwa nchi yetu. Ni lazima tufanye uwezeshaji ambao utainua uwezo wa watu wetu kuwa sehemu ya usimamizi na unufaikaji wa rasilimali zetu badala ya kuwaachia wageni.
Kuwa sehemu ya historia mpya, jiunge na CHADEMA; chama kinachoamini katika kujengea uwezo Watanzania.
Mabadiliko tunayotamani yako mikononi mwetu.
Kwa wingi na umoja wetu, tujitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kuweka nadhiri ya kushirikia chaguzi kuanzia ule uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Ni jukumu letu sote kuamua kesho ya Taifa letu na vizazi vijavyo, tuwe sehemu ya kuandika historia mpya ya Tanzania kwa kuchagua viongozi wenye uwezo na dira ya kutufikisha kule tunakotamani kwenda.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe ametangaza kujiuzulu kufanya siasa endapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kitashinda angalau kiti kimoja tu cha jimbo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro wenye majimbo tisa (9) ya uchaguzi
Mbowe ametangaza ahadi hiyo Julai 05.2024 wakati akizungumza na wakazi wa Maore, wilayani Same, mkoa wa Kilimanjaro kwenye muendelezo wa mikutano ya hadhara ya chama hicho inayolenga kufikia mikoa yote ya kanda ya Kaskazini ikiwa ni muendelezo wa 'oparesheni +255 Katiba mpya' ambapo amesema msingi wa kuweka ahadi hiyo ni kutokana na ukweli kwamba mkoa wa Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini kwa ujumla wake CHADEMA imekuwa nguzo imara mara zote
Ametolea mfano uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo CHADEMA chini ya mwavuli wa UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) uliohusisha vyama vingine vitatu (3) wakati huo vya CUF, NCCR Mageuzi na NLD, vyama vya upinzani vilishinda majimbo saba (7) kati ya tisa (9) ya mkoa wa Kilimanjaro
Ametaja majimbo yaliyochukuliwa na upinzania kuwa ni pamoja na Same Mashariki, Rombo, Vunjo, Moshi vijijini, Moshi mjini, Hai na Siha, huku CCM ikiambulia majimbo ya Mwanga na Same pekee, hivyo kutoa wito kwa wakazi wa Same na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla wake kujipanga sawasawa ili kurejesha heshima hiyo kwa kuhakikisha wanashinda sehemu zote kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu (2024) na uchaguzi mkuu mwakani (2025)
Kuhusu mkoa wa Arusha, Mbowe ameeleza kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 CHADEMA iliibuka kidedea kwenye majimbo sita (6) kati ya saba (7) yaliyoko mkoani humo, ambapo CCM iliambulia jimbo moja (1) pekee ambalo ni la Ngorongoro, jambo ambalo amedai kuwa haoni dalili ya CCM kushinda tena kwenye jimbo hilo kwa kuwa wakazi wa Ngorongoro wameahidi kuipigia kura CHADEMA kutokana na kile alichodai kuwa shukrani ya chama tawala (CCM) na serikali yake baada ya kuchaguliwa ni kuwahamisha watu wa jamii ya Masai kutoka kwenye eneo lao la asili na kuwapeleka Msomera, wilayani Handeni, mkoani Tanga
Aidha, kwa upande wa mkoa wa Tanga Mbowe amebainisha kuwa mkoa huo umekuwa ngome ya CCM kwa miaka mingi kwani katika majimbo 12 ya uchaguzi yaliyopo mkoani humo CCM ilikuwa inashinda majimbo yote, hata hivyo amedai kuwa kufuatia mikutano 72 aliyoifanya hivi karibuni kwenye mkoa huo tathmini ya CHADEMA inaonyesha kuwa majimbo pekee ambayo CCM inaweza kushinda ni matano (5) tu huku CHADEMA ikiwa na uhakika wa 'kunyakua' majimbo yote yaliyosalia ambayo ni saba (7)
Mbowe ametoa wito kwa wakazi wa Same, mkoa wa Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini kwa ujumla wake kuhakikisha wanashinda chaguzi zote zijazo, yaani kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji baadaye mwaka huu (2024) na uchaguzi mkuu mwakani (2025) kuanzia kwenye viti vya Madiwani ili waweze kuunda Halmashauri, Wabunge na hatimaye nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kile alichodai kuwa chama hicho kinaenda kuunda serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwakani (2025).
Pamoja na changamoto zake Ruto ila angalau ana details za na anaijua Nchi yake vizuri anayoiongoza.. Kila swali ana majibu na anajua kujielezea vizuri..!!
VIDEO:
Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ametoa wito kwa Halmashauri na taasisi za serikali mkoani humo pale wanapofanya kazi na mtu au taasisi binafsi basi wahakikishe wanalipa stahiki za mtu au taasisi hiyo kwa wakati ili muhusika atimize malengo yake
Makonda amezunguza hayo wakati akitoa salamu za mkoa huo kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) kanda ya Kaskazini, hafla iliyofanyika jijini Arusha Julai 04.2024, ambapo ametolea mfano kuwa siku za nyuma alimuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum Halmashauri ya jiji la Arusha lakini mambo yaliyobainika kutokana na ukaguzi huo ni ya 'aibu'
Msikilizeni @rollymsouth akizungumza mengi kuhusu kadhia unazoweza kuzipata katika siasa za upinzani na mengine mengi.
Ingia https://t.co/jQMTsVU8Uw kutazama zaidi namna #SiasaZetu zilivyo kwa ujumla.