Tukiwa Arusha, pahali panaitwa Uzunguni City Park, tunapata chakula cha mchana kabla ya kuelekea katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la soko kuu..
Akapita mama mmoja umri wa miaka 55 fulani hivi kwenda juu.. yule mama alipotuona, akasimama, akasema “Mungu wangu, nimefurahi kuwaona”
Akatusogelea na kuingia mfukoni kwake na kutoa kiasi cha shilingi 60,000 akamkabidhi John Heche. Akatuombea na kuondoka.. kidogo akarejea tena..
Akasema ndugu zake hawawezi kumuamini kama amekutana na watu wa CHADEMA bila picha, akatoa simu yake akiwa na furaha sana, akapiga picha..
John Heche akachukua ile Tsh. 60,000 akampa msaidizi wake akamuelekeza iwekwe yote katika akaunti au namba za chama za TONE TONE na aletewe risiti..
Tunataka kunyanyuka, amekuja mwingine, mwanaume, umri wake kama miaka 40 kwenda juu.. akafurahi kutuona pale, na imekuwa siku nzuri kwake…
Akasema bili yote ambayo tumetumia hapo, atalipa mwenyewe, tusitoe hata buku… bili kama Tsh. 265,000 hivi… akatoa na kuongeza ‘tip’ kwa muhudumu..
Mwenzake akasogea na kumuuliza, bili hii ningepewa mimi. Muhudumu akasema ishalipwa yote. Jamaa akauliza kwani kiasi gani? Aliyelipa akadakia….
“Kidogo, hii bili elfu tano tu, yote nimemaliza”…. Aah! katoa jiwe tatu kasoro lakini anasema ni bili ndogo tu ya buku tano.. upendo mkubwa sana kwa CHADEMA..
Akapiga picha nyingi na kila anayempenda na kati yetu, ikawa siku ya furaha sana. Hatukushangaa sana kwa kuwa hiyo ni kawaida kila sehemu tunapokwenda..
Hapo ni mchana, bado usiku, bado maeneo mengine tunayopita, story za hivi ni nyingi… unalipiwa bili za vinywaji na chakula, kwa upendo wa CHADEMA..
Kitu ambacho wanaokuwa viongozi hawaelewi ni kwamba, wanapendwa na umma kwa kuwa wapo ndani ya CHADEMA, wakiondoka na upendo umekwisha.
Watanzania wanaipenda CHADEMA na wanaiona CHADEMA na viongozi wake ni mali yao. Nashindwa kumuelewa mtu anayeamua kuiharibu CHADEMA.
Chama pekee ambacho Watanzania wanajivunia na kujiona ni sehemu yake ni CHADEMA. Wanaamini CHADEMA ni UHURU na MABADILIKO ya KWELI.
Usichoke kuchangia harakati za uendeshaji wa CHADEMA popote. Endelea kuchangia TONE TONE tumuoneshe msajili SISI NI NGUVU YA UMMA.
Ingiza namba ya kuchangia 0744446969; Jina - CHADEMA HQ. Weka TONETONE lako hapo kwa maslahi ya chama chetu na tuendeleze harakati.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
@IAMartin_ Mwaka juzi kwenye operation 255 kasulu, nikaongea na Mwalimu tukiwa banda la bidhaa za CDM anafuatilia mauzo. Nilikuwa nimechukua tisheti na katiba, nikamuomba picha na number akakataa. Jioni nikakutana na Mrema na Kigaila pale highway nao wakanipuuza wakati nilitaka kulipia bill
Hebu fikiri uko ndani ya lifti na Mkurugenzi Mtendaji wa benki kubwa hapa Tanzania—tuseme CRDB!
Wewe unamfahamu, lakini yeye hakufahamu. Hata hivyo, unataka kujenga network naye!
Je, utaanzaje mazungumzo? Na lini utaanza?
Uzi:👇
The end of a COVERSATION
REMAIN in Power Ngugi wa Thiong’o ! Thank you for your Master Pieces…The River Between, Petals of Blood, Wizard of the Crow and so many more !