@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
serikali haina mamlaka ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, na katazo la katambi halina msingi wowote wa kikatiba au kisheria; ni katazo batili.
🎥: @BoniphaceEric:
jwtz likatae kutumiwa kutisha watu. naelewa kunaweza kuwa na ugumu wa kuiambia serikali hapana, but wanapaswa, jwtz si law enforcement organ. halihusiki kusimamia sheria. halipaswi kuingilia purely civilian stuff. jwtz lijichunge, heshima iliyonayo inatokana na kujua mipaka yake!
Kaka @zittokabwe habari yako!
Umekuwa mkali baada ya Mkuu wa Majeshi Uganda, Dikteta Muhoozi Kainerugaba kutoa agizo la kufunga vituo vya NTV na gazeti la Daily Monitor, ukisema ni shambulio dhidi ya uwekezaji wa Kitanzania.
Nyumbani kwetu hapa, kituo cha JAMBO TV (kinachomilikiwa na rafiki yako, John Marwa) kimefungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa siku 90 kwa kukiuka kanuni zao.
JAMII FORUMS, ilifungiwa kwa siku 90 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Septemba 2025 kwa tuhuma za kuchapisha maudhui ya kupotosha na kudhalilisha serikali. Hukupaza sauti kabisa.
Walistahili kupiganiwa ipasavyo kwa wewe kupaza sauti. Unatetea maslahi ya matajiri (tycoons) wa kisiasa waliowekeza nje ya nchi wakati huo ukipuuza ukandamizaji wa vyombo vya habari ndani.
Unakaa kimya wakati JAMBO TV inafungiwa hatua inayoumiza waandishi wa habari wa Kitanzania moja kwa moja, unasimama kutetea maslahi ya kampuni ya Mauritius inayofanya biashara Uganda.
Kwamba kufungwa kwa vyombo hivyo Uganda ni pigo kwa uwekezaji wa Watanzania? Muundo wa kampumi ya TAARIFA LIMITED unapingana na hoja yako ya msingi. Huo siyo uwekezaji wa Kitanzania.
TAARIFA LIMITED ni kampuni ya uwekezaji (investment holding company), ilichaguliwa kama muundo wa kisheria kwa ununuzi wa hisa kubwa katika kampuni ya Nation Media Group (NMG)
Ilitumika katika ununuzi wa hisa (54%) katika kampuni ya Nation Media Group (NMG), kupitia kununua NPRT Holdings Africa LTD kutoka Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED).
TAARIFA LIMITED, ambayo ilichukua 54% ya hisa zilizokuwa za Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) ndani ya Nation Media Group (NMG) imesajiliwa MAURITIUS siyo Tanzania
Kisheria na kiuchumi, uwekezaji uliosajiliwa katika maeneo yenye nafuu ya kodi (tax havens) kama MAURITIUS haunufaishi uchumi wa Tanzania moja kwa moja. Siyo ‘Tanzanian-owned businesses’
Hakuna namna fedha zinazozalishwa na vyombo hivyo nchini Uganda zitakavyoingia kwenye mfumo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuongeza akiba yetu ya fedha za kigeni (foreign reserves). HAIPO
Zinaishia akaunti za mabenki ya kigeni Mauritius au kwingineko. Mauritius inajulikana kwa kuwa na mikataba ya kuzuia utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Avoidance Agreements - DTAAs)
Inapotokea kampuni imeuza hisa zake au inapata faida, kodi ya faida inalipwa MAURITIUS (ambako viwango ni vidogo au ni sifuri) badala ya Tanzania au nchi ambako biashara halisi inafanyika.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haiwezi kudai kodi ya mapato (income tax) ya moja kwa moja kwenye miamala inayofanyika chini ya mwavuli wa kampuni iliyosajiliwa katika nchi ya Mauritius.
Kampuni ikisajiliwa Mauritius, iko chini ya sheria za makampuni Mauritius. Tanzania haina mamlaka ya kisheria (jurisdiction) kuhoji muundo wa utawala, akaunti za benki, uwazi wake wa kifedha.
Kodi, faida, na miamala ya kimkakati ya kampuni hiyo haiingii katika mfumo wa mapato ya ndani wa Tanzania. Huo siyo ‘uwekezaji wa Kitanzania’. Labda utafute jina lingine la kuita huo uwekezaji.
Faida inayopatikana kupitia mianya hii ya tax havens hairudi kama kodi ya kujenga shule, hospitali au barabara, ni pesa za mifukoni za wafanyabiashara wakubwa wa kisiasa na makada wa CCM.
Fedha hizi ndizo zinazotumika kufadhili harakati za kisiasa za ndani, ikiwemo kampeni za uchaguzi na matukio ya ukandamizaji wa kisiasa kama yale yaliyoshuhudiwa nchini mnamo Oktoba 29.
Badala ya kuhoji ni kwa namna gani uwekezaji huo wa Taarifa Limited katika vyombo vya habari vya Uganda unamsaidia mwananchi wa kawaida wa Tanzania, unakuwa mtetezi wa biashara za MaCCM.
Unapigania maslahi ya matajiri ambao wanatumia faida zao kudhoofisha demokrasia. Unasikitikia uwekezaji uliosajiliwa Mauritius usiokuwa na tija ya kodi au ajira ya moja kwa moja kwa Mtanzania.
MMM, Martin Maranja Masese, Masese
It would be a grave mistake for the U.S. Senate to address the October 29 massacre in Tanzania without also examining the role that @Meta played in helping the Tanzanian government conceal the killings and extend its repression beyond Tanzania’s borders.
When a foreign government can pressure a U.S. technology company into silencing critics, while the U.S. government itself appears unable to protect those voices, it raises serious national security and free speech concerns.
I was sitting in Los Angeles, California, yet I lost my voice on a major social media platform because of actions taken by the Tanzanian government through a U.S. tech company. The repression did not stop at Tanzania’s borders, it followed its critics into the United States.
No government should be allowed to use American platforms to suppress dissent, silence victims, or hide evidence of human rights abuses. Accountability must extend not only to those who commit atrocities, but also to those who enable their concealment.
At the very least META should face fines for its roles in the Tanzania massacre and human rights violations. Meta is an accessory after the fact.
@POTUS@SenateForeign@SFRCdems@SenTedCruz@SenatorShaheen@SecRubio@Meta@CNNAfrica@bbcswahili@LarryMadowo@tausilikokola@Liberatus80 We need to push for this as much as we are pushing for accountability from the Tz government. Bila kupata zile account za instagram hakuna movement ya maana Tufanya hapa.
SWAHILI
Itakuwa kosa kubwa sana kwa Seneti ya Marekani kujadili mauaji ya kikatili ya Oktoba 29 nchini Tanzania bila pia kuchunguza nafasi ambayo Meta ilicheza katika kuisaidia serikali ya Tanzania kuficha mauaji hayo na kueneza ukandamizaji wake nje ya mipaka ya Tanzania.
Wakati serikali ya kigeni inaweza kuishinikiza kampuni ya teknolojia ya Marekani kuwanyamazisha wakosoaji wake, huku serikali ya Marekani yenyewe ikionekana kushindwa kulinda sauti hizo, jambo hilo linaibua wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa taifa na uhuru wa kujieleza.
Nilikuwa nimekaa Los Angeles, California, lakini nilinyang’anywa sauti yangu kwenye moja ya majukwaa makubwa ya mitandao ya kijamii kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya teknolojia ya Marekani. Ukandamizaji huo haukusimama kwenye mipaka ya Tanzania; uliwafuata wakosoaji wake hadi Marekani.
Hakuna serikali inayopaswa kuruhusiwa kutumia majukwaa ya Marekani kukandamiza maoni tofauti, kuwanyamazisha waathirika, au kuficha ushahidi wa ukiukwaji wa haki za binadamu. Uwajibikaji haupaswi kuwahusu tu wale wanaotenda maovu hayo, bali pia wale wanaosaidia kuyaficha.
Angalau, Meta inapaswa kukabiliwa na faini kutokana na nafasi yake katika kuficha mauaji ya Tanzania na ukiukwaji wa haki za binadamu., Meta inaweza kuonekana kama mshirika aliyesaidia kuficha au kuwezesha vitendo hivyo baada ya kutokea kwake.
@MsigwaPeter Inaelekea @MsigwaPeter hujui kuwa mwenzakeo anatafuta pahala salama pa kuhamia (asylum home) immediately baada ya ICC indictment warrant kutolewa. Tayari nyumba imekaguliwa. Swali alilomeulizwa; unahama na dola kiasi gani? Swali hili limejibiwa na @LuhagaMpina juzi. Tzs57tr.
Hebu tuwaze nje ya BOX!!🤔
What if, ni mchezo wanautengeneza ili kumfanya VICEnt apate sympathy kwa wapiga kura….kisha ndio iwe next kete yao 2030!!🤔
Yes, coz sio mara yao ya kwanza kuyafanya hayo!! Wameshaitumia sana hii strategy huko nyuma na wakafanikiwa!!
Nikurudishe 2017
TAL alipopigwa pyuu pyuu 🔫
wengi walimchukia Banza kwa lile
tukio!!
Hisia zangu zinanambia #MasterMind aliitumia hii opportunity akamtuma Kizim-Job akampe pole TAL!!
sidhani kama ile move ya kwenda kumuona na kumpa pole TAL ilikuwa bahati mbaya ile, huwa always nahisi it was strategically planned na pengine mtoa pole hakujua kama ni mchoro anachorewa, yeye aliamini anatenda utu….but kuna watu behind the scene walipush ile move!!
Ili kumjengea sympathy,imani na upendo kwa raia, kwamba kati ya wanachama waandamizi wooote, ni huyu pekee kajitoa kwenda kumuona mgonjwa.
Basi huyu ana upendo sana!
Basi huyu atatufaa kutuongoza!
Huyu sio katili kama Banza!!
Kumbe MasterMind anasema huyu
Ni next kete yetu tutamtumia siku za mbeleni, tayari anauzika kwa wapiga kura!!
Haya miaka imepita….
vipi leo bado sio katili!!?🤔
Sasa nashangaa sana kuwaona baadhi ya wanafamilia wakiingia kwenye huu mtego tena mapema sana, bila hata kuwaza nje ya box!!
Tena wengine ni watu senior na very influential kwenye siasa na harakati!!
Wanaanza kumpongeza VICEnt kuona huruma, kumfanyia PR na kumu-endorse kwa raia….Pasi kujua kufanya hivyo ni kurudia makosa yaleyale ya kujikuna Nyashi kisha unakata kucha kwa meno!!
Ni kweli VICEnt anaonekana kuwa mtu poa currently, lakini shida ni familia ileile!!
Iko hivii…..hawa jamaa ni very smart na calculated!
Wanajua fika now wako kwenye nyakati ngumu sana kujiuza kwa wananchi kutokana na waliyoyafanya….Nyama ngumu kwelikweli!!
Wana changamoto kubwa
ya who is next? ambaye wata msimamisha na raia wakampokea na kumkubali bila makwasukwasu yoyote!!
Hapo sasa kwenye Who is next, ndiyo nahisi #The_Master_Mind huwa anakujaga na mchoro wa kutafuta exit!!
Kwamba watengeneze beef/vita/misunderstandings wao kwa wao ndani kwa ndani, then habari zitoke nje kwa raia….kuwa kuna mpasuko ndani ya chama!!
Then ile kete wanayoitaka wao ndio ionekane kwa raia kama ndiyo inaonewa ndani ya chama au kama ndiyo shujaa inasimama na raia!!
Na raia tulivyo na mtindio wa ubongo tunajaa kwenye huo mfumo!
Tena wakati mwingine #MasterMind anaweza akachezesha huu mchoro bila hata kuwashirikisha wahusika wakuu, yaani main characters wakawa wanapasuana kiukweli, kumbe kuna mtu behind the scene anawachezesha filamu!!
Anagusanisha nyaya, anapigisha cheche bila wao kujua….
KUWENI NA MISIMAMO
KUWENI NA KUMBUKUMBU
WAZENI NJE YA BOX
MSIJAE KIZEMBE
Nways labda niko wrong na hisia zangu!!
Tatizo naangalia sana movies za watu waBad wanavyoRemote Gavoo na Viongozi!!
zinaniharibu sana!!
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inafanya kazi ya kuchochea machafuko.
Sisty Nyahoza aliekwenda kwa marehemu mama Komu na kumshawishi kusaini karatasi ya kufungua kesi ambayo ilifungia chama chetu kufanya kazi siku 309..
Madhara mengine walitaka kukifuta chama kupitia kesi hiyo ya Said Issa.. kwa uwezo wa Mungu tumeshinda..
Sasa Sisty huyo huyo na ofisi hiyo hiyo ambayo inafanya kazi ya kuhujumu chadema usiku na mchana tena wazi kabisa. Inatuandikia barua kila baada ya mkutano na kila neno tunalosema… Maneno pekee tunayoweza kusema tusiandikiwe barua na Sisty ni kumsifia Samia na serikali yake dhalimu ambayo haikuchaguliwa.
Kwa kifupi ofisi ya msajili itaingiza Nchi hii kwenye machafuko ya kisiasa..
Chadema ni taasisi ya Watanzania na Watanzania watailinda dhidi ya hujuma zote.
Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi amemuelezea aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kama kiongozi ambaye alimuamini pamoja na kuwa walitofautiana mwaka 2015.
Dkt. Nchimbi anaeleza kuwa aliamua kupumzika siasa na aliwahi kumueleza JPM kuwa hayupo tayari kufanya siasa hata alipotaka awe mbunge wa kuteuliwa alikataa.
Anaeleza kuwa baadae JPM alimpigia simu na kumuuliza kama hajachoka kupumzika akajibu kuwa anaendelea kupumzika ndipo kesho yake akashangaa kusikia ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil.
Anaeleza kuwa baada ya uteuzi huo JPM alimtumia meseji Dkt. Nchimbi akimuambia "haijalishi yaliyopita yamepita wewe bado ni kijana siwezi kuharibu future yako" amesoma meseji hiyo Dkt. Nchimbi.
Taarifa: Ili kumuunga mkono Mwenyekiti wetu Lissu na struggles zake gerezani, nimeamua kumuiga style yake mpya ya nywele…Sitachana wala kunyoa nywele zangu mpaka atoke jela akiwa HURU✌🏾✌🏾
#LiMwenyekiti#KatibaMpya#FREELISSU
STOP USING PROPAGANDA OVER THE LIVES OF TANGANYIKANS.
No nation is oppressing us. Our problems are the result of our own ignorance and cruelty.
We have abandoned accountability founded on the rule of law and the Constitution, and have turned ourselves into untouchable gods.
We cannot continue killing and attacking thousands of people and then claim to be sovereign; that is ignorance born out of a lack of understanding.
Sovereignty in any nation exists within civilized limits recognized by the international community.
IF WE ARE NOT READY TO HOLD OURSELVES ACCOUNTABLE, THEN THE INTERNATIONAL COMMUNITY WILL HOLD US ACCOUNTABLE.
Truth, Justice, and Accountability are the only foundations upon which this nation can be rescued from its current crisis.
BAK MWABUKUSI
@MsigwaPeter We mzee njaa imekufika ubongoni... ulienda CCM kutafuta madaraka baada ya kukosa madaraka chadema... karibu ila uishie kuwa mwanachama wa kawaida... uaminiki we mzee
Je, una picha au video ya mtu akiuawa au aliyefariki wakati wa uchaguzi Tanzania uliofanyika tarehe 29 Oktoba?
Weka picha/video hiyo hapa na jibu maswali yatakayofuata. Wasaidie Human Rights Watch kurekodi kilichotokea. https://t.co/bWZtUtJex2