أحياناً نتمنى أن تكون أحلامنا حقيقة، وأحياناً نتمنى لو كانت حقيقتنا حلماً
Wakati mwingine tunatamani ndoto zetu zingekuwa kweli. Na wakati mwingine tunatamani ukweli ungebaki kuwa ndoto.
Tumuombe Mwenyezi Mungu atujalie ni katika wale watakao tajwa kwa uzuri baada ya mauti yetu! Isije ikasemwa; Bora hata amekufa!
Rabbi! Na ufanye mzuri mwisho.
Kila msafiri huandaa zawadi ya aendako, mauti nayo yatuhitajia hata kwa uchache zawadi, kwani huja ghafla mmno!
Na bora ya zawadi, ni kumcha Allah (Azza wa Jallah)
Mwisho wa mambo, ni mwisho mzuri.
Hata kabla ya adhana misikiti ilikuwa tayari imejaa waja wa #Allah mtukufu! Sijui waja wa #Allah wamekipata walichokuwa wakikifuata?
Vipi mkulima unayaacha makulima yako/ mazao yako yakiwa tayari kuvunwa? Rejea ukavune siku10 bora
#Ramadan 20
Pamesemwa; Pambanua ukipendacho, ila ustakabari, gombana na yoyote, lakini usimdharau abadani, ghadhibika upendvyo, lakini usimdharau yoyote.
Tuhifadhi ndimi zetu, ndani ya ramadan na nje.
#Ramadan 22.
Na wala hatusubirii mbadala isipo kuwa kwa Mola wa waja. Ee Mola tunakuomba yaliyo mazuri na kheri kwetu, nayo ni umri mzuri, riziki ya ukarimu na halali, na matendo mema, na mwisho mzuri.
Mshairi anasema; Katika haya maisha tarajia kitu chochote kutoka kwa mtu yeyote na wakati wowote ule. Watu wote waliotuzunguka ni mbegu, tunawapuuzia aina zao, lakini tunagundua uhalisia wao tunapo waotesha kwenye maisha yetu, wanaweza kuwa waridi au mwiba katika maisha yetu.
Ee Mola wetu Mlezi! Tunakuomba utujalie sisi ni katika wale ambao watakao ambiwa;
Hii ndio Pepo mliyokuwa mkiahidiwa, ingieni humo na mustarehe kwa yale mema mliyokuwa mkifanya duniani.