Uwezo wa KIKEKE kuhoji UMESHUKA sana aisee..!
Kikeke wa BBC hapa ningetegemea maswali kadhaa kama haya;
1. Uchunguzi wa KUSHAMBULIWA kwa faza Kitima umefikia wapi?
2. Mdude , soka, Mlay, tunaenda mwaka wa pili kupo kimya.
3. Polepole aliekuwa BALOZI mpaka leo hakuna majibu ya kutekwa kwake kwanini?
Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanatakiwa kuulizwa angle ya UTEKAJI, leo mjadala unaisha juu juu tuu kama wapo VILABUNI.
Siku moja Clouds Media wawaite wasanii na kutoa public apology. They have killed so many talents, kwa maelezo ya Hussein ilikuwa ukidai pesa yako tu ni kosa!
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa wito kwa viongozi wa dini kuacha kuwapa sakramenti watu wanaojihusisha na ukandamizaji na badala yake waanze kuwafukuza kanisani na misikitini.
Mwabukusi ametoa wito huo leo mkoani Singida alipokuwa akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa Alute Mughwai Lissu.
Ameeleza kuwa kanisa limekuwa mwepesi kuwahukumu watu wanaotenda dhambi zingine kama vile uzinzi, lakini wanaowakandamiza wenzao wamekuwa wakiachwa wakiendelea kupata huduma za kiroho bila kukemewa.
Katika hatua nyingine, Mwambukusi amesema chama hicho kinashirikiana na mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kwa kuzingatia maelekezo ya Lissu mwenyewe ili kushughulikia kwa haraka maombi yake ya dhamana na usikilizaji wa rufaa dhidi ya hukumu yake.
"Sisi kama TLS tutaendelea kuwasiliana na familia yake kwenye hatua zingine zinazofuata lakini vilevile tutashirikiana na mawakili kwa kuzingatia maelekezo ya Tundu Lissu mwenyewe. Sisi Baraza la Uongozi na mawakili wake Tundu Lissu kushughulikia swala la rufaa kwa haraka lakini vilevile maombi yake ya dhamana huku tukisubiri usikilizwaji wa rufaa," ameeleza.