This Mother’s Day, while some children are held in loving arms, others live only in memory.
Every child, everywhere, has the same right to life, safety, and a future.
Baada ya miaka 35, tumelazimika kufanya tena tathmini ya mfumo wa kodi nchini ambapo leo nimepokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi Nchini niliyoiunda Julai 2024. Tume imewasilisha mapendekezo 284 yanayolenga kuboresha mfumo wa kodi ili uendane na mabadiliko ya kiuchumi, kiuwekezaji na kibiashara duniani.
Maboresho ndiyo maendeleo. Kwa muktadha huo, tumechukua hatua hii kwa malengo makuu mawili; kwanza, kupanua wigo wa walipakodi, ili kila mwananchi ashiriki kujenga uchumi wa nchi yetu, na pili, kutambua kuwa mfumo bora wa kodi ni muhimu katika kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani, sawa na malengo ya Dira 2050.
Ninawashukuru wananchi wote kwa kutoa maoni kwani mmeshiriki kuamua hatma ya leo na kesho yetu na Taifa letu. Aidha, katika utekelezaji wa mapendekezo hayo, tutashirikiana kikamilifu na sekta binafsi, wananchi na wadau wengine ili tufanikishe lengo la ukusanyaji rasilimali zinazohitajika kwa ustawi wa watu na maendeleo ya nchi yetu.
Karibuni Tanzania.
Karibuni Nyumbani.
Leo nimejumuika na Marais wa nchi na Wawakilishi wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha.
Miaka 26 tangu kurejeshwa kwa umoja huu, umeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha nguvu za nchi zetu kama ndugu, kuongeza sauti ya pamoja katika masuala mbalimbali, na kujenga mustakabali wenye mafanikio kwa wananchi wa Afrika Mashariki.
Leo tumeandika historia nyingine kubwa kwa Taifa letu kwa kuzindua Makao Makuu ya kwanza ya Ulinzi wa Taifa mkoani Dodoma. Hatua hii imekamilisha maono ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya mwaka 1964 wakati Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilipoundwa.
Majengo haya ambayo tumeyajenga kwa fedha na wataalamu wa ndani ni uthibitisho wa ukomavu wa Taifa letu katika kupanga, kuamua na kutekeleza kwa ufanisi miradi mikubwa. Kuziweka pamoja ofisi za JWTZ na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kutaongeza tija na ufanisi wa kazi, na ni kielelezo cha dhamira yetu ya kujenga taasisi imara za kulinda uhuru, mipaka, rasilimali na watu wetu.
Mafanikio ya mipango tuliyojiwekea yanategemea sana uwepo wa amani na utulivu. Hivyo, wito wangu kwetu sote ni kuendelea kuimarisha ulinzi, usalama, umoja na mshikamano wa nchi yetu.
🇷🇺🇹🇿 Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mhe. Sergey Lavrov amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mhe. Mahmoud Kombo aliyefika Moscow akiwa na misheni maalum.
✉️ Waziri Kombo amewasilisha ujumbe wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia, kwa Mhe. Rais Vladimir Putin.
Karibu Tanzania Mheshimiwa Rais.
Ikulu, Dar es Salaam leo nimempokea Kaka yangu, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni. Ziara yake hii nchini ikiwa ni siku chache tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda inaonesha namna Uganda inavyothamini ushirikiano wake na nchi yetu, ambao umejengwa katika misingi ya udugu, ujirani na kuheshimiana.
Tumejadili maendeleo ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Mradi huu ambao ni moja ya vielelezo vya uhusiano wetu, unatarajiwa kuanza kufanya kazi Julai mwaka huu. Vilevile, tumejadili mpango wa kuunganisha reli (SGR), ujenzi wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia na mafuta, kukuza matumizi ya bandari za Tanzania, ulinzi na usalama, pamoja na namna bora ya kukuza biashara baina ya nchi zetu kwa kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi.
Leo jioni nimewasili Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo nitaungana na viongozi wengine katika uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS) pamoja na Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit - WGS) 2026 unaolenga kujenga mwelekeo wa namna serikali zinavyoweza kuhimili mabadiliko ya dunia na kuchochea maendeleo endelevu.
Ushiriki wa Tanzania katika majukwaa haya ni kielelezo cha uthabiti wake kisiasa, na dhamira yake ya kuendelea kuvutia uwekezaji toka ndani na nje ya nchi, utakaozalisha ajira zaidi na kuchagiza maendeleo yetu. Aidha, ni utekelezaji wa Dira 2050 pamoja Sera mpya ya Mambo ya Nje katika Diplomasia ya Uchumi.
Hotuba yangu kwa Taifa tunapomaliza mwaka 2025 na kukaribisha mwaka 2026.
Ninawatakia nyote kheri ya Mwaka Mpya 2026. Mwenyezi Mungu atujalie ukawe mwaka wa baraka na mafanikio zaidi kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mungu ibariki Tanzania.
Ninaipongeza timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars kwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.
Heshima hii kubwa kwetu ni matokeo ya maandalizi mazuri na kujituma kwenu katika kila mchezo. Mmeandika historia kubwa kwa Taifa letu na mmeleta furaha kwa Watanzania wote. Hongereni sana.
Ninawatakia kila la kheri katika michezo inayofuata.
WASIRA: VIJANA MSIKUBALI
KUTUMIKA KUHARIBU NCHI
*Asisitiza wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura nchi ipo salama
NA MWANDISHI WETU, TARIME
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewataka vijana kukataa kutumika kwa maslahi ya wengine wenye nia ovu, huku akiwahakikishia wananchi kuwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu utafanyika kwa amani na salama.
Amesema yapo baadhi ya mashirika ya kimataifa yanatamani kuona amani iliyopo inavurugika, lakini hawatafanikiwa kwa kuwa Chama kimesimama imara kulinda amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.
Wasira ameyasema hayo kwa wakati tofauti leo Oktoba 16, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wakiwemo wa mashina katika vikao vya ndani vilivyofanyika Tarime mjini na vijijini, wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
"Nataka niwaambie Watanzania uchaguzi utafanyika tarehe 29 tena kwa amani, na yule ambaye anaota amani itapotea anapoteza wakati wake, kwa sababu CCM bado tunashikilia dola, amani itakuwa tele, waambieni wapigakura hakuna mtu atakayefanya chochote.
Amesema yapo baadhi ya mashirika ya kimataifa yasiyotaka kuona amani inaendelea kuwepo nchini na yapo tayari kutoa fedha kuvuruga utulivu wa Watanzania.
"Yapo baadhi ya mashirika ya kimataifa yana matatizo na mengine hayataki kuona amani ya nchi yetu, yapo tayari kutoa fedha ili amani itoweke," amesema.
Aidha, Wasira amewataka vijana wakatae kutumika kuleta vurugu kwa kuwa ustawi wa maendeleo yao na nchi kwa ujumla unategemea amani na utulivu.
== ==
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2025.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi Ilani ya Uchaguzi wagombea Ubunge wa Majimbo mbalimbali mkoani wa Kagera mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Bukoba mjini tarehe 16 Oktoba, 2025.
Sehemu ya Wananchi wa Bukoba mjini waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2025.
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2025.
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2025.
Sehemu ya Wananchi wa Karagwe mkoani Kagera waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 15 Oktoba, 2025.