Kihistoria muda wa kitu ukifika hauwezi kubadili tena.
Tangu zamani..
Muda wa biashara ya utumwa kukomeshwa ulipofika haikuwezekana kuzuia tena.
Muda wa uhuru ulipofika wakoloni walilazimika kuachia hizi Nchi, hata walipojaribu kutumia mabavu haikuwezekana..
Moyo wa wananchi umeishakataa CCM, Muda wa ccm umekwisha, bunduki, mabavu, mauji na utekaji haviwezi kubadili hali hiyo.
Kucheza na hisia za wananchi na mioyo ya watu ni kucheza na moto.
Uhalali wa serikali dhalimu hauwezi kuletwa na bunduki.
EXENOPHOBIA kama inayoendelea Afrika ya Kusini ni hofu dhidi ya wageni na msingi wake unaeleweka lakini hapa Tanzania kuna TL-Phobia ni hofu dhidi ya Tundu Lisu.Uadilifu wake ,Ukweli wake na Uzalendo wake.
Ya kwanza ina weza kueleweka au kuzungumzika hii ya pili ni zao la Ujinga na Kutofikiri sawasawa. Ni aibu kwa Taifa.
BAK MWABUKUSI.
#TajiriLaKihaya
KUNA MASWALI MAKUBWA YANAYOPASWA KUJIBIWA MUHIMBILI NA JKCI.
Leo familia yetu imepoteza mdogo wetu. Moyo wangu umejaa huzuni, uchungu na maswali mengi ambayo hadi sasa hayajajibiwa.
Siku ya kwanza nilipofanikiwa kumpeleka mdogo wangu JKCI na kupata chumba cha VIP, nilifurahi sana. Niliona kama tumepata mwanga wa matumaini. Baada ya vipimo, tuliambiwa tatizo lake la moyo lilihitaji upasuaji mdogo tu na angeweza kuendelea na maisha yake kawaida.
Tukaahidiwa upasuaji ungefanyika ndani ya siku mbili au tatu.
Lakini siku zikageuka wiki.
Kabla hata ya kulazwa, tulikuwa tumepambana kwa zaidi ya mwezi mzima tukizungushwa kutoka leo hadi kesho. Mara daktari hayupo, mara jopo la wataalamu halijakaa, mara kipimo kirudiwe, mara tusubiri dawa zifanye kazi kwanza. Kila siku ilikuwa ni ahadi mpya na tarehe mpya.
Baada ya kulazwa tuliamini safari ngumu imekwisha. Lakini ndipo mateso makubwa zaidi yalipoanza.
Mdogo wangu aliingia hospitalini akiwa bado anaweza kutembea, kuongea, kula na kujitambua. Kila siku tulisubiri upasuaji ulioahidiwa, lakini haukufanyika. Badala yake hali yake ilianza kuzorota mbele ya macho yetu.
Wiki moja ikapita.
Wiki mbili zikapita hadi wiki tatu
Hakukuwa na upasuaji.
Kulikuwa na sababu mpya kila siku.
Kisha tukahamishwa kutoka chumba tulichokuwa tumepewa kwa madai kuwa kingefanyiwa fumigation. Lakini usiku huo huo mgonjwa mwingine akawekwa kwenye chumba hicho. Hadi leo hatujui ukweli ulikuwa nini- lazima UFISADI ULITUMIKA HAPA!
Tulihamishiwa chumba kingine JAPO kilikua VIP… ila hakikua kwenye standard sawa!
Hata nakumbuka kuna Daktari wa Kihindi alikuja kusoma vipimo akasema ile MONITOR haipo sawa! Mapigo ya moyo na oxygen haisomeki kwa usahihi…
Sasa kwa nn tulihamishwa chumba? Kutoka chumba kizuri kuja hiki?? Kwa nn kile tulichokuwepo alipewa mwingine usiku huo tumehamishwa? CORRUPTION!
Baada ya hapo hali ya mdogo wangu ilizidi kuwa mbaya zaidi. Akapoteza nguvu, akashindwa kuzungumza, akashindwa hata kuwatambua watu waliomzunguka.
Tulikuwa tunauliza maswali. Tulikuwa tunaomba msaada. Tulikuwa tunaomba hatua zichukuliwe haraka.
Lakini muda uliendelea kwenda.
Leo asubuhi mdogo wangu amefariki dunia.
Siandiki haya kwa hasira pekee. Naandika kwa maumivu ya familia iliyokuwa na matumaini makubwa ya kumuona mpendwa wao akirudi nyumbani akiwa mzima.
Kama kweli kulikuwa na uzembe, kucheleweshwa kwa huduma, ukosefu wa uwajibikaji au mifumo mibovu ya utoaji huduma, basi kuna haja ya uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa. Maisha ya Watanzania yana thamani. Wagonjwa hawapaswi kupoteza maisha wakisubiri tarehe nyingine, kikao kingine au ahadi nyingine.
Tunataka majibu.
Tunataka uwajibikaji.
Na zaidi ya yote, tunataka familia nyingine isipitie maumivu tuliyoyapitia sisi.
Kama hapa ni VIP… je wagonjwa wa kawaida wanapata huduma gani???
Pumzika kwa amani mdogo wangu. Tulipambana kwa kila tulichoweza. Mungu akupokee katika makao ya milele. 💔🕊️
Mange Kimambi is not a politician hajui chochote,akili ya Mnyika na Chadema ni kubwa wacha wananchi ndiyo waongoze maandamano na siyo CDM vinginevyo watajinasa. Polical Science is a science
Hii serikali haijifunzi wala haijali yale yaliyotokea!!
Jana wasafi, waziri anahojiwa anaulizwa sababu za utekaji anatumia dakika 10 kuongelea sababu tofauti tofauti halafu the main one anai-skip!
Anakumbushwa na Ade kuhusu sababu za kisiasa, anasema kauli chonganishi za kisiasa zinaweza kuwa sababu!!
So adhabu ya mtu anayetoa kauli chonganishi za kisiasa ni kutekwa na kuuliwa, hakuna adhabu nyingine!
Imagine na huyo ndio waziri wa Home Affairs!!
Majibu kama haya ya kujifanya hujui tatizo! Ndio hujaza vijana hasira na chuki na kuamua kuingia barabarani then baadae mnasema wameshawishiwa na watu wa nje
ILI TAIFA Lipone linahitaji mambo Muhimu 5
1. Tume ya Ukweli,Haki na Uwajibikaji kuhusiana na matukio ya Mauwaji na upotezwaji wa watu na Miili Kabla,wakati na baada ya uchaguzi
2.Kuachiliwa kwa mahabusu wote ,wafungwa wakisiasa ikiwamo kuachiliwa kwa Wakili Tundu Antipas Lissu.
3.Kuhuishwa kwa sheria ya Uandikwaji wa Katiba Mpya na Kuweka utaratibu utakao anzia pale Tume ya Warioba ilipoishia.
4.Kuruhusu Uchunguzi huru wa Kimataifa kuhusiana na matendo yote yanayohusiana na ukiukwaji wa haki za Binadamu na haki za kiraia.
5.Raia wote kujikana kukataa rushwa,hofu,woga,kukataa hila na ghilba za kisiasa na kutanguliza maslahi Mapana ya Taifa mbele
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI UTALIPONYA TAIFA.
BAK MWABUKUSI.
Kesi ya uongo ya mgogoro fake wa mali, ni kesi ya Msajili wa vyama..
Marehemu mama Komu alituelezea namna ambavyo Sisty Nyahoza, Msajili msaidizi akiwa na mtu anaitwa Salehe Bohora, walivyomfuata nyumbani kwake na kuomba aweke jina kwenye kesi..
Marehemu Mama Komu alituambia hata malipo ya mawakili yalilipwa na Salehe Bohora na bwana Sisty, kwa mujibu wa mama Komu huyu bwana Salehe alitumwa na Rais.
Mtakumbuka pia kuna mtu alijiita Mwenyekiti wa Chadema Mwanga.. huyu nae alikua analipiwa mpaka mahali pakukaa na ofisi ya msajili, kupitia ofisi hiyo hiyo ya msajili walidai kutotambua uongozi halali wa Chama, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na wajumbe wa kamati kuu ya Chama.
Hii kesi ilifunguliwa siku hiyo hiyo ambayo Mwenyekiti wetu alikamatwa na kupewa kesi ya uhaini.
Kesi hii ilipangwa kwa Jaji mwingine awali lakini katika mazingira tata ikapelekwa kwa jaji Mwanga.
Jaji Mwanga tangu awali alionekna wazi kutofuata sheria, kuendesha Kesi kibabe na kudharau kila hoja iliyotaka upande wetu… alikua na maelekezo ya wazi na alionesha upendeleo uliovuka mipaka..
Kupitia kesi hii shughuli za Chama zilizuiliwa kinyume cha sheria kwa siku 309, Mpaka mahakama ya rufani ilipofuta zuio fake..
Kupitia Hilo zuio watu wetu walipigwa mara nyingi na polisi kila walipojaribu kufanya shughuli za chama.
Tutakumbuka siku ya wanawake duniani namna wanawake wa Bawacha walivyopigwa mpaka kanisani kwasababu ya zuio hili haramu..
Mali za Chama zimeharibika, Mimi pamoja na Katibu mkuu tulifunguliwa kesi ya contempt of the court. Kutokana na Amri hizi hizi.
Jaji Mwanga alipuuza hukumu ya mahakama ya rufani ambayo ilikua inamlazimisha kutokifungia Chama chetu..
Nani atalipia maumivu, usumbufu, matatizo ya makusudi, nani atalipia hasara zisizolipika za kuzuia chama mda wote huu kufanya kazi zake..
Tunafurahia leo, lakini Fikiria damage zote hizi hazikutakiwa kuwepo, zilifanywa kwa makusudi kwa manufaa ya Samia na Ccm.
Bado msajili anatufuata fuata na kutuandikia barua baaada ha maumivu yote haya aliyotusababishia..
Kama ilivyo kesi ya uongo ya kumtesa Mwenyekiti wetu ndivyo zilivyo zote hizi ni kwa manufaa ya Samia wala sio Nchi..
Tuacheni tufanye wajibu wetu wa kisiasa. Hatutapiga magoti wala kununuliwa.
Sidhani kama kuna Ubaya mtu kulipwa kushawishi watu wajitambue,,, shida ni watu kulipwa kutetea uovu ili watu wasijitambue
Au labda mimi ndio sielewi,,, kuna watu walilipwa kushawishi watu wafanye vurugu?? Naombeni nifahamishwe
@EsirEid Kaka Uyo kikatuni miyeyusho nilitegemea ataongea tusiyo yajua na kutupa hint muhimu za maswali magumu kwenda kwa wanaharakati. Leo ndo kaharisha kabisa
@EsirEid Sijui Mzito Anakwama Wapi
Vunja Baraza La Mawaziri
Fukuza Wakuu Wote Wa Ngazi Za Usalama
Timua Ma Afisa Wote Wa Ikulu
Mwachie Lissu
Futa Kesi Zote Za Kisiasa
Wape Ruzuku Na Malimbikizo Yao
Waruhusu Wafanye Mikutano Ya Kisiasa
Kwenye Kuteua Teua Sura Mpya Kabisa.
Ruhusu Hoja.